Maiti juu ya sahani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
MAITI JUU YA SAHANI

Na Robert Heriel


Binadamu ni kiumbe mbinfasi mno, ni kiumbe hatari mno. Hujipendelea na hupenda kupendelewa, hujithamini na kupenda kuthaminiwa.

Hupenda apendwe kuliko yeye apendavyo, hupenda kujaliwa kuliko ajalivyo wengine, Huyo ndiye binadamu.

Binadamu hujiona wa thamani kuliko viumbe wengine wakati hana thamani yoyote ile kuwazidi viumbe wengine.
Binadamu hujiona yeye ndio mwenye haki kuliko viumbe wengine.

Binadamu huendeshwa na roho yake mbaya ya ubinafsi na ndio maana dunia hii sio sehemu salama.
Siku ubinafsi wa mwanadamu utakapoisha ndipo dunia itakuwa sehemu salama kwa yeye mwenyewe na viumbe wengine.

Sheria huwekwa kwa watu wenye tamaa na ubinafsi. Pasipo tamaa na ubinafsi hakuna sheria, na pasiposheria basi hakuna uovu, na pasipo uovu basi hakuna hukumu.

Binadamu hula wanyama wengine lakini yeye hataki kuliwa, hula samaki wa baharini, Nyuni wa angani, na wanyama wa mwituni na kufugwa.

Hula kwa ubinafsi wao, huwachinja na wakati mwingine kuwaua pasi na utaratibu.
Mtu alaye nyama ya mnyama hajui thamani ya uhai, hajali uhai wa viumbe wengine. Hujali tamaa na starehe zake za tumbo.

Ikiwa mwanadamu angeweza kufikiri muda ule anaomla samaki aliyepo juu ya sahani akiwa anamtazama kuwa yeye ndio analiwa, angefiki kuwa samaki yule naye huenda alikuwa anataka kuishi kama yeye, kisha akajawa na roho ya imani basi kamwe asingemla samaki huyo. Lakini kwa vile roho ya mwanadamu imejawa na ubinafsi na kujipendelea basi haona shida kuua kiumbe kingine.

Haoni shida kutoa uhai wa kiumbe kingine kisa tumbo lake ambalo angeweza kulishibisha na vyakula vyenye asili ya mimea, naam ndizo hizo nafaka, mbegu, majani, mizizi na magome.

Embu jiweke nafasi ya kuku unayemla muda huo, jiweke nafasi ya samaki, kondoo au ng'ombe kama sio mbuzi unayemla hivi leo, unapomla hakuna alafu uanatafakari unajiona upo sahihi? Unapomla samaki huyo unapata hisia gani, huoni kuwa wewe huna tofauti na shetani?

Watu husema majini, sijui mashetani, sijui wachawi chakula chao ni nyama za watu, ukisikia hivyo unalaani vikali kwa sababu unajua ngoma inakuhusu kuwa nawe ipo siku unaweza geuzwa msosi na majini au mashetani kama sio wachawi. Alafu muda huo huo wewe ndio wa kwanza kwenda kuchinja kuku, kula samaki, kula mbuzi, hiyo kwako ni sawa, si atii? Hahahah! Mwanadamu acha ubinafsi, acha tamaa.

Thamani ya mwanadamu ni kubwa pale anapothamini viumbe wengine kwa maana aliambiwa avitunze, avitawale na sio kuvila.
Mwanadamu anajiona anathamani kwa kujidanganya yeye mwenyewe wakati hana la ziada mbele za Mungu. Yampatayo mnyama naye humpata, hakuna linalompata mnyama alafu lisimpate mwanadamu.

Mwanadamu amejaliwa tuu akili kisha Mungu akawatiishia wanyama ili wamtumikie ila sio ili awale.

Ujasiri wa Binadamu kutoa roho za wanyama wengine ulitoka wapi ikiwa aliambiwa ale mazao ya mimea huku mazao ya wanyama hakuambiwa?

Embu tuone nukuu hapa;

Mwanzo 1;
29. Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. 30. Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo

Katika aya hizo mbili hapo juu tunaona, mazao ya mimea kama vile matunda, mbegu, n.k ndio yalitolewa amri ya kuliwa na sisi wanadamu. Pia wanyama na ndege waliamriwa kuwa chakula chao kitakuwa ni mazao ya mimea. Sasa nini kimetokea baada ya uasi.

Kinachofanya watu wale nyama sio kitu kingine ni ushetani, uchawi na dalili ya roho mbaya ambayo mwanadamu amejiundia mwenyewe.

Haukuwa mpango wa Mungu watu kupata shibe kwa kumwaga damu za viumbe wengine. Lakini tamaa na ubinfasi wa mwanadamu ndio uliompelekea kula wanyama wengine, huku akidharau uhai wa viumbe wengine na kuuona uhai wake ni bora kuliko.

Uroho ndio chanzo cha yote.

Wewe unasema wachawi wanakula nyama za watu, sijui majini, sijui mashetani, mbona wewe unakula nyama za viumbe wengine? Ikiwa unajiona unathamani basi tambua hata viumbe wengine wanathamani vilevile. Ikiwa unajiona wastahili kuishi basi kaa ukijua hata viumbe wengine wanastahili kuishi.

Kama unaona nyama za wengine ni tamu basi fahamu fika hata yako ni tamu vile vile. Acha uroho.

Hivi kama mwanadamu anaakili za kiutu kwa nini asingeridhika na maziwa ya viumbe anaowala. Kama angekuwa na akili kwa nini asingeridhika na mayai ya ndege anaowala, huku akijitahidi ku-manage Ecosystem katika mazingira yake.

Nakushauri siku ukila nyama iwe ya samaki, au kuku, au dagaa, au mnyama yoyote assume wewe ndio hiyo nyama, kisha mchukulie anayekula nyama yako utamuonaje?

Jichukulie wewe ndio jini baya, shetani, na kigagula ambaye mbele yako umeletewa sahani ya wali yenye samaki mzima, jisni unavyofurahi wakati unapokula nivyo unadhihirisha kuwa wewe ni shetani.

Wanadamu tuache kujimwambafai, tuache kula maiti za viumbe wengine.
Kuna watu hapa watasema maiti ni mwili wa mtu hahahaha! Mwanadamu kazi kujipa heshima ambayo kimsingi haimstahili.

Kama simba angebadilishwa awe mwanadamu nakuhakikishia asingekula nyama, simba hula nyama kwa sababu hana chagua, ni asili yake, anatomia yake ya mdomoni kwenye meno haimsapoti kula majani, nafikiri hata mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula haumsapoti.

Nakupa homework;
Mchukue samaki aliyejuu ya sahani iliyojaa ubwabwa, kisha mtazame kwa dakika tano ukimtafakari. Fanya hivyo kisha urudi utoe maoni yako umejionaje.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Arusha
 
I'm on thoughts how I can defeat President Magufuli!!

I'm readying to shade my boodly
 
Mwandishi Kwa iyo na mimea pia inahusika kutupatia hewa ya oxygen yenyewe haistahili kuishi?
Vegetarians na vegans huichukulia mimea kama sio "viumbe" hivyo haistahili kuonewa huruma kwa namna inavyokatwakatwa, kupikwa mapishi mbalimbali na kuliwa.
Kiukweli mimi binafsi namuelewa zaidi mtu ambaye anakula vyakula vya mimea pekee kwa sababu za kiafya kuepuka madhara yatokanayo na nyama, sio sababu za kuepuka "kuua" kiumbe! Plants do exist, feel pain and they die!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom