Maisha yanazidi kuwa magumu Tanzania gesi nayo imepanda nani wa kulaumiwa nataka jibu watu watajinyonga

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Nilisema nikatukanwa humu nikaambiwa ukiona mambo magumu sijui bidhaa zikipanda kalime

Sukari imeanza kupaa au haijapanda? nilisema

Unga nilisema watu wakanibeza sasa oneni

Sasa bei ya kujaza gas nayo imepanda na tunajua mkaa ulivyo ghali na serikali inazuia mkaa kwa nguvu zote bila kushusha bei ya nishati kama umeme na gesi

Angalau watu walianza kutumia gesi kupikia kuepuka mikaa sasa mnaturudisha mulemule umeme nao huo wa kununua unit 14 5000 utapikia nini?hata ukinunua umeme wa elfu 40 kwa mwezi sidhani kama utatosha kupika

Mkiambiwa mshushe bei ya units mjini huku wapangaji kila siku migogoro ya kununua umeme haiishi watu wanapata headache juu ya umeme!!!

Mkiambiwa mruhusu sijui taarif ndo taarif 4 ya kununua elfu 5 units 40 muiruhusu iende mpaka limitation ya units 100 per month consumption hamtaki....

Mnawalimit watu kama wanataka taarif 4 wawe na matumzi ya below 75 units per month mimi sipingi ila shida nyumba za kupanga wapangaji hawawezi kutumia mpaka limit ya 75 units tu mkiambiwa ongezeeni kwamba iwe units 100 au 120 limitation kwenye hiyo offer ya tariff 4 hamtaki.

Tanesco mnatutesa sana

Huku gas nao washaanza kututesa

Bei ya vyakula inatutesa

Bei ya bidhaa muhimu inatutesa


Bili za dawasco zinatutesa

Bei ya sukari inaanza kututesa hivi karibuni

Bei ya petrol kwa wenye magari wanateseka


Kodi kodi na faini na traffic zinaua watu kwa msongo wa mawazo

Wasio na ajira wanateseka,,,,fursa za kujiajiri ni kama zinawekewa vikwazo tu na watu hawaonyeshwi

Angalau kungekua na ajira watu wasiongea sana hata vitu vingepanda lakini wapi

Kwa hali hii watu watapata msongo wa mawazo na kuanza kujinyonga maana kila kitu ni kama kinazibwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom