SoC02 Maisha yetu yako vichwani mwetu ila utekelezaji upo mikononi mwetu

Stories of Change - 2022 Competition

Ngully28

New Member
Sep 5, 2022
1
0
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna kisichowezekana katika maisha kwani tuna mifano mingi ya watu waliozaliwa katika familia maskini ila wakawa kuja matajiri. Tambua kuwa umakini, uthubutu na jitihada zako ndizo zinaweza kuamua kesho yako.

Wapo waliobahatika kupata pesa ila hawakudumunazo, nikimaanisha kuna watu wengi waliozaliwa katika familia tajiri ila wakashindwa kuuendeleza huo utajiri na hatimaye kufilisika, pia wapo baadhi waliopokea mishahara minono kipindi cha uhudumu wao kazini ila baada ya kustaafu wanaishi maisha ya kawaida sanaa na wengine wanafikia kuuza rasilimali walizopata wakiwa kazini ili tu waweze kujikimu si kwamba wanapenda ila walijikwaa sehemu. Hivyo mimi na wewe itoshe kusema tunaweza kutimiza ndoto zetu tukiwa na mipango thabiti, jitihada, uthubutu kwenye baadhi ya mambo;

Kujifunza bila kuchoka. Ili kuzifikia ndoto zetu hatuna budi kuishi huku tukipokea mawazo mapya kila leo kwani maisha yanabadilika na mawazo mapya yanazaliwa kila leo hivyo hatuna budi kukubaliana kuwa kuna watu wanajua zaidi vitu mbalimbali kuliko vile ujuavyo wewe. Hivyo tukiishi kwa kujifunza tunaweza kupata mawazo mapya yanayoweza kuboresha au kurahisisha utekelezaji wa ndoto zetu kwa ufanisi zaidi. Haina maan kuwa watu waliosoma hawapaswi kupokea mawazo kutoka kwa wasiosoma kwakuwa wao wana elimu kubwa la hasha kwani hata wale wasiosoma wana uzoefu na ujuzi wa vitu vingi mno katika maisha halisi tofauti na yale maisha ya kwenye kitabu.

Ishi na ziishi ndoto zako popote uwapo. Kuna muda tunakosea kwa kuwa na utekelezaji hafifu wa malengo yetu mfano mwanafunzi hawazi elimu hadi afike darasani, mkulima hawazi kilimo hadi afike shambani kwake la hasha bali tunapaswa kuyaishi mawazo yetu popote panapohitajika kufanya hivyo. Tunapaswa kuvaa uhalisia wa kila kazi au ndoto mahali popote tunapokutana na vitu vinavyofanana na vile tunavyolenga kuvitekeleza kama wewe ni mkulima au una ndoto za kuja kuwa mkulima basi ulionapo shamba basi jikute wewe ndio mmiliki na ujaribu kujiuliza jee! kama shamba hili lingekuwa la kwangu ningefanya nini kwa hatua hii lilipofikia?. Kwa kufanya hivyo itatusaidia kupanua wigo nawe ukija kulima utaboresha zaidi shamba lako.

Screenshot_20220905-073723.jpg

(Picha- Quote BP)
Tuwashirikishe mambo yetu watu waliotuzunguka. Kumekuwepo na kauli inayodai "Usiwaambie watu unapanga kufanya nini ila mafanikio yako ndio yaongee badala yako". Ninachoamini sio kila mtu ana nia mbaya au hapendi maendeleo yako la hasha ila wapo baadhi wataziunga mkono jitihada zako. Kuwashirikisha wengine kunaweza kutusaidia kutukumbusha pale tunaposahau kutekeleza majukumu yetu kama tulivyopanga muda uliopita.

Tukumbuke kutokana na maisha tuliyonayo tumekuwa tukikumbana na changamoto na mambo mengi kiasi kwamba tunajikuta tukisahau vitu vingi sana vya msingi na kujikuta kila siku tukiamka na kuanza kuwaza mambo mapya, kupitia kuwashirikisha wengine wanaweza kuwa hazina ya kumbukumbu kukukumbusha ulichoazimia kukifanya muda uliopita hivyo wanaweza pia kuturudisha kwenye mstari.

Screenshot_20220905-073217.jpg

Namna mawazo ya wengine yanavyowezq kusaidia jitihada zetu(picha Quote BP)

Aidha, tunapaswa kujiona viongozi na watendaji wakuu wa maisha yetu. Hakuna atakayeamua au kufanya maamuzi kwaajili yako yanayoendana na matakwa na ndoto zako zote kwa asilimia mia moja (100%) isipokuwa kwa kiasi chake. Utashauriwa vitu vingi, utawashirikisha watu vitu vingi ila mwisho wa siku wewe ndiye mtu pekee ulineba maamuzi ya mwisho ya kupokea na kuchambua ushauri upi sahihi uufuate ili ukuletee tija. Mwisho ya yote utagundua safari ya mafanikio imebebwa mikononi mwetu wenyewe.

Chagua unachotaka kukifanya. Katika suala zima la kutafuta hatupaswi kufuata mkumbo. Wengi wetu tumekuwa na hurka ya kuvamia ndoto za watu wengine na kuziacha ndoto zetu zikipata kutu kwani hatuwezi kufanikiwa kwa kuwaza kufanya kitu kipya kila leo bali kwa kuendelea kuboresha kile tulichoanza kukifanya tangu jana kupitia ndoto hiyo.

Hivyo tuwe wavumilivu na kabla ya kudandia ndoto ya mtu mwingine jiulize, 1.Je, hakuna waliofanikiwa kupitia ndoto zinazofanana na hiyo yako?, 2. Je, kwenye hiyo ndoto unayotaka kuirukia kisa umemuona mtu fulani kafanikiwa jee hakuna maskini au walioshindwa kuitimiza?. Ukijiuliza maswali hayo utajiona hata nawe una nafasi ya kufanikiwa kupitia hiyo hiyo ndoto yako ya siku zote.

Screenshot_20220905-073629.jpg
(Picha-Quote BP)

Usijilinganishe na watu waliofanikiwa. Hii pia itatusaidia katika kutafuta kwani kujilinganisha na mtu aliyefanikiwa kunaweza kutukatisha tamaa na kujiona hatuwezi kufikia walipofikia wao au kuwa na hurka ya kufanikiwa kwa haraka na kujikuta tukiingia katika matatizo kwa kutamani na kutaka mafanikio ya haraka, vilevile kufanya kazi zaidi ya uwezo wa miili yetu na hatimaye kupata maradhi ya kifua na mwili kuchoka kupindukia na kujikuta tukisimamisha ndoto zetu kwa kuanza matibabu. Hivyo basi hatutakiwi kujilinganisha na wengine waliofanikiwa isipokuwa mafanikio yao yatupe chachu na ari ya upambanaji ili siku moja tusijekuwa wao ila tuwe na maisha kama yao.

Jitihada, kujitambua, kuthamini upatacho kwa pamoja vinaweza kukufanya uwe na maisha bora. Sina maana unaweza kuwa tajiri kama Mohamed Dewji (MO) au Bakhressa ila unaweza kuishi maisha ya ndoto zako au zaidi hata ya hao wawili kwani maisha hayana kikomo cha mafanikio isipokuwa kila mmoja anaweza kufanikiwa zaidi ya wengine kwani hata hao niliowataja ukiwauliza leo hii kama walikuwa wanawaza nini miaka 30 iyopita kuhusu kiwango cha utajiri walionao leo naamin majibu yao yatakuwa tofauti na uhalisia walionao sasa hivi.

Mwisho; Tukumbuke mafanikio hayana fomula maalum isipokuwa yana hatua ndio maana wapo wanaofanikiwa kwa haraka na wale wanaochelewa isipokuwa hatupaswi kukata tamaa na kusafiria ndoto za watu wengine tukumbuke hatuwezi kufanikiwa kwa kubadilisha ndoto kila siku kwani hata wale waliofanikiwa hawakujua siku au tarehe maalum waliyopokea mafanikio isipokuwa walikuwa na matumaini kuwa ingefika siku nyota yao ingeng'aa.

Mimi na wewe bado tuna nafasi ya kuwa miongoni mwa watakaofanikiwa muda wowote kuanzia sasa kikubwa tuwe na subira na mara zote tuiishi leo yetu tukiikumbuka jana yetu huku tukiwaza namna ya kuijenga kesho yetu. Kuzaliwa maskini kusitukatishe tamaa bali kutupe ari ya upambanaji na kujituma na kuamin ipo siku tutafanikiwa kwakuwa "MUNGU NI WETU SOTE NA ANATUPENDA WOTE". Bado hatujachelewa amka sasa tuianze leo safari yetu ya mafanikio.



Screenshot_20220905-081131.jpg

(Picha-Amka Mtanzania).
!!!!.....MWISHOOOOO....!!!!

Makala hii ni matokeo ya baadhi mawazo ya kijasiriamali, ushauri kutoka kwa watu mbalimbali na uhalisia wa maisha halisi ya jamii iliyonizunguka.
By JAMALI NGULI - 0782243156
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom