Maiti' ameamka Afrika Kusini

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=1]'Maiti' ameamka Afrika Kusini[/h]
090731213751_sp_entierros_226x170i.jpg

Jeneza

Raia mmoja wa Afrika Kusini aliamka akajikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mwishoni mwa juma, na akaanza kupiga kelele akitaka atolewe- akiwatisha wahudumu wakidhani ni mzimu.
Familia yake ilidhani amekufa baada ya kushindwa kumwamsha Jumamosi usiku na kuwasiliana na ofisi moja yenye vyumba vya kuhifadhia maiti ya mtu binafsi katika kijiji kimoja mjini Eastern Cape.
Alikuwepo kwenye chumba hicho kwa muda wa saa 24, msemaji wa idara ya afya mjini humo aliliambia shirika la habari la Sapa.
Wahudumu hao baadae walirejea na kupiga simu kuita gari la wagonjwa.
Mtu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alitibiwa hospitalini kwa kukosa maji mwilini.
Msemaji wa idara ya afya ya Eastern Cape Sizwe Kupelo alisema, "Daktari walimfanyia uchunguzi na kuona kuwa anaendelea uzuri."
"Hakuhitaji matibabu ya ziada."
Bw Kupelo alisema mtu huyo aliamka saa tisa za Afrika Mashariki siku ya Jumapili, akitaka kutolewa kwenye chumba hicho chenye baridi kali kwenye kijiji cha Libode, na kuwatisha wahudumu waliokuwa zamu.
Bw Kupelo alisema, "Mwanzo watu hao walikimbia kwa kasi."
Maafisa wameusihi umma kuwasiliana na madaktari au wanaotoa huduma za dharura ili waweze kumtangaza mtu kufariki dunia kabla ya kuwaita wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti.
Bw Kupelo alisema, "Unaanza kujiuliza ni watu wengine wangapi waliokufa kwa namna hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

mtu aliyekuwa akidhaniwa amekufa, amezindukia katika vyumba vya kuhifadhia maiti baada ya kupelekwa huko akidhaniwa kafa, nafikiri ingekaa hivyo......
 
Iliwahi kutokea Dar pia. Kuna kipindi pia kilikuwepo RTD nadhani kiliitwa "Karibu RTD" na walikuwa wanakaribisha watu mbali mbali na kuwahoji kuhusu maisha yao walizaliwa wapi, walisoma wapi na wanafanya shughuli gani za kujipatia mkate wao wa kila siku. Nilikuwa sipendi kukikosa kipindi kile. Sasa kuna siku jamaa mmoja alipojitambulisha jina lake katika kipindi kile akamalizia kwa kusema jina lake la utani ni marehemu. Baada ya kuhojiwa akarushiwa hilo swali kwanini jina lake la utani ni marehemu? Basi ndipo akahadithia kwamba alipata ajali ya gari na kudhaniwa amekufa na kupelekwa chumba cha kuhifadhiwa wafu pale Muhimbili. Basi usiku wa manane baada ya kupigwa na baridi ya mle ndani akaanza kupata fahamu na kugundua kwamba yuko katika chumba cha wafu, basi alitoa ukelele wa hali ya juu :) :) :) njemba iliyokuwa zamu usiku ule ikatoka mkuku na kukimbilia hosteli nadhani ilikuwa ya manesi pale Muhimbili jirani na chumba cha wafu na kuwaelezea baadhi ya wanafunzi walioamka kilichojiri na kuomba msaada. Ndipo kufuatilia na hatimaye jamaa yule kuhamishiwa wodini kwa matibabu na alifanikiwa kupona kabisa na marafiki zake ndipo walipomtungia jina la utani la marehemu.
 
Jamaa paka anatengenezewa jeneza yeye kalala tu. Yaani nafikiri alikuwa bwi huyu. Sasa hao madaktari hawakumwangilia kama alikuwa mfu au la. Saint I, hii mambo inatisha sana ikianza kwa magamba. Watazika wapiga kura.
 
Yahudi,

Naona kila ukilala na kuamka wewe na magamba tu! Kweli Mgamba wamepollute nafsi za watu hapa nchini.
 
I didn't even noticed that. Thanks for reminding me.

Sasa turudi kwenye mada.
 
hahahahaha u remind me this guy

Hahahahahah lol! hiyo scene ya huyo jamaa ilinichekesha sana lol! Kwa kweli hii Hang over 2 nilicheka sana sijawahi kucheka katika movie hivi karibuni kama nilivyocheka katika movie hii halafu alipoingia Tyson kwenye ile sherehe ya harusi hahahahahaha lol!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom