Maisha yamenishinda, vita imenishinda

Kuna dada alikua rafiki yangu kamaliza chuo udsm kazi hana,kwao sumbawanga anategemewa,tempo aliyopata kapigwa chini,maisha magumu,kodi hana,kazi anatafuta hapati..alikua ananilalamikia hadi nikawa nahisi atajiua,nilijaribu sana kumpa moyo alikua anaongea Kama wewe mtoa mada,kama mtu ambae kapangiwa FUNGU LA KUKOSA..siku moja natoka kwa mama jioni natembea mdogo mdogo,mdada kanitumia meseji ndefu,nzito Sana,wakati napandisha kilima cha forest,kuna kijana mlemavu akaniomba nimsaidie kumsukuma,hana MIGUU,Mikono yake mifupi Sana,kwenye baiskeli anaonekana Kama mtoto,roho iliuma Sana nikakumbuka kufuru zangu ukikosa mlo mmoja unaona Kama Mungu hakujali kabisa,kakukosea,anakuonea,nikafikiria nilivyo,ninavyoweza kufanya,nikajilinganisha na rafiki niliyekua namsukumiza,nikasema Asante Mungu,umenipendelea Sana..tangu hapo nikaanza kumpuuza yule dada,,hatuna shukurani..silalamiki sina viatu wenzangu hawana MIGUU..learn to show gratitude,kua na moyo mgumu,angalia ulivyobarikiwa,unachomudu,unachoweza fanya..kua jasiri maisha yetu wote yana pressure Life ain't sweet bro for both of us..and we don't owe Lord nothing...
Hii safari ya kuwa positive huwa siyo ndogo

Tujifunze kuhainisha mambo positive kila wakati na kujitafakari kwenye namna ya uchanya na hiyo inakupa nafasi ya kuona furaha ya maisha,hata katika vitu vidogo vidogo.

Mtoa mada Mungu akupiganie na wewe pia uzidi kujipigania.
 
Kuna changamoto moja nimempitia hii miezi mitatu nimechoka siwezi kuieleza hapa nimekosa msaada Kwa wote niliowahi kuwasaidia hata ambao sijawasaidia nimeamua baada ya hili tatizo Kwisha nasajili line mpya nianze upya. Kilichonifanya niwasamehe wanadamu ni kuwa tatizo langu ( la fedha) lingetatuliwa kupitia mradi WA familia cha ajabu mdogo wangu akanizunguka. Nikawaza Kama ndugu wa damu yangu ambaye ni mdogo wangu anaweza kujifanyia hivi ni halali MTU Baki kunipa mgongo. Line nitabadili marafiki na watu WA karibu nilionao hawezi kunisaidia hata elfu mbili ya nauli.
Pole mkuu. Nikisema umasikini mbaya hua naamanisha, nisiongee mengi. Nitafute mkuu.
 
Kuna changamoto moja nimempitia hii miezi mitatu nimechoka siwezi kuieleza hapa nimekosa msaada Kwa wote niliowahi kuwasaidia hata ambao sijawasaidia nimeamua baada ya hili tatizo Kwisha nasajili line mpya nianze upya. Kilichonifanya niwasamehe wanadamu ni kuwa tatizo langu ( la fedha) lingetatuliwa kupitia mradi WA familia cha ajabu mdogo wangu akanizunguka. Nikawaza Kama ndugu wa damu yangu ambaye ni mdogo wangu anaweza kujifanyia hivi ni halali MTU Baki kunipa mgongo. Line nitabadili marafiki na watu WA karibu nilionao hawezi kunisaidia hata elfu mbili ya nauli.
Pole sana
Maisha yana mambo mengi mno
 
Una uhakika baada ya kufa yaani huko uendako kitakuwa na maisha mseleleko?
 
Mkuu usikate tamaa, endelea kupambana
Nimepambana kwenye nyanja nyingi za kimaisha ila bado, nimeitafuta furaha kwa muda mrefu ila siku zangu za kuishi hapa duniani zimekuwa za mateso na maumivu,

Matatizo yako ni yako binadamu hawajali na hata hawatawaza hicho ndio kitu kikubwa nimekutana nacho, nimehangaika kwa kila namna kufanikiwa kimaisha, ila ukweli destiny yangu nimeishaijua niliandikiwa kufeli toka nazaliwa, hilo nimejua,

Sioni haja ya kuendelea kuhangaika kwenye dunia hii ambayo imeshanihukumu kwamba mimi nitakuwa mtu wa kufeli maisha yangu yote, siku za kukosa furaha na maumivu zinatosha sasa, mimi moja kati ya wanadamu ambao furaha tumegombana nayo,

Naishia hapa na hii ndio point ambayo sina budi kurudi kwa yule aliyeniumba
 
Nawashukuru sana wote mlionigusa kwa jumbe zenu wakuu labda sijapata nafasi ya kueleza nini kimenisukuma kuwa kwenye hali hii najua siwezi pata wasaa wa kuelezea pia kweli wapo wanaopitia changamoto nyingi kuliko zangu najua kabisa, sistahili kulalamika lakini ndani ya nafsi yangu yapo mazito ya kuumiza sana, naomba kuishia hapa na kushukuru mchango wa kila mmoja wetu kuhusu hili nafahamu haikuwa sehemu sahihi kulileta, niwaage kwa sasa na mungu awabariki nyote

Jifunze kuridhika kwa yote uliyojaliwa, ni dalili ya mtu mwenye shukrani.
 
Nawashukuru sana wote mlionigusa kwa jumbe zenu wakuu labda sijapata nafasi ya kueleza nini kimenisukuma kuwa kwenye hali hii najua siwezi pata wasaa wa kuelezea pia kweli wapo wanaopitia changamoto nyingi kuliko zangu najua kabisa, sistahili kulalamika lakini ndani ya nafsi yangu yapo mazito ya kuumiza sana, naomba kuishia hapa na kushukuru mchango wa kila mmoja wetu kuhusu hili nafahamu haikuwa sehemu sahihi kulileta, niwaage kwa sasa na mungu awabariki nyote

Soma hapa mkuu>>>>>>>Maisha yanaogopesha ila wewe usiogope.
 
Pole sana,maisha haya yanachangamoto mnoo...chamsingi mshirikishe Mungu hali unayopitia kwani anasema ... sikio lake si zito hata asiweze kusikia na wala mkono wake si mfupi hata asiweze kutenda.
 
kama huna kazi ndugu yangu ebu soma hapo chini pengine unaweza kupata pa kuanzia

ndugu zangu, kutokana na changamoto ya ajira inayotukumba, watu tumesoma lakini ajira zinakuwa ngumu kupatikana, kikubwa tujifunze kutokuchagua kazi, waswahili wenyewe wanasema ni bora kidogo cha halali kuliko kukosa kabisa ama ukapata kikubwa cha halamu ambacho kinaweza kukutia mashakani. vile vile "ukitaka kupata kitu ambacho hujawahi kukimiliki ni lazima uthubutu kufanya kitu ambacho hujawahi kufanya"

niliangahika sana kutafuta ajira, japo ni holder wa diploma ya uandishi wa habari, lakini nilijikuta ndoto zangu za kufanya kazi kwenye vyombo vya habari zinafifia kwani kila nilipo bahatika kupata kazi kwenye kampuni za habari, mishahala ilikuwa haikidhi vigezo haswa ukizingatia kupanda kwa gharama za maisha.

niliamua rasmi kuachana na taaluma niliyosomea baada ya kuona malengo yangu yanazidi kufifia. naomba niwape moyo ndugu zangu mnaotafuta ajira, msikate tamaa. weka mipango kichwani huku ukitafuta mbinu mbadala za kujikwamua.

safari yangu ya maisha ilivyoanza

View attachment 1742667
baada ya kuhangaika sana bila mafanikio kutafuta ajira inayoendana na elimu siku moja nikiwa huko Arusha, nilienda kuomba kazi kwenye godauni moja la bia, lililopo pale ngusero...kalibu na FFU. kwenye hilo godauni kulikuwa na mlinzi wa kampuni ya KK. ambayo hivi sasa inatwa garda yule mlinzi aliniambia "pale hakuna kazi" ila kama nitapendezwa na kazi ya ulinzi basi nipeleke vyeti vyangu vikafanyiwe uhakiki kwenye kampuni yao ya ulinzi ya garda, iliyopo huko kijenge karibu na Impala hotel ARUSHA.

