green rajab
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 11,289
- 35,798
Members nije kwenye maada husika. Hii mada inalenga hasa wale watabaka la chini tunajiita wa uswazi, kwanza kabisa ifahamike kua familia nyingi za kishua wamekua hawatumii fedha nyingi kwenye mahitaji ya msingi ya kila siku kwa mwanadamu kama mavazi na chakula wengi hua na ratiba ya kula ugali mboga za majani wiki nzima na jpl ndio siku ya kula nyama.
Kwetu uswahilini tunaongoza kwa kununua nguo za gharama na kukaangiza vitoweo mbali mbali kama kuku nyama na samaki kila siku huku tukiunga na nazi tatu nyanya kisado. Tunasahau kua tupo kwenye utumwa wa kifikra uswazi ukila dona mchicha au tembele unaonekana ni umechoka kiuchumi hiyo dhana ndio inawatesa watu na kuwamalizia akiba zao.
Jambo lingine ni ununuaji mavazi ya gharama kuliko uhalisia wa maisha yako afu umepanga nyumba ya gharama kubwa wakati kuna nyumba za bei nafuu lengo lako uonekane upo vizuri lakini kiukweli unajitesa fedha yote unayopata inaishia kujaza kabati na kukaangiza.
Umepanga apartment vyumba vitatu huna familia ili uonekane nawe upo vizuri, umekopa umenunua gari used unashindwa kukatia hata bima kubwa ukipigwa pasi unatelekeza gari gereji huo ni utumwa tutafute pesa na tuitumie kwa nidhamu itusaidie zaidi. Tuishi kulingana na hali zetu sinema hazina faida....ni hayo tu