Maisha yanaenda kasi sana; siku hizi Buza imekuwa maarufu kuliko Masaki na Oysterbay

soul provider

JF-Expert Member
Jun 21, 2014
1,330
2,071
Kwa wanaoifaham Buza vizuri kuanzia 2010 kushuka chini wanakumbuka tulipotoka. Me nimebahatika kuwa mwenyeji wa hapo. Ebana asikwambie mtu Buza ilikuwa mbaya mbovu kiasi kwamba ni ngumu mjuba kujitambulisha kwa mchuchu eti unaishi Buza utaachwa mara moja.

Vimbwenga vilikuwa vingi sana lakini ninachokumbuka hadi leo ni Vile vilima vya pale relini na kwa ma kibonge ilikuwa hatari sana sababu usafiri wetu ulikuwa mbovu balaa.

Yani gari ikishakongoloka inahamishiwa ruti ya kuja buza. Vile vilima ilifika wakati abiria tunashuka na kupandisha kwa miguu kuhofia gari kufeli kupandisha mlima.

Nimenusurika kifo mara kibao tu, gari kushia njiani ni kawaida sana ujanja wa konda anakudai nauli mapema kabla hata hujafika davis corner.

Abiria watata tulikuwa hatulipi nauli mpaka ufike unapokwenda. Balaa mvua inyeshe hapo noma inakuwa kilo kumi mzee usafiri unakuwa wa shida, nan akaue gari yake kisa 300 yako.

Sisi waenda shule nouma purukushani nyingi inabidi shati jeupe uweke kwenye bag utavaa ukifika shule. Tumepanda sana canter za kubebea mihogo asubuh.

Siku hizi fresh tu buza yetu imekuwa maarufu kushinda hata oysterbay na huko masaki.Ebu tukumbushae kdgo tulipotoka wenyeji wa hii mitaa kuanzia kilakala, abiola, njoo kwa ma kibonge usisahu makao makuu kwa lulenge, hapa ndo mjini kwetu.
 
Buza imekuwa Maarufu kwa yepi Mkuu? Kumbuka Hata Manzese kwa Mtogole ni Maarufu, Mbagala pia Ni Maarufu, Buguruni kwa Kimboka pia ni Maarufu.

Naona kama Umaarufu wa Buzza ni vile inaonekana UNDERDOG kulinganisha na hatua kubwa iliyopo kwenye Vitongoji Vingine vya Dsm kama Kimara, Mbezi, Tegeta, Tabata nk
 
Hapo kwenye underdog ndo tulipopatia umaarufu. Kuna kipindi hata network ilikuwa ngumu kupata
 
Buza imekuwa Maarufu kwa yepi Mkuu? Kumbuka Hata Manzese kwa Mtogole ni Maarufu, Mbagala pia Ni Maarufu, Buguruni kwa Kimboka pia ni Maarufu.
Naona kama Umaarufu wa Buzza ni vile inaonekana UNDERDOG kulinganisha na hatua kubwa iliyopo kwenye Vitongoji Vingine vya Dsm kama Kimara, Mbezi, Tegeta, Tabata nk
Waganga wa kienyeji walikuwa wengi sana, baada ya Buza kuchangamka wakakimbilia mbagala rangi tatu, mara wakakimbilia chamazi, huko ndo wamejaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom