Maisha ya waTanzania hatarini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya waTanzania hatarini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by collezione, Mar 1, 2012.

 1. c

  collezione JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Naandika hii topic kutoka na experience ya kupoteza ndugu zangu mwezi uliiopita.... Hata kabla sijasahau, jana nimepoteza ndugu mwingine kwenye ajali ya basi.

  Ndugu zangu Maisha ya waTanzania kwasasa si salama tena... Na wengi watafanyia mzaha swala hili mpaka yatapowakuta kama mimi.

  Mimi naamini asilimia kubwa ni uzembe wa vyombo vyetu vya usalama.. Nchi yenye usimamizi mzuri ajali hazitokei mara kwa mara kama hivi.

  Mimi naona niweke mambo yafuatayo kama vyavzo vya ajali barabarani.

  1) Tanzania hakuna sheria au adhabu imposed kwa hawa wamiliki wa mabasi. Pindi ajali zinapotokea... And this is a huge advantage to them. Kwao ni sawa kuruhusu basi lisafirishe abiria, hata kama anajua basi lake ni bovu.. Na kwasababu hakuna chombo cha usalama kinachofuatilie ubora wa haya mabasi.. That is too big advantage to them.

  Mimi nakumbuka kuna siku nilisafiri kutoka Dar kwenda Arusha. Katikati ya safari tairi la nyuma likapasuka. Na kutokana na maelezo ya Dereva inaelekea alikua anajua ubovu wa tairi lake la nyuma... But who cares tungepata ajali na watu kupoteza maisha?? This is very sad.

  Ndo maana mimi nasema ajali zingine ni makusudi. Naomba Tanzania na sisi tuwe na sheria ya kulipa fidia kubwa pindi ajali inapotokea. Mmiliki anapaswa kutoa fidia kwa kila abiria aliye-athirika na hiyo ajali. Hii itapunguza huu uzembe.


  Hakuna asiyejua, kuna baadhi mabasi huwa yanatoa kafara, kutokana ushirikina... Lakini pindi inapotokea ajali, na kutokana na uelewa mdogo wa wananchi... Msemo mkubwa huwa "yote tumwachie Mungu..." Tusimweke Mungu kwenye huu upuuzi.

  2) La pili " ubovu wa barabara zetu". High way zetu ni nyembamba sana. Hazikidhi usafishaji wa abiria. (Kwa wale walioishi nje wananielewa nikisema hivyo).

  I am sure serikali inaweza kupanua hizi barabara zetu. Especial zile sehemu korofi "accident zone". Ila kwa sababu, kipaumbele chetu ni "siasa" na "kilimo kwanza" . Hakuna anayejali.

  Swali, je tuendelee kuvumilia kuona hizi ajali za kila siku??? Maana hili ni janga la taifa sasa.

  Natoa wito kwa waTanzania wenzangu. Tuanze kupigia kelele swala hili. Tuwawajibishe hao tuliowapa mamlaka kusimamia maisha yetu..

  Nchi yetu haina usalama kwenye nyanja zote... Ukija madukani kuna wajanja wanauza bidhaa feki. Mahospitali, siku hizi kuna madawa feki...
  Mtaani ujambazi ndo umeshamiri... Barabarani ajali kila siku.
  Sasa tukimbilie wapi? Nchi yetu haina usalama hata kidogo...
   
 2. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Usijali, ukishakufa utaenda sehemu ambayo ni salama zaidi na utakuwa guaranteed kuwa hutakufa tena
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Na sio barabarani tu... Majini angani, vyombo vyetu si salama
   
 4. c

  collezione JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Duh, ndugu yangu. Kama ni hivyo wewe ungekuwa unashinda ndani tu, unasubiri kifo.

  Haha, usiweke jokes kwenye vitu kama hivi. Kesho yatakukuta, utaikumbuka hii thread.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua kila mtu na upeo wake wa kuelewa, hoja yako ni nzito lakini watu wataleta mzaha!
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,201
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Hata majirani zetu Zambia hawewezi kuvumilia upuuzi wa wafanya biashara kuwapa watu vilema na kuwaua bila fidia. Kuna kampuni moja ya kitanzania kwa jina Sayuni ilikimbia moja kwa moja Zambia baada ya kusababisha ajali na mahakama ya kule kuamuru majeruhi wote walipwe. Hutashangaa polisi Trafiki wa kitanzania kupokea rushwa ya buku mbili na kuruhusu basi bovu mkweche kabisa lililoshehemu watu kuendelea na safari. Utamuona trafiki akiisha simamisha gari badala ya kulikagua anaenda nyuma ya gari na kondakta anamfuata kule na kumsalimia kwa kumpa mkono, halafu ghafla anarudi mbio ndani ya gari na kuliruhusu kwa kuligonga makofi huku wakiagana na yule trafiki kwa ishara ya dole gumba. Nchi yetu imechinjiwa baharini kwa sasa na hatuna baba mwenye nyumba.
  Kwa nini abiria tusichukue hatua mkonono kwa kumchoma moto trafiki anaepokea rushwa na kuhatarisha nafsi zetu, kama tunavyofanya kwa vibaka wa simu? Pia ninashauri kama ingeliwezekana ipigwe marufuku kwa mtu kupeleka basi lake kwenye biashara moja kwa moja na badala yake makampuni ndio yachukue jukumu hilo. Kama una kibasi kimoja tu basi itakulazimu kulisajili katika kampuni iliyoridhiwa na kuaminiwa kwa masuala ya usafirishaji.
  .
   
