barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Ukiangalia katika takwimu za Tume ya Uchaguzi,Jimbo la Isimani ni moja kati ya ngome za Chama Cha Mapinduzi mkoani Iringa,ni jimbo ambalo mbunge wake Lukuvi amekuwa "akipita bila kupingwa" toka mwaka 1995.
Joto na vuguvugu la Uchaguzi wa mwaka 2015,Chadema iliweka mgombea ambae naye nasikia hakupata kura za kutosha sababu watu wa huko wanaamini sana Chama
Haya ndio maisha ya Wananchi wa Jimbo la Isimani,hili ni Jimbo la Waziri wa Ardhi Mh.William Vangimembe Lukuvi,ana zaidi ya miaka 20 akiwa mbunge wa Jimbo la Isimani.Aliingia mara ya kwanza kama mbunge mwaka 1995.
Hali ya huduma za kijamii ni mbovu sana,kuanzia shule,afya na huduma ya maji.Eneo hili katika picha ndio vyanzo vya Maji ya kunywa binadamu na Mifugo katika eneo hili.Watu wanakunywa maji ya kwenye makorongo na mto Ruaha.Sehemu hizi watu hunywa maji pamoja na wanyama kama ng'ombe,Punda na ngedere.
Maji ni uhai,hawa watu ukitembelea maeneo haya utawaonea huruma.Nilibahatika kukaa miezi kadhaa katika shughuli zangu.Hiki ndicho nilichokishuhudia katika ubovu wa huduma ya Maji.
Waziri Lukuvi na Mbunge wa Jimbo la Isimani,usiishie tu kwenye siasa za kitaifa,tupia jicho wapiga kura wako,maana hata sisi wageni tukitembelea jimbo lako tunaona kabisa hali ya wananchi wako haifanani na ukubwa wa jina lako