Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chase Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chaser Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo.

Sasa ni karibia mwezi wa saba huu tangia nianze biashara hii ya kuendesha Taxi bubu. Nilianza mwezi wa tano (May) mwaka huu wa 2020. Biashara imekuwa ngumu sana kwa maana siku hizi kuna Bajaj.

Mtu anaona bora akodishe Bajaj kwa bei nafuu ndio ampeleke mgonjwa hospital au kwenda mjini. Sisi Taxi Drivers tupo hoi biashara imeshuka. Kabla ya Bajaj kuja huko mambo yalikuwa shwari sana mwaka jana 2019, ila sasa hivi ni balaa tupu.

CHASER AVANTE NUMBER "A"

images (2).jpg


Kabla ya kuja Bajaj kulikuwa na hawa bodaboda ambao wao hawakuwa kikwazo kwetu kwa maana mtu hawezi kukodi bodaboda akabeba maharusi au akampeleka mama mjamzito kujifungua hospitali ya mbali.

Niliwahi kuwaza niendeshe gari hii kama Uber ila kutokana na ukubwa wake wa engine nisingeweza kupata faida yoyote. Ninaombeni msaada wenu wa mawazo.
 
Da pole ndugu yangu, tax now days zinachangamoto sana. Utandawazi umerahisisha viusafiri vya haraka, tax inaonekana old school pia tax ni gharama ukilinganisha na bajaji na boda kwa sababu ya mafuta inayo consume.

Mi nakushauri ili uende sawa na mabadiliko, uza hiyo tax nunua bajaji au boda mbili nyingine ajili mtu zina mishe kibao hasa Kama unaisimamia mwenyewe. Ni wazo langu tu maana kwenye biashara siku hizi nako kugumu hatari, Bora biashara ya usafirishaji.
 
Uza gari fungua biashara ya mgahawa na uisimamie mwenyewe, watu ni lazima kila siku wale chakula hivyo ni jambo la muhimu.

Kufungua pub ni jambo la ziada tu, siyo lazima kila siku watu kunywa pombe.

Ukizingatia huu ushauri wangu utakuja kunishukuru siku zijazo.
 
Japokua hela utakayouza hiyo gari haitatosha kununua bajaji mpya ila jichangechange uuze hiyo gari uongezee ununue bajaji mpya

Au huwezi kundesha bajaji siyo level yako?
yani ununue babaji milioni 7 ili dereva akuletee sijui 20,000 kwa siku mpaka upate faida cjui lini hapo una-assume haijaharibika ,haijakamtwa,hujaibia spare,haijapata ajali ,mwendo wa presure tu
 
Back
Top Bottom