 7. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KWELI HALI NI MBAYA, TUZIDI KUMWOMBA MUNGU.Ajali za barabarani ni janga endelevu linalotutafuna. Waliopewa mamlaka kulinda sheria wamegeuka kuwa wahalifu waliovaa yunifom. Hebu safiri na basi/gari toka unaanza safari ubungo,trafiki wanapokea kitu kidogo,mpaka unafika uendapo. wenye mabas ndo hao hawagusiki! Mwaka jana nilipata ajali dodoma ya bus la allys la kwenda mwanza. Mmiliki alifika na kuanza kuwapa pesa abiria/majeruhi, posho hiyo ilienda mpaka kwa maripota wa vyombo vya habari waliokuja kushuhudia ajali ili waripot na hawakuripot ajali hiyo. Huu ni mfano mmoja tu jins ambavyo taasisi zlizopewa jukumu la kulinda maisha ya watz zina-conspire na wahalifu na matokeo yake maisha ya watu yanaangamia. Tumwombe Mungu atusaidie.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Serikali ya Kikwete hiyo ,wanapiga kelele majukwaani kupinga rushwa lakini TAKUKURU wakiwakamata watoa rushwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa. Joseph Mungai alikamatwa na TAKUKURU akitoa rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi mwaka 2010 lakini kesi ikaja kufutwa kiaina aina; hiyo ndio serikali ya washikaji!
   
 9. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Wewe endelea kuhudhuria Angaza maana kila ukipunguza mahudhurio tu,akili zako zinaanza kuwa hivi!
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umesema "Nchi yenye usimamizi mzuri ajali hazitokei mara kwa mara kama hivi.".

  Tujulishe ni nchi ipi ili tudadavue ukweli.
   
 11. S

  Samsindima Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la usalama barabarani ni kubwa na pana kiasi kwamba sisi wadau wote tunahitaji kutoa mchango wetu kulipunguza kama sio kuliondoa kabisa.
  1. Kuwe na umakini mkubwa katika utoaji leseni. Bahati mbaya hata watu wenye vichwa maji wanapewa leseni kwa sababu wanatumia rupia.....Rushwa.
  2. Wamiliki wa magari hawako makini katika kuajiri madereva. Hutumia madalali kuwapata ambao nao hutaka chochote ili
  wampatie mtu ajira kwa boss wao....Rushwa.
  3. Magari yanafurumushwa barabara kuu utadhani ya mashindano. Dereva akikamatwa na akatoa chochote mambo yanakwisha hapo hapo. Nilipanda Ngorika kwenda Arusha njiani nilipoona mwendo mkali nilimwomba Konda amweleze Dereva apunguze mwendo. Konda kwa majigambo akanambia kuwa yule si dereva mwenyewe kwani angekuwa ni dereva mwenyewe mwendo ungekuwa maradufu. Nilipofika highway Korogwe nilishuka na kupanda basi jingine. Tulipofika Himo relini tulikuta lile basi la Ngorika limepata ajali iliyoua watu kadhaa!
  4. Ushabiki wa abiria pia huchangia ajali.
  5. Ulevi. Gari moja liondokalo mchana kwenda mikoani linangurumishwa takribani saa nzima abiria wakijifuta majasho ili mradi tu dereva apate stimu kwanza. Likiondoka Ubungo utadhani Jet fighter! Bahati mbaya linashabikiwa. Ukiwa stendi hasa za Moshi, Iringa, Mbeya na Dodoma basi la kwanza kuingia toka Dar linapigiwa mayowe ya ushujaa!
  6. Ubovu wa magari ambayo mengi ni chakavu! Wenzetu wana taratibu za kukataza magari yaliyotumika kwa ama miaka 4 au kilomita laki 2 unusu yasihudumie abiria labda yathibitishwe kuwa yamefanyiwa ukarabati mkubwa.
  Vinginevyo tutakwisha eeh Mola tunusuru.
   
 12. c

  collezione JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu ajali sasa ni janga kubwa la taifa...sasa sijui tuchukue hatua gani, au movement gani ili tushughulikie hili swala.

  Kusafiri sasa hivi imekuwa kama unaenda kukitafuta kifo. Sasa tutafika kweli na hii hali?

  Mi naomba ndugu zangu tuchukulie hili swala serious. Lisiishie hapa tu. Tuje na mikakati ya kuliondoa kabisa.
   
 13. c

  collezione JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu, Zambia sasa hivi wameshaachana na ujinga. Na kama tongotongo sasa hivi zimeshaisha.

  Tanzania bado tuko kwenye siasa. Na wananchi bado wako kwenye tongotongo.
   
 14. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Mkuu! Pamoja na hayo, lipo tatizo kubwa ambalo liko gizani na hakika litatumaliza!
  Nalo ni vipuli BANDIA!
  Fikiria umenunua brake lining au bearing za hub bandia! umefunga kwenye gari, baada ya km30 zimeungua huku dereva akijiamini ana breki mpya, KIAMA LAZIMA KIFIKE!
  Tafakari na uchukue hatua!
   
 15. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,545
  Likes Received: 1,591
  Trophy Points: 280
  collezione
  mwaka huu hii hatari imezidi kuwa hatari.

  na serikali bado haijatoa suluhisho.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. CHAULA RICH

  CHAULA RICH JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 3,880
  Likes Received: 677
  Trophy Points: 280
  Acha kufanya mzaha kwenye matatizo mazito km haya wewe!.
   
Loading...