Maisha yamekuwa rahisi sana kwa wahitimu wa vyuo na Wafanyakazi wa Serikali Tanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,240
2,000
Wanabodi, Leo hii kila kona ya nchi kuna vyuo vikuu bora na vya kisasa zaidi ya Harvard ,Yale pamoja na Stanford ambavyo vinatengeneza vijana wenye maarifa katika utafiti, uongozi na teknolojia

Mfano mfumo wa malipo wa GEPG (Government electronic payment gateway system) imeundwa na vijana hawa wazalendo wakiongozwa na kubwa lao kijana toka pale BOT sasa ni mkurugenzi wa mifumo wizara ya fedha na alisoma University of Dar es Salaam(UDSM).

Mfumo wa GEPG kwa kutumia control number umerahisisha malipo ya maji na umeme kwa kila mtanzania hilo halipingiki kuwa kwa sasa elimu yetu ni bora na vijana wanajiajili na wameajilika kwa maelfu

Kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2020 maelfu ya vijana wameajiriwa serikalini mfano Mamlaka ya mapato Tanzania TRA pamoja na Bank kuu ya Tanzania BoT huku wakilipwa mishahara mikubwa inayowawezesha kuendana na kasi ya awamu ya tano ya hapa kazi tu

Wafanyakazi wa serikali wameweza kumudu gharama za familia hasa upande wa vyakula na matibabu muhimu ya afya

Bima ya afya ya Taifa yaani NHIF imeboreshwa na kuwa Bima bora zaidi ukilinganisha na Bima za mashirika binafsi kama strategies,Jubilee au GA insurance hivyo watu wote hasa wa serikalini wanakula bata kwa gharama hizi nafuu

Chama changu Cha Mapinduzi kinatakiwa kufanya yafuatayo baada ya kushinda Octoba 28 mwaka huu 2020 ili wahitimu na wafanyakazi wazidi kuwa na furaha zaidi na nchi yao.

Mosi,Kuondoa Chuki iliyopandwa na viongozi wetu kati ya vyama vya siasa yaani wana ccm na wana chadema,Hii chuki imekuwa kubwa na imepoteza furaha kwa watu,Ukifuatilia ni kama watu wanasubiri mtu wa kusema na nyinyi upande wa pili jibuni mapigo,Akitokea mtu akasema jibuni mapigo vita hii haitazimwa kirahisi watu wana uchungu na hasira sana mioyoni mwao wanafikiria ccm inabebwa awamu hii ya tano.

Pili,Hoja zijibiwe kwa hoja na pale unapozidiwa hoja unachutama na kurekebisha makosa mfano suala la uhuru wa habari na vyombo vyake limekuwa linaongelewa kila kona ya nchi,Hii sekta sasa inaanza kujenga chuki kati ya waandishi na Raia.

All in all mapambano yanaendelea tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi na zilizoboreshwa technically tutawapiga mchana kweupe huku mkifikiri ni usiku.
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,364
2,000
Wanabodi,Leo hii kila kona ya nchi kuna vyuo vikuu bora na vya kisasa zaidi ya Harvard ,Yale pamoja na Stanford ambavyo vinatengeneza vijana wenye maarifa katika utafiti , uongozi na teknolojia...
BOT na TRA zinaajiri watu wangapi kwa mwaka? Na vijana wanaomaliza vyuo wapo wangapi?

Na kiwango cha huduma za Jubilee , Strattegies utafananisha na NHIF ?

Kafanye uchunguzi nakupa hizi home work 2 ukishamaliza kaa kimya usiwe unapost pumba.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
9,651
2,000
Wanabodi,Leo hii kila kona ya nchi kuna vyuo vikuu bora na vya kisasa zaidi ya Harvard ,Yale pamoja na Stanford ambavyo vinatengeneza vijana wenye maarifa katika utafiti , uongozi na teknolojia...
Mimi nimekuelewa.
 
Chikwuemeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
12,741
2,000
Unapingana vipi na anayetawala wakati amekiri mwenyewe,acha ujinga
Screenshot_20201013-125342.png
 
parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
1,424
2,000
BOT na TRA zinaajiri watu wangapi kwa mwaka? Na vijana wanaomaliza vyuo wapo wangapi?

Na kiwango cha huduma za Jubilee , Strattegies utafananisha na NHIF ?

Kafanye uchunguzi nakupa hizi home work 2 ukishamaliza kaa kimya usiwe unapost pumba.
👊👊 akili kubwa.
 
yungwe

Member
May 1, 2019
40
95
Wanabodi,Leo hii kila kona ya nchi kuna vyuo vikuu bora na vya kisasa zaidi ya Harvard ,Yale pamoja na Stanford ambavyo vinatengeneza vijana wenye maarifa katika utafiti , uongozi na teknolojia....
Hii ya Wafanyakazi sijui ! umebugi
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,717
2,000
Mkuu wewe ni mgeni nchi hii? Unazungumzia wahitimu gani? Unaeuelewa juu ubora wa huduma za bima zitolewazo na kampuni binafsi? Unatambua uhalisi wa tatizo la ajira nchi ktk sekta binafsi na ya umma toka awamu hii ya tano ilipoingia madarakani?

Kwa kuwa hili ni jukwaa la "Great Thinkers" pengine Mkuu hoja yako umeiweka ktk mtizamo wa "negation" ili kuweza kuibua zaidi mijadala kutoka kwa wachangiaji. Lakini kama umeandika kwa kumaanisha, basi naweza tu kusema, huu ndiyo uhuru wenyewe wa mtu ktk kutoa mawazo yake.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,240
2,000
BOT na TRA zinaajiri watu wangapi kwa mwaka? Na vijana wanaomaliza vyuo wapo wangapi?

Na kiwango cha huduma za Jubilee , Strattegies utafananisha na NHIF ?

Kafanye uchunguzi nakupa hizi home work 2 ukishamaliza kaa kimya usiwe unapost pumba.
Wale wenye ufaulu mkubwa na bright darasani wanawaajili

Wewe kama ulikuwa unacheza chuo ukapata GPA ya 2.7 hilo sahau mkuu

Ukitaka idadi nenda kwa vice chancellors udsm au ITA au IFM uliza wale wenye GPA kubwa wapo wapi?

Mwezi huu TRA imeajili mamia ya vijana waliofaulu interview

Kama ulifeli huwezi kupata taarifa hizi kwani umekaa kufeli feli tu
 
Dreadnought

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,612
2,000
Hayo maisha mazuri ya wafanyakazi yanakuwaje mazuri pasipo nyongeza ya mshahara miaka mitano?

Sijui huwa mnatumwa mje huku kujaribu kuhadaa watu.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,240
2,000
Hayo maisha mazuri ya wafanyakazi yanakuwaje mazuri pasipo nyongeza ya mshahara miaka mitano?

Sijui huwa mnatumwa mje huku kujaribu kuhadaa watu.
Utaongezewaje mshahara wakati huzalishi?

Unalipwa kutokana na huduma au bidhaa unayauza au kutoa

Wewe unafanya kazi mpaka utishiwe na Rais halafu unataka mshahara nani atakupa
 
Dreadnought

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,612
2,000
Utaongezewaje mshahara wakati huzalishi?

Unalipwa kutokana na huduma au bidhaa unayauza au kutoa

Wewe unafanya kazi mpaka utishiwe na Rais halafu unataka mshahara nani atakupa
Unaelewa maana ya kuzalisha au unaongea tu, kila mtumishi anazalisha kutokana na kada yake sina haja ya kuzungumza zaidi hapa.

Kingine annual increment iko KISHERIA, usifikiri aliyeweka hiyo sheria ni mpuuzi.

Hivi unadhani maisha huwa yako static? 2015 huenda huyu mtumishi alikuwa hajaoa, 2016 kaoa, mwaka huo huo kapata mtoto, mwaka 2019 labda mtoto wa pili, hivi huoni hapo majukumu yanaongezeka na bado mshahara ule ule.

Halafu from nowhere unasema maisha yamekuwa mazuri.
 
Congressman

JF-Expert Member
Jun 2, 2020
305
1,000
Wale wenye ufaulu mkubwa na bright darasani wanawaajili

Wewe kama ulikuwa unacheza chuo ukapata GPA ya 2.7 hilo sahau mkuu

Ukitaka idadi nenda kwa vice chancellors udsm au ITA au IFM uliza wale wenye GPA kubwa wapo wapi?

Mwezi huu TRA imeajili mamia ya vijana waliofaulu interview

Kama ulifeli huwezi kupata taarifa hizi kwani umekaa kufeli feli tu

Acha upotoshaji, nina lower second ya 3.3 lakini ni mtu muhimu sana katika Insurance industry nikiongoza vipanga wa GPA za 4.4 etc tena uzuri wengine ni classmates wangu wa pale Mzumbe Main campus pamoja na postgraduate.

Ila huwa nacheka sana nikiona madogo mnaumiza kichwa kuhusu sjui GPA mara mwingine ahangike na majina ya vyuo, haya yote nilikuja kuona upuuzi baada ya kuingia kwenye field.

Nachoweza kukumbuka ni kuwa, ukiwa na confidence yako na ukasoma vizuri kuelewa darasani In practical, ukabobea kwenye fani unayoipenda pamoja na kudevote muda wako wa ziada kujikumbushia ya darasani hata baada ya kuwa umemaliza chuo. Hakika ushindi kwako ni hakika.
 
natoka hapa

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
8,636
2,000
Wanabodi,Leo hii kila kona ya nchi kuna vyuo vikuu bora na vya kisasa zaidi ya Harvard ,Yale pamoja na Stanford ambavyo vinatengeneza vijana wenye maarifa katika utafiti, uongozi na teknolojia

Mfano mfumo wa malipo wa GEPG (Government electronic payment gateway system) imeundwa na vijana hawa wazalendo wakiongozwa na kubwa lao kijana toka pale BOT sasa ni mkurugenzi wa mifumo wizara ya fedha na alisoma University of Dar es Salaam(UDSM).

Mfumo wa GEPG kwa kutumia control number umerahisisha malipo ya maji na umeme kwa kila mtanzania hilo halipingiki kuwa kwa sasa elimu yetu ni bora na vijana wanajiajili na wameajilika kwa maelfu

Kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2020 maelfu ya vijana wameajiriwa serikalini mfano Mamlaka ya mapato Tanzania TRA pamoja na Bank kuu ya Tanzania BoT huku wakilipwa mishahara mikubwa inayowawezesha kuendana na kasi ya awamu ya tano ya hapa kazi tu

Wafanyakazi wa serikali wameweza kumudu gharama za familia hasa upande wa vyakula na matibabu muhimu ya afya

Bima ya afya ya Taifa yaani NHIF imeboreshwa na kuwa Bima bora zaidi ukilinganisha na Bima za mashirika binafsi kama strategies,Jubilee au GA insurance hivyo watu wote hasa wa serikalini wanakula bata kwa gharama hizi nafuu

Chama changu Cha Mapinduzi kinatakiwa kufanya yafuatayo baada ya kushinda Octoba 28 mwaka huu 2020 ili wahitimu na wafanyakazi wazidi kuwa na furaha zaidi na nchi yao

Mosi,Kuondoa Chuki iliyopandwa na viongozi wetu kati ya vyama vya siasa yaani wana ccm na wana chadema,Hii chuki imekuwa kubwa na imepoteza furaha kwa watu,Ukifuatilia ni kama watu wanasubiri mtu wa kusema na nyinyi upande wa pili jibuni mapigo,Akitokea mtu akasema jibuni mapigo vita hii haitazimwa kirahisi watu wana uchungu na hasira sana mioyoni mwao wanafikiria ccm inabebwa awamu hii ya tano

Pili,Hoja zijibiwe kwa hoja na pale unapozidiwa hoja unachutama na kurekebisha makosa mfano suala la uhuru wa habari na vyombo vyake limekuwa linaongelewa kila kona ya nchi,Hii sekta sasa inaanza kujenga chuki kati ya waandishi na Raia

All in all mapambano yanaendelea tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi na zilizoboreshwa technically tutawapiga mchana kweupe huku mkifikiri ni usiku
Hivi mnapewaga nini kuwasemea uongo watu ambao hawajawatuma kuwasemea?

Ungejua watumishi walivyo na hasira na huyo ndugu yako hata huu uzi ungefuta..
Wahitimu wana hasira nae unajua hilo.
Subiri 28 Oktoba
 
natoka hapa

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
8,636
2,000
Acha upotoshaji, nina lower second ya 3.3 lakini ni mtu muhimu sana katika Insurance industry nikiongoza vipanga wa GPA za 4.4 etc tena uzuri wengine ni classmates wangu wa pale Mzumbe Main campus pamoja na postgraduate.

Ila huwa nacheka sana nikiona madogo mnaumiza kichwa kuhusu sjui GPA mara mwingine ahangike na majina ya vyuo, haya yote nilikuja kuona upuuzi baada ya kuingia kwenye field.

Nachoweza kukumbuka ni kuwa, ukiwa na confidence yako na ukasoma vizuri kuelewa darasani In practical, ukabobea kwenye fani unayoipenda pamoja na kudevote muda wako wa ziada kujikumbushia ya darasani hata baada ya kuwa umemaliza chuo. Hakika ushindi kwako ni hakika.
Point nzuri ila nakukumbusha kitu, kusoma kutakusaidia usifanye kazi ngumu ila sio kupata hela, namaanisha hela nyingi.

Anyway tuendelee kufanya kazi kwa maslahi ya kupata msosi mzuri, kijumba kizuri, kigari kizuri na watoto kusoma English medium schools.

Maisha bhana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom