Maiti Wa 'Kusomeshea' Wazua Kizaa Zaa Muhimbili

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Maiti Wa 'Kusomeshea' Wazua Kizaa Zaa Muhimbili

592119841.jpg


Tafrani kubwa iliibuka juzi usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya lori moja kutiliwa shaka kuwa liliingia hospitalini hapo kwa ajili ya kuiba maiti 10.

Habari kutoka ndani ya hospitali hiyo zinasema kuwa uliibuka mzozo kati ya walinzi na walioingia kuchukua maiti hizo kuanzia saa 2:00 usiku.

Habari zinasema kuwa maiti hizo zilibainika baada ya walinzi wa hospitali hiyo kutilia shaka lori hilo na baada ya kulikagua walibaini kuwa lilikuwa limebeba maiti 10 ambazo zilikuwa zinaondolewa hospitalini wakati wa usiku na bila wao kuwa na taarifa.

Maiti hizo zilizuiliwa kwa muda wa saa kadhaa mpaka polisi walipoitwa kuthibitisha ukweli wake.
Akizungumza na NIPASHE kuhusiana na tukio hilo, mmoja wa walinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema gari hilo lilionyesha kibali cha kubeba mzigo na ndipo walipofanya maamuzi ya kulikagua lori hilo saa 4:00 usiku.

Alisema walibaini lori hilo likiwa limebeba maiti nyingi, jambo ambalo liliwashtua na kulizuia lisitoke mpaka hapo uongozi wa hospitali hiyo utakapotoa maamuzi.

Mlinzi huyo alisema kutokana na hali hiyo, polisi walipatiwa taarifa ambao walifika majira ya usiku na kuzizuia maiti hizo kusafirishwa hadi watakapokutana na uongozi wa hospitali hiyo.

NIPASHE ilifika hospitali hapo jana alifajiri saa 12:00 asubuhi na kushuhudia lori hilo aina ya Mitsubishi Fuso.
NIPASHE pia ilishuhudia polisi wakiwa wanalinda lori, na baadaye walilisindikiza kutoka hospitalini hapo baada ya suala hilo kumalizwa na uongozi wa Muhimbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema kuwa suala hilo ni la kiutawala linaloihusu Hospitali ya Muhimbili na kwamba wao hawawezi kulitolea taarifa bali wenye mamlaka hiyo ni uongozi wa hospitali hiyo.

“Ni kweli tulifika na kufanya uchunguzi wetu ila hakuna kesi ya jinai na suala hilo ni la kiutawala zaidi, hivyo sitaweza kulizungumzia kwani lipo chini ya Muhimbili, nadhani ukizungumza nao watakupatia taarifa,” alisema Kamanda Shilogile.

Ofisa Habari wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha, aliliambia NIPASHE kuwa maiti hizo zilikuwa zinapelekwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kilichoko mkoani Dodoma.

Aligaesha alisema kuna utaratibu ambao huwa unafanyika kwani vyuo vya tiba huomba maiti kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wao na wana utaratibu wa kutoa maiti hizo kwa vyuo vikuu vya tiba. Chini ya utaratibu huo vyuo husika huwa vinaandika barua kwa uongozi wa Hospitali ya Muhimbili kuomba maiti kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wao. Maiti ambazo huwa zinatolewa ni zile ambazo zimekaa katika chumba cha kuhifadhia maiti zaidi ya siku 14, baada ya ndugu kushindwa kujitokeza, “Na ikishafikia hapo maiti haina ndugu na imekaa zaidi ya siku hizo huzikwa na Manispaa kwa kushirikiana na polisi,” alisema Aligaesha.

Alalisema Chuo Kikuu cha Dodoma kina shule ya kufundishia madaktari, hivyo waliomba maiti 10 kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wao na waliruhusiwa. Ilipofika juzi saa 1:00 jioni walifika hospitalini hapo kuchukua maiti na kupandishwa kwenye lori wakiwa wamepatiwa kibali. Lori hilo lilipokuwa linataka kutoka katika geti la pili la upande wa kutokea magari, walizuiliwa licha ya kuonyesha vibali kwa ajili ya kusafirisha maiti hizo. Walinzi walikuwa na wasiwasi na ndipo walipozuia lori hilo ingawa hawakuwa na nia mbaya.

Polisi walifika kufuatilia tukio hilo majira ya usiku na kuzizuia maiti hizo zisitolewe getini mpaka hapo watakapozungumza na uongozi wa hospitali. Kisha walifika jana asubuhi na kuzungumza na uongozi wa hospitali na kufanya ukaguzi kama wahusika walikuwa na vibali vya kuwaruhusu kuondoka na maiti hizo. Baada ya mazungumzo polisi ilibaini kuwa wahusika walipatiwa vibali vya kuruhusu kuchukua maiti hizo 10 na ndipo gari hilo liliporuhusiwa kuondoka jana kuelekea mkoani Dodoma.

Aligaesha alisema maiti kusafirishwa usiku ni utaratibu wa kawaida kwani wahusika hao walipendelea kusafirisha muda huo na hospitali yake isingeweza kuwazuia kwa kuwa tayari walishapatiwa kibali

Akasema maiti huandaliwa vizuri na kuwekwa dawa ili wanafunzi wanaozitumia kwa masomo wasidhurike.

______________


My take:

Hivi nchi ya Tanzania aina taratibu za kuandikisha watu watakaotaka maiti zao kufanyiwa Postmortems na organ donation pale watakapokufa...!?

Pili raia wa Tanzania wanajuwa ili kama maiti imekaa siku kumi na nne (14), maiti za ndugu na jamaa zao zitazikwa na serikali au kupelekwa vyuoni ili zitumike kwa ajili ya kufundishia?

Nadhani imefikia sasa hii kitu iwekwe wazi kwamba mtu akifa basi ndugu au mgonjwa mwenyewe akubali maiti yake itolewe baadhi ya viungo au itumike kwenye mashule kwa ajili ya kufundishia, na si kujichukulia tu maiti kwa kisingizio cha kuwa haina mwenyewe au ndugu wamechelewa kutoa maiti hospitali.

Watangaziwe wale wote wanaotaka kuwa organ donor na wawe na vitambulisho maalum... Na kwa wale wenye vitambulisho basi kuwepo na sehemu kwenye kitambulisho kuonyesha kuwa huyu mtu ni donor na si vingine.
 
Back
Top Bottom