Maisha yanaenda kasi sana, inakuaje vijana wa sasa wanakubali kulelewa kama watoto wa kike

Kwa kipindi hiki n kawaida kumkuta binti mzuri kabisa anatembeza uji,matunda au mboga mboga na kijana mwenye nguvu zake kabisa hawezi hata kufanya baadhi kazi kwa kujitoa angali elimu Hana kwa kuhofia kushushwa cheo.,anaona Bora ashinde kituo Cha bajaji&boda kusubiri deiwaka na akikosa ndo basi siku imepita atashindwa kuchangamkia ZALI kama hilo MKUU!!..miaka inavyozidi kwenda pesa naona inahamia kwa wanawake maana nowdays wamekua wapambanaji kutuzidi na wengi wao pesa yao inafanyiwa mambo muhimu(FUTURE PLANS)
Acha porojo wewe..wanaume tukiuza uji mtaani unadhani tutapata wateja wengi kama wanawake?.

Vijana wakiume wavivu ni wachache sana,tuache kuropoka ropaka,,vijana wa kiume wanapitia mengi kuanzia kupata mitaji na pia kupata michongo mitaani..
 
Acha porojo wewe..wanaume tukiuza uji mtaani unadhani tutapata wateja wengi kama wanawake?.

Vijana wakiume wavivu ni wachache sana,tuache kuropoka ropaka,,vijana wa kiume wanapitia mengi kuanzia kupata mitaji na pia kupata michongo mitaani..
Sikatai ila wengi hawapo siriaz mishe nyngine za kuokoteza zipo ukitafutiza..Sasa wao Hadi ziwafate mkuu!!..naposema wanashinda kwa kijiwe ina maana pakiwa na ugum unakuta bado hawaz kubadili mchongo ko anaona Bora aende kupiga story tu akikosa POA..na KESHO anarud
 
Hii nimeishuhudia leo Mlimani city katika mgahawa mmoja maarufu wa chakula, yaani kijana na nguvu zake inakuaje anakubali kununuliwa chakula na mwanamke ili hali angeweza kutumia nguvu na akili zake katika kutafuta pesa.

Na katika uchunguzi nimegundua yule mama atakuwa amemzidi kijana wa watu miaka si chini ya 20.

Sisi kama taifa tunaelekea wapi katika malezi, huyu kijana niliye mshuhudia leo alikuwa amejazia kifua, kachora tatoo kila mahali kavaa nguo zimebana miguu kama skin tight za wadada, au ndio ule msemo unaosema kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake.

Vijana wa sasa mnatuabisha wazee wa zamani, nikiweka kumbukumbu sawa kwa miaka yetu hali haikuwa hivi, mambo yalikuwa tofouti sana vijana wa sasa wanatumia muda mwingi katika kioo (kujipodoa) na gym (kutengeneza mwili) badala ya kutumia muda huo kutafuta pesa.

Vijana wa sasa mnatuangusha sana sisi wazee, mbadilike.
Heading inasema watoto wakike ila kwenye maelezo unasema mwanamke kamzidi dogo miaka kama 20.

Sasa hapo si unatakiwa useme mwanamke na mtoto wa kiume?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom