Maiti zaidi za wana CHADEMA zaokotwa Igunga!

MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
999
815
Maiti za wanawake wawili zimeokotwa jana katika msitu wa kijiji cha Ulaya, Kata ya Nkinga wilayani Igunga zikiwa zimeharibika vibaya.

Wakati uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaeleza kuwa mmoja wao ambaye ni mama wa makamo, anajulikana kuwa ni shabiki mkubwa wa Chadema na Mhamasishaji maarufu mwenye ushawishi wa kisiasa, alikuwepo siku Helikopta ya CHADEMA ilipotua Nkinga na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa ajili ya kampeni siku ya J'4 kabla J'2 ya uchaguzi, Baada kumalizika mkutano huo muda wa jioni sana, mama huyo alikuwa akirudi kijijini kwake, lakini kuna kikundi cha vijana wa makambi wa CCM walionekana wakimfuatilia, wakiwemo watoto wawili wa Diwani wa kata hiyo ambao ni maarufu kwa ujambazi lakini mara zote wanakingiwa kifua na baba yao kwa wadhifa wake wa udiwani, mama huyo hakuonekana tena hadi maiti yake ilipookotwa jana msituni ikiwa bila nguo (zimetundikwa juu ya mti) na imeharibika vibaya na kuliwa na wadudu.

Upande wa pili wa barabara alipookotwa mama huyo kulikutwa maiti nyingine ya mwanamke mwingine aliyeuawa kwa staili ileile na kuachwa bila nguo, ila kutokana na kiwango cha kuharibika kwake inaelekea aliuawa siku tofauti na kuja kutupwa hapo, pembeni yake wauaji hao waliweka kitambulisho cha mtu wanaetaka ahusishwe na mauaji hayo, dalili zote zinaonesha wauaji ni walewale, inasemekana mwanamke huyo ametokea kata jirani ya Ndembezi.

Polisi zaidi ya kuchukua maiti hizo kwa pamoja na kuondoka nazo haijasema lolote, jitahada kubwa zinafanywa kulifunika suala hili liishe kimyakimya lisije likaleta kashfa kubwa ya mauaji kwa chama tawala, baada ya Nape Nauye kuahidi kuwa watafanya hivyo na wasilaumiwe kwa kuwa kuna kijana wao amemwagiwa tindikali.

Inaelekea kuna maiti nyingi zaidi hazijapatikana maporini na nyingine zimefukiwa huku ndugu zao wakidhani wamesafiri au wako kwenye mihangaiko, lakini kwa kuwa La Kuvunda Halina Ubani, basi kitaeleweka tu!
 
Sasa hili si jambo la kunyamazia wachukueni watu wa haki za binadamu na viongozi wa CDM waende kusimamia hili ili wananchi wasema yote wanayoyajua pia dunia lazima ielewe na lazima lipigiwe mbiu kubwa
 
Please hivi tunamuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa utawala wa sheria na haki, yaani maisha ya Mtanzania yako mashakani kwenye Nchi yake mwenyewe kiasi kuwa hakuna anaye yalinda.

Maumivu ya kichwa huanza mara moja!. What goes around comes around.

Damu za marehemu hao kama ni juu ya dhamana za kisiasa basi walihohusika wanatudanganya sisi wanadamu lakini dhambi kuu za matendo yao anaezijua ni Mungu na hukumu yao hapa Duniani na mbiguni ni huyo huyo ndie atakae wahukumu wahusika.

Ndio maana waswahili wakasema malipo duniani watalipia tu na si muda mlefu kilio cha wengi kitafumua wahusika wa mauaji hayo.
 
Damu hizi ni ushahidi ya kwamba hazitapotea bure. Ole kwa wao waliofanya hivi. Hawataishi kwa amani mpaka kieleweke....

Huu ni ushenzi na ni muda tu watajulikana kwa mazuri au mabaya.... Tusubiri
 
Green guards siku ya kufa kwao lazima kila moja aliwe tigo halafu akikata roho anachomwa moto
 
Hizo ni ishara za kuishiwa nguvu ya hoja...ukiona watu wanaanza kutoa roho za wengine kwaajili ya madaraka ujue mwisho wao ukaribu sana karibu kama neno lilivyo kinyani mwa mtu....Mungu awape raha ya milele mashahidi wote hao wa haki....
 
Aaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhh,
Kama ni kweli ni mauaji ya kisiasa, namuomba Ocampo aje hata leo!!!!
 
Inatia huzuni na hasira sana, watu wamefikia hatua hii? Tuombe mungu lazima damu za hao watu zitawalilia tu. Na mungu hatanyamaza kwa ukatili huu unaoendelea kufanyika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom