Maiti yakutwa chooni, alikopa laki 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti yakutwa chooni, alikopa laki 4

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BWANA FETO Philemon, mkazi wa Ubungo Maziwa amekutwa amekufa chooni, nyumbani kwake
  Maiti hiyo ilikutwa chooni jana majira ya saa 7 mchana wakati alipoingia kwa lengo la kupata haja.

  Kamanda wa Polisi Kinondoni, Bw. Charles Kenyela alisema, taarifa hiyo kituoni ilipelekwa na mke wa marehemu, aliyetambulika kwa jina Jesca Andrew (33),

  Kenyela amesema kuwa, mke huyo wakati anatoa taarifa hiyo alisema huenda mume wake alikuwa amekunywa sumu kwa kuwa hakukuwa na maelewano kati yao.

  Alisema mke huyo alidai walikuwa na ugomvi uliosababishwa na mke kumgombeza baada ya marehemu kukopa shilingi laki nne na kuzimaliza kutumia katika starehe zake binafsi.

  “Huenda alikunywa vidonge ama chochote kwa kuwa alishakopa pesa hiyo na aliitumia kinyume na malengo” mke

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na upelelezi wa kina wa kipolisi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.
   
Loading...