Maisha yako yote Jifunze kutoka kwa Punda huyu alichokifanya

Facha Don

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
345
315
JIFUNZE KUTOKA KWA HUYU PUNDA
668a665fc26542b14ede8ac37b08b4b9.jpg

Mkulima mmoja alikuwa na Punda ...Punda aliyedumu nae kwa miaka mingi sana aliyemsaidia shughuli za kilimo na uchukuzi..alikaa naye toka akiwa mtoto mpaka punda akawa mzee kabisa.

Siku moja wakiwa wanatoka shambani, kwa bahati mbaya yule punda alitumbukia kwenye kisima kirefu sana ambacho kwa wakati ule kilikuwa kimekauka.

Yule Mkulima akawaza sana atafanyaje kumtoa yule punda..na baada ya kutafakari sana akasema kwanza hata hivyo huyu punda ameshazeeka ni hasara kuingia gharama za kumtoa...akaona vema tu amzike humo humo
Akaenda kuita majirani ,wakaja na sepetu wakaanza kumwagia udongo ,mchaka na kokoto shimoni kumfukia.

Mwanzoni tu ni kama punda alijua kinachoendelea..akapaza sauti na kulia kwa sauti kali ajabu..sauti ya malalamiko...hawakujali waliendelea kufukia..kwa kutupia kila aina ya taka taka

Baadae kidogo kwa mshangao wa wengi ghafla punda alinyamaza kimya kabisa sauti ikapotea....baada ya kutupia taka kadhaa..mkulima yule akaamua kuchungulia shimoni....Alistushwa mno na alichokiona Kila taka na mchanga ulipokuwa ukiangukia mgongoni mwa punda...alikuwa akifanya kitu cha kushangaza.

Kila udongo ulipomwangukia..alijitingisha ukamwagika na akaukanyaga akainuka juu kidogo...kila ulipokuja aliendelea kufanya hivyo hivyo..hatimaye baada ya Muda mkulima na majirani walishangaa kuona amefika juu kabisa ya ukingo wa kisima na akatoka kwa furaha kabisaa.

Kuna wakati maisha yanakurushia matakataka ya kila aina,acha kulia na kupiga kelele, jitingishe...yafanye ngazi..Kila jaribu linalotupata ni ngazi ya kupandia.
Kamwe hatuwezi toka kwenye visima virefu kwa kulia peke yake..bali kwa kupambana kuchomoka.

Wacha waone uko kimya baada ya makombora waliokurushia...yatake yapange..yafanye ngazi ya kupandia...

Changamoto yeyote unayopitia sasa...ni shimo na michanga..sisi ni zaidi ya punda..acha kulia, jikung`ute, yakanyage ,nyanyuka juu, toka Kanyaga Twende
 
nakushukuru sana mkuu..! kwa kunipotezea muda na kusoma hadithi yako, nakutakia heri ya mwaka mpya
Na sio wewe tu, kila aliye mjinga atajiona amepoteza muda kusoma mistari hii michache ya maandishi, ndio shida yetu...hatupendi kusoma.

Mimi nikushauri, badala ya kuilalamikia hadithi imekupotezea muda fanya kama Punda. Itumie kunyanyuka badala ya kupayuka.

Hutapata nabii mwingine wa kukuongoa katika hili zaidi yangu.

Wasalaam,
Mwana Mtoka Pabaya
 
nakushukuru sana mkuu..! kwa kunipotezea muda na kusoma hadithi yako, nakutakia heri ya mwaka mpya


Umedhihirisha jinsi Wengi Wa Watanzania tulivyo, Angeweka mada ya Umbea hapa au Ngono ungeona mnavyoishupalia.

Hatupendi mambo yenye jumbe ndani yake na za makala ndefu ndefu.

Si ajabu hata Vitabu tu huwa husomi.
 
Maisha sio rahisi kihivo bro!!!!! Wewe umepata matatizo umeswekwa ndani unajitikisa vipi? Au umemtia mimba mtoto wa shule hapo vipi? Au nyumba yako imevunjwa na serikale na una mke na watoto watano hapo je? Au umefirisika hujui hata wanao wanakula nini . Samahani lakini ukweli ni kwamba matatizo yanarudisha nyuma na kuvunja moyo hayajengi. Mafanikio ndio yanayo jenga
 
Back
Top Bottom