Maisha ya Ndoa ni Simba na Yanga?

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
5,349
1,224
Jamani wana jamvi, hili linatusumbua sana. Utashangaa wakati wa uchumba na urafiki watu wanakuwa na mapenzi tele, wanakumbatiana na mengine mengi! wanapendana na kuambiana you mean the world to me!

Shida inakuja baada ya kufunga ndoa! Wakiwa kwenye gari utajua tu ni mke na mume. Vile vicheko vya zamani vimekwisha, kukimbizana, kukumbatiana kwa mbinde? shida iko wapi? Utakuwa wanawake wengi kama sisi tunabaki kuangalia cinema za kina Ramsey wa Nigerai na Kanumba za Tanzania kukumbushia mapenzi! Tunakuwa tunajifariji na kuona ile ndio reality!

Recent study in America imeonyesha kuwa couples wengi wenye maisha mazuri na kuelewana na wale WALIOFANIKIWA KUBAKI MARAFIKI BAADA YA NDOA ZAO. Wenghi wetu tuliweka urafiki kando, tukawa na maisha ya kupaniana, kukomoana, na wakati mwingine kila anachofanya mwenzako unaona ni kosa. Jiulize, jambo hilo hilo analofanya mwenzako kama ungelichukulia positive na kuongea naye kwa upole, wala msingekwanzana.

wana JF, hasa wale ambao hawajaingia kwenye ndoa, jitahidini sana kubaki marafiki, mkivunja urafiki na mkawa MKE NA MUME, wait for countlessc sleepless nights!
 
Cha msingi mnapokuwa kwenye ndoa ni kila mmoja(mke na mume) a'stiki kwenye wajibu wake kama mwanandoa kwa mwenzi wake hapo mtaishi kwa furaha.
 
Jamani mie kila nikiingia humu nakutana na matatizo ya ndoa tena yanahuzunisha, wekeni basi na sred za mambo mazuri ya ndoa japo mtume moyo wale amabo hatujaolewa tuwe na hamu ya kuolewa,hizi nyingi zinakatisha tamaa jamani,kwan huwa kinatokea nn hasa mpaka ule upendo wa mwanzo unaisha?
 
mimi nimesoma hii sredi kuna mtu alikuwa anataka nioa nikamwambia subiri kwanza! mnatutisha!!
 
tatizo watu hawapo real everybod is untrue mwisho wasiku watu wanapotoa makucha yao wanashindwana kujifek kwingi jmn
 
Jamani mie kila nikiingia humu nakutana na matatizo ya ndoa tena yanahuzunisha, wekeni basi na sred za mambo mazuri ya ndoa japo mtume moyo wale amabo hatujaolewa tuwe na hamu ya kuolewa,hizi nyingi zinakatisha tamaa jamani,kwan huwa kinatokea nn hasa mpaka ule upendo wa mwanzo unaisha?

Jiulize kwa nini mfungisha ndoa/padre/n.k, anawaapisha kuwa wavumilivu? ana maana kuvumilia raha? NI SHIDA! walakini usiogope kuolewa, jitose tu.
 
Jamani wana jamvi, hili linatusumbua sana. Utashangaa wakati wa uchumba na urafiki watu wanakuwa na mapenzi tele, wanakumbatiana na mengine mengi! wanapendana na kuambiana you mean the world to me!

Recent study in America imeonyesha kuwa couples wengi wenye maisha mazuri na kuelewana na wale WALIOFANIKIWA KUBAKI MARAFIKI BAADA YA NDOA ZAO.
wana JF, hasa wale ambao hawajaingia kwenye ndoa, jitahidini sana kubaki marafiki, mkivunja urafiki na mkawa MKE NA MUME, wait for countlessc sleepless nights!

Yeah mi nataka niseme na walio kwenye ndoa jaribuni sana kurudisha ule urafiki wa mwanzo ndani ya nyumba zenu bado ni rafiki huyo mwenzi wako...wanawake/wanaume msiwachukie wandani wenu wala msiwe na uchungu nao sameheaneni makosa yenu yote nyie wawili wala msikimbilie wachenga na makorokoro yote .....Nyumba yenu iwe nyumba ya sala.. ombeaneni bila kuchoka.....na mahitaji yenu yote yajulikane na baba yenu wa mbinguni...
 
Jinsia za wavaa suruali a.k.a wanaume hatuna matatizo. matatizo yapo kwenu nyie tuu na mengine mnayaleta wenyewe wala sio ya kwetu
Mbona sisi tuko poa sana

Nakukubali sana kaka Rocky,mkeo ni wachache waliobahatika ...ila nasikitika kuwa halijui hilo...
 
Jamani mie kila nikiingia humu nakutana na matatizo ya ndoa tena yanahuzunisha, wekeni basi na sred za mambo mazuri ya ndoa japo mtume moyo wale amabo hatujaolewa tuwe na hamu ya kuolewa,hizi nyingi zinakatisha tamaa jamani,kwan huwa kinatokea nn hasa mpaka ule upendo wa mwanzo unaisha?

Catalisia wale ambao wako nje ya ndoa shetani hana shida nao sababu anajua wale ni wake......Kazi /vita inaanza na baada tu ya kutoka kanisani mama....kama huna Mungu unaweza ujute...lakini ukimtanguliza yeye mambo yote simple tu ..na si kweli kama ndoa zote zina matatizo kivile basi tu wengine temper zinakuwa juu ndio anayaleta huku...DEVIL IS A LIER HE WANTS TO DESTROY THIS GENERATION ...Just this ...NDOA NI NJEMA ASIKWAMBIE MTU NA TENDO LILE LINANOGA NDANI YA NDOA
 
Jinsia za wavaa suruali a.k.a wanaume hatuna matatizo. matatizo yapo kwenu nyie tuu na mengine mnayaleta wenyewe wala sio ya kwetu
Mbona sisi tuko poa sana
100%. Kuigaiga mpaka hata visivyo igika. wajisaili kwanza wajue wapi walipoipotezea ramani.
 
Jamani mie kila nikiingia humu nakutana na matatizo ya ndoa tena yanahuzunisha, wekeni basi na sred za mambo mazuri ya ndoa japo mtume moyo wale amabo hatujaolewa tuwe na hamu ya kuolewa,hizi nyingi zinakatisha tamaa jamani,kwan huwa kinatokea nn hasa mpaka ule upendo wa mwanzo unaisha?
unapewa facts ili ukijitosa uwe tayari umejiwekea misingi ya kukabiliana nayo. lakini asikudanganye mtu, maisha ya ndoa matamu ajabu. kinachohitajika tu ni understanding coz watu wanapokuwa katika uchumba huwa wanaficha makucha. wakioana tu ndo utajua kweli urefu wa makucha ya mwenzio. utadiscover weakness nyingi sana kumhusu mwenza wako. itabidi uvumilie.
 
Simkumbuki ni mdada gani alitoa hii kauli ntamkumbuka humu jamvini milele: 'Mwanamke hufikiria mwanaume atabadilika na mwanaume hufikiria kwamba mwanamke hatabadilika'. Kwangu hii kauli ina maana kubwa sana, hebua angalia na hii: "when a woman gets married she attains a Master whereas a Man losses his Bachelor". Teheheheheeeeee! Tatizo la wanawake mkishaolewa ndo mnaona basi ni wakati wenu sasa kumrekebisha mwanaume. Ziataanza kanuni na taratibu za ajabu ajabu hapo mpaka njemba unaanza kujuta why ulimuoa huyu demu.

Ila wenye busara zao, akhaa, wanenda taratibu mpaka mwanaume unajishtukia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom