BabaTina
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 429
- 573
Huko nchini Thailand, timu ya watoto wachezaji mpira waliamu kufanya matembezi ya utalii wa ndani baada ya mazoezi yao ya mpira wa miguu katika moja ya mapango maarufu huko kwao. Wakiwa na baiskeli zao walipofika eneo la kuingilia ndani walipaki nje na wao kuanza safari ya matembezi kujionea uumbaji wa Mungu kwenye eneo hilo.
Kwa bahati Mbaya sana, Mvua kubwa ikanya na kujaza maji ndani ya pango hilo na vijana kulazimika kutafuta upenyo katika moja ya miinuko ya pango na kujibanza eneo hilo.
Mmoja kati ya vijana waliokuwa kwenye msafara huko alipaswa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa siku inayofuata. Kutoonekana kwake kukazua hofu ambayo iliwafanya wazazi wake watoe taarifa katika vyombo husika. Nayo mamlaka ikachukulia taarifa hizo kwa umakini mkubwa na kuanza kuwasaka vijana hao yapata 12 pamoja na mwalimu wako wa soka.
Jitihada zikafanyika na kugundulika kuwa vijana wamebandwa kati ya viunga vya pango hilo lenye urefu wa KM 10. Waokoaji toka nchini Thai wakajaribu na kukwama hivo kuitisha msaada wa kutoka jumuiya ya Kimataifa.
Hatimaye timu kutoka UK, china na sehemu nyingine zikafika na kufanikiwa kuwanasua vijana hawa ambao walikaa ndani ya pango hilo kwa siku 10.
Binafsi nimejifunza kuwa, Mamlaka za nchi zipo kwa ajili ya watu wake na sio watu wake kwa ajili ya wenye mamlaka. Ndio sababu wanapaswa kuthaminiwa na kulindwa kwa namna yoyote ile.
Ushauri wangu kwa vyombo husika hususani wanaosema wakati mwingine mtu akipotea ni masuala binafsi hawawezi kuingilia wakajifunza hapa. Tazama video ya historia nzima ya tukio husika kwenye link hii