Maishani mwako umeshakutana na yule moyo wako umemdondokea?

Miss Champagne

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
2,156
6,308
Hi,

Katika maisha unakuta kuna mtu anampenda mmoja kufa, yaani moyo wake hapo unadondokea na kutuama kabisa, hauendi tena kokote, hauoni njia nyingine, yaani ndo mwisho wa safari.

Ni ile yaani unakutana na mdada/mkaka msibani, shuleni, hospital, daladala nk, unafall inlove kiasi kwamba wengine huwaoni. Upendo ni ule pure, ije mvua liwake jua hakuna cha kukufanya utengane nae
Sijui nielezeje.

Hebu mfano music producer maarufu Tz alioa akazaa watoto, akakaa kwenye ndoa kama miaka 10 katika kazi zake. Akaingia kwenye project ya kukuza vipaji akakutana na binti mmoja akafall inlove, haambiwi hasikii mpaka ndoa alikua radhi kuivunja na kuendelea na huyo binti. Alidate nae zaidi ya miaka 10 hawaachani japo kuna tetesi wametibuana.

Baba yetu JBourne59 kakutana na pisi za kutosha enzi zake, ila alipomwona Hamida bint Burhan moyo wake ukadondokea hapo. I am sure hata angekua na familia tayari sijui kama ingepona sababu ya hamida.

My friend aliolewa zamani akiwa 25 just kutimiza tu matakwa ya ndoa. Alidumu 10 years, akakutana na huyo jamaa wa sasa, ndoa ikavunjika. Amekuja ulipodondokea moyo wake, humwambii kitu kuhusu huyo jamaa, yupo radhi auze dunia nzima ampe.

Wengine huwa wanakutana mara ya kwanza inakuwa mwanzo mwisho bila kuumiza wengine. Yanii unaweza ukawapenda wengi tu lakini kunakuwa na yule mmoja ambaye ukiwa nae unaona mwendo umeumaliza.

Wengine unaishia kuwatamani lakini upendo wa moyo wako upo pale. Ndio wale wenzangu na mie akiachwa na huyo mwenza anataka kujiua, kujinyonga, anakondaa na kuingia kwenye ulevi ama depression, sijui naeleweka?

Umeshakutana naye maishani?
 
Usipojua unachokifanya ndio utakuwa limbukeni wa hivi, mtu kuacha jua ukafata tochi khaa! Betri ikishaisha unatamani jua, unaanza kugundua kumbe ulikuwa unapoteza muda na kuumponza mwili.
Ni bora hata anayekimbia mtu kufuata mahitaj, jamii itamuelewa...
 
Hi,

Katika maisha unakuta kuna mtu anampenda mmoja kufa, yaani moyo wake hapo unadondokea na kutuama kabisa, hauendi tena kokote, hauoni njia nyingine, yaani ndo mwisho wa safari.
rne59[/USER] kakutana na pisi za kutosha enzi zake, ila alipomwona Hamida bint Burhan moyo wake ukadondokea hapo. I anakondaa na kuingia kwenye ulevi ama depression, sijui naeleweka?

Umeshakutana naye maishani?
Bado, ni lazima itokee?
 
Maisha ya sasa ni ngumu kujua mtu ana kupenda kweli au ana igiza pia upande wangu nina amini kama hakuna pesa upendo ni mdogo sana
Ndio huo upendo niliouongelea..huwa hauangalii hali ya kipato cha mtu..hata uwe mwanaume kapuku atakupenda wewe ulivo sio kwa ulichonacho.
Huoni kuna wanawake wako tayari wampe mahari kijana akalipe kwao?

Hujawahi ona familia tajiri zikiwa na mgogoro wa kupinga ndoa na familia maskini..?
Hujawahi ona binti tajiri humwambii kitu juu ya kijana hohehahe?

Hujawahi ona ndoa wenza wanaporomoka kiuchumi toka kula hotelini hadi kukopa kitunguu gengeni but still wanapendana hakuna wa kumkimbia mwenzie hata kama anapo pazuri pa kwenda
na wanainuka pamoja tena?
 
Back
Top Bottom