kweli nilibahatika kwenda na walipo kagua vyeti vyangu viliwarizisha hivyo safari yangu ya ulinzi, ilianzia hapo, nilifanya mafunzo yao ya takribani siku 14, wakatutunuku vyeti kwenye mafunzo hayo tulikuwa walinzi zaidi ya 60 wenye elimu kubwa zaidi ya yangu. lakini wote tuliweka elimu zetu kando, tukaamua kuwa wafungua mageti ama wabeba virungu.
View attachment 1742669

kipindi naanza kazi hii ya ulinzi nilikuwa nalipwa 250k kwa mwezi lakini kuna miezi mingine ilikuwa inafikia hadi 280k...kiujumla kamshahala hako kalikuwa hakaitoshi kabisa, lakini nilivumilia nikajipanga na bahati ilikuwa yangu kwani kwenye hii kampuni huwa kuna promosheni ya kwenda kusoma kozi zinazoendana na mahitaji ya ofisi, kila ukienda kozi na kimshahala nacho kidogo kinatuna. kidogo hivi sasa kimshahala kimetuna na mimi natembea na pochi kubwa mfukoni.

View attachment 1742670

hivyo ndugu zangu, tusiogope kufanya kazi kwakuwa ndugu zetu watatucheka, kuna walinzi wana mishahala mikubwa kama watu wa serikali na pengine mikubwa zaidi ya watu wa serikalini. hivyo karibuni kwenye sekta ya ulinzi, japo bado napambana kuhakikisha ndoto zangu za kuendeleza taaluma niliyosomea lakini napambana huku nikiwa kwenye kazi ambayo kwa kiasi fulani inaniletea heshima mtaani ata pakitokea tatizo ninaweza nikatoa mchango japo kidogo.
View attachment 1742671

hivyo nimeona niwaletee hii fursa kwa watanzania ambao hamchagui kazi karibuni sana Gardaworld.

jinsi ya kujiunga na GARDAWORLD

1. uwe Mtanzania ambae utanzania wako hauna shaka kabisa
2. uwe na vyeti halisi vya shule {tumia cheti cha elimu ndogo kabisa isiwe juu ya kidato cha nne.... utakuja kunishukuru hapo baadae kwa mbinu hii}
3. uwe na cheti cha kuzaliwa
4. uwe mrefu haswa.
5. uwe na namba ya nida ama kitambulisho cha nida pia ukiongeza kitambulisho cha mpiga kura itakuwa poua
6.uwe na wadhamini wawili ambao watakuwa teyari kufika ofisini kwaajili ya kujaza fomu maalum za kukudhaminiView attachment 1742673

kama unavyo vigezo tajwa hapo juu, na upo Dar es salaam panda dala dala zinazoelekea Kawe haswa zinazopitia ubarozi wa marekani {moroco} kisha utashuka kituo cha KWA MWINYI {ukiwa mitaa hiyo unatakiwa kuwa makini muda wote ujiepushe na kushangaa shangaa haswa nyumba za karibu na ofisi ya Garda kwani ofisi hiyo ipo karibu na nyumbani kwa Rais mstaafu AL-HASSANI MWINYI na maeneo hayo yana ulinzi mkali}

View attachment 1742674
baada ya kufika kwenye ofisi za garda wakakufanyia vipimo na usaili wa awali utapewa maelekezo ya hatua inayofuata. hakuna rushwa katika kupata kazi hii, wala mimi mtoa post sina uwezo wa kukusaidia kuruka kigezo chochote ili uweze kupata kazi hii, kitakachokubeba kwenye kazi hii ni vigezo tu. ukiwa na vigezo stahiki utapata kazi. ukiwa huna kigezo mwenyezi Mungu akupe hitaji la moyo wako katika makampuni mengine yanayoendana na vigezo ulivyo navyo.

hivyo nafungua rasmi mianya kwa watanzania wenye mapenzi ya dhati kwa wenzao kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa kutuandikia hapo chini juu ya ajira iliyo karibu na wewe lengo ni kukwamuana, nina uhakika hii itakuwa sadaka kubwa kuliko kusaidiana fedha. na wale ambao tutabahatika kupata kazi kupitia uzi huu turudi kutoa ushuhuda ili wengine wapate pakuanzia.

View attachment 1742676

MUNGU IBARIKI JAMIIFORUMS,

MUNGU WABARIKI WANA JAMIIFORUMS

MUNGU IBARIKI TANZANIA

MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Back
Top Bottom