Maiti Yazinduka Iringa na Kuzua Kizazaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti Yazinduka Iringa na Kuzua Kizazaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 26, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maiti iliyozinduka monchwari Iringa Saturday, November 26, 2011 5:40 PM
  Alitangazwa amefariki baada ya kuanguka kanisani ambako alipelekwa kwaajili ya kufanyiwa maombi maalumu kwaajili ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu, aliwashtua watu alipoanza kurusharusha miguu alipofikishwa monchwari. Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Gerald Tadei Ngusi aliacha gumzo mjini Iringa baada ya kutangazwa kuwa amefariki dunia na baadae kuzinduka alipofikishwa monchwari.

  Tukio hilo lilitokea juzi mjini Iringa, wakati Gerald alipofikishwa kufanyiwa maombi kwenye kanisa la mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani Iringa aliyejulikana kwa jina la Boaz Sollo ambaye kanisa lake linajulikana kwa jina la Overcomers.

  Mke wa Gerald, Amina Ramadhan, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mume wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya juzi kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa.

  Amina aliendelea kusema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mumewe aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alidondoka chini na kukata kauli huku akionyesha dalili zote za kufariki.

  Baada ya wanandugu na watu waliokuwepo hapo kuafikiana kuwa Gerald atakuwa amefariki, waliamua kuupeleka mwili wake kwenye monchwari ya hospitali ya mkoa.

  Baada ya kufikishwa monchwari na mwili wake kuingizwa kwenye mojawapo ya vyumba vya monchwari, maiti hiyo iliamka ghafla na kukaa huku ikurusha rusha mikono yake hali iliyozua kizazaa hospitalini hapo.

  Uamuzi wa haraka ulikuwa ni kumrudisha Gerald kwenye mapokezi ya hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi.

  Baada ya uchunguzi wa madaktari, taarifa kamili ilitolewa ambapo ilisema kuwa Gerald amefariki dunia.

  Polisi wanalifanyia uchunguzi tukio hilo lililotokea kwenye majira ya saa 10 za jioni.
  Chanzo: Maiti Yazinduka Iringa na Kuzua Kizazaa
   
Loading...