Maisha ya ndoa ni magumu

Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?
Ni wazi mpaka umefika hapa, kuna mengi unapitia katika ndoa yako. Umekuja hapa kwa lengo la kupata ushauri. Kwa uchache wa taarifa ulizozitoa juu ya hayo yanayokukabili itakuwa ni vigumu kupata ushauri unaoendana na matatizo uliyonayo.
 
Hakuna kitu kizuri hapa duniani kama ndoa....ni vile tu ujue ni kwanini unaingia kwenye hiyo ndoa, na nani unaingia nae na je? Yale niliyoyatarajia nisipoyakuta naweza vumilia, unachotaka kutendewa na wewe mtendee mwenzako.

Choose life, choose happiness
 
Ifike mahali watu wa ustawi wa jamii waanze kutoa elimu kwa uma juu ya mahusiano ya ndoa, maana inapokuja kuachana licha ya dini za kila mmoja kabla ya kufika kuchukua talaka mahakamani lazima muanzie ofisi za ustawi wa jamii.

Tangu watoto waelimishwa kwanini uingie kwenye ndoa na ukiingia ujue hiki na hiki na hiki ukitarajie na hiki na hiki unaweza usikipate na hakuna kufanana na kadhalika na kadhalika. Yaani iwe suala la kujiandaa kisaikolojia zaidi ili wanaokataa ndoa waikatae tangu wadogo.

Sio waingie kichwa kichwa halafu baada ya miezi, mwaka au miaka kadhaa wanasema ndoa haina maana.Siwalaumu maana sijui wanayokutana nayo huko, sina uzoefu ila ni swali la kujiuliza, kwanini uingie kwenye ndoa? na uingie na nani?....

Walioko kwenye ndoa pia wana jukumu kubwa kuwaelimisha uzao wao kuhusu masuala haya haswa kipindi hiki cha utandawazi.
somo la Ndoa ni gumu sana dada yangu....ninyie wawili tuuu.....unajua wengi tunaingia kwa mihemko ambukizi.....tunafikira ndoa ni furahaaa weeeeeee....tunasahau kuwa ndoa ni maisha....unfreedom life...hahaaaa...kwamba unajivua gamba....ukiingia na gamba.....utataka kuushi kisaniii...ngumu sana....mafundisho mengi ya dini zetu yamefafanua misingi ya ndoa....but kiuhalisia si mchezo.....Mungu atusaidie...
 
Niliwahi kusema humu ndani,wahenga walioweka jando na unyago sio kwamba walikuwa hawana akili,kulikuwa na faida nyingi kuliko hasara,tukaja na elimu zetu tukawaponda eti ooh tunawafundisha watoto mambo makubwa wakati bado wadogo,sasa naona unachokisema kinashabihiana na yale ya kizamani ila hiyo yako ni ya kidigitali zaidi...

Uko sawa kabisa,tuko mstari mmoja.
 
somo la Ndoa ni gumu sana dada yangu....ninyie wawili tuuu.....unajua wengi tunaingia kwa mihemko ambukizi.....tunafikira ndoa ni furahaaa weeeeeee....tunasahau kuwa ndoa ni maisha....unfreedom life...hahaaaa...kwamba unajivua gamba....ukiingia na gamba.....utataka kuushi kisaniii...ngumu sana....mafundisho mengi ya dini zetu yamefafanua misingi ya ndoa....but kiuhalisia si mchezo.....Mungu atusaidie...

Kikubwa wanasema ni kuheshimiana na kuvumiliana. Nje ya hapo ni kuumizana na kukomoana.
 
Tafuta shida iko kwa nani kwanza usikurupuke kuchukua maamuzi haraka
Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?
 
We ni ke au me
Mkuu anaedai talaka ni me au ke?///JF inabidi ibadili sheria za kujiunga hapa aghalau MTU aoneshe cheti cha diploma kwasababu jukwaa hili ndo pekee ambalo maoni yake yanasikilizwa na kufanyiwa kazi...hata tiss wengi hushinda huku hivyo kilaza kama ww bora ubaki kuwa guest tu
 
Ifike mahali watu wa ustawi wa jamii waanze kutoa elimu kwa uma juu ya mahusiano ya ndoa, maana inapokuja kuachana licha ya dini za kila mmoja kabla ya kufika kuchukua talaka mahakamani lazima muanzie ofisi za ustawi wa jamii.

Tangu watoto waelimishwa kwanini uingie kwenye ndoa na ukiingia ujue hiki na hiki na hiki ukitarajie na hiki na hiki unaweza usikipate na hakuna kufanana na kadhalika na kadhalika. Yaani iwe suala la kujiandaa kisaikolojia zaidi ili wanaokataa ndoa waikatae tangu wadogo.

Sio waingie kichwa kichwa halafu baada ya miezi, mwaka au miaka kadhaa wanasema ndoa haina maana.Siwalaumu maana sijui wanayokutana nayo huko, sina uzoefu ila ni swali la kujiuliza, kwanini uingie kwenye ndoa? na uingie na nani?....

Walioko kwenye ndoa pia wana jukumu kubwa kuwaelimisha uzao wao kuhusu masuala haya haswa kipindi hiki cha utandawazi.
Asilimia 75% ya wanaoingia kwenye ndoa husukumwa na mambo makubwa matatu ambayo kimsingi hayana tija kwenye neno LOVE!
Kwanza wengi husukumwa na MATARAJIO - expectations ! Pili wengi hutafuta unafuu wa maisha na tatu wengi Hufuata legacy ya mume mtarajiwa au mke mtarajiwa! Sasa hayo yoote yakishaanza kuondoka ama kutokuwepo kabisa ndio malalamiko ya Kusema nilikosea kuoa au kuolewa yanaanza Kuvuma! Nakinacho vunja ndoa nyingi ni usaliti unaoongozwa na tamaa ambazo nyingi huwa ni zao la kukosekana mambo matatu niliyoyasema hapo juu!
hongereni sana mliopendana kama mlivyo!
 
Uko sawa kabisaa.
 
Tuma japo kapicha basi ili tuweze kukushauri vizuri ubaki au utoke; unaeza kuta yeye ndio anakuvumilia
 
Back
Top Bottom