Maisha ya Ndoa (mahusiano) ya Wanasiasa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Salim Said, Babati
KAMPENI za uchaguzi mkuu zimezidi kunoga baada ya mgombea urais wa Chadema, Dk Slaa kumgeukia mke wa Rais Jakaya Kikwete akieleza kuwa anatumia vibaya rasilimali za nchi kumpigia kampeni mumewe huku akimtaka katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba aeleze kisa cha kufukuzwa ualimu mkuu wa shule ya msingi.

Kwa muda mrefu Salma Kikwete, mke wa Rais Kikwete na ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), amekuwa katika ziara kwenye mikoa mbalimbali, jambo ambalo limekuwa likitafsiriwa kuwa anafanya ziara za kampeni kwa ajili ya mumewe. Kwa sasa yuko mkoani Manyara.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa ambaye ameripotiwa kuwa na makombora 20 kwa ajili ya kuimaliza CCM, alisema kitendo cha mke huyo wa rais kumpigia kampeni kwa kutumia rasilimali za umma ni ufisadi.

"Mke wa rais si rais," alisema Dk Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwara ulio Babati Mjini.

"Mama Salma anatembea na askari wa serikali; magari ya serikali na wakuu wa mikoa na wilaya. Anatumia fedha za Ikulu kwa sababu walinzi wake wanalipwa na Ikulu. Huu ni ufisadi."

Dk Slaa, ambaye alikuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema), aliongeza kusema: "Nimepita huko nimeambiwa (mke wa rais) anatembea na msafara wa magari 20 na kila gari moja lina thamani ya Sh200 milioni ambayo pia yanatembea kwa mafuta ya serikali. Ni ufisadi.

"Kama mke wa rais anatembea na msafara wa magari 20, je rais mwenyewe atatembea na msafara wa magari mangapi? Wakati mgombea urais wa Chadema akitembea kwa basi, mke wa rais anatembelea magari ya serikali. Ni ufisadi mkubwa kutumia magari hayo kwa maslahi binafsi."

Aliyeanza kumlipua Mama Kikwete katika mkutano huo ni mkurugenzi wa kampeni wa Chadema, Suzan Kiwanga ambaye alidai kuwa kama mke huyo wa rais anataka kushiriki kwenye siasa angesajili chama na kuchukua fomu ya kugombea badala ya kutumia Wama.

Kiwanga alidai kuwa Mama Kikwete anafanya ziara hizo bila ya ratiba iliyoidhinishwa na Tume ya Uchaguzi (Nec), akimpigia debe mumuwe jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Nataka nimwambie huyu mtu aitwaye Mama Salma kwamba kiherehere chako kitakufikisha mahali pabaya. Unatumia fedha za wanawake za Wama kwa maslahi yako... ni kinyume cha sheria," alisema Kiwanga huku akishangiliwa.

Makombora ya Dk Slaa hayakuishia kwa Mama Salma pekee, bali pia kwa katibu mkuu wa CCM, ambaye alinukuliwa na vyombo vya habari akisema mgombea urais huyo wa Chadema anateswa na ndoa yake baada ya kuachana na Rose Kamili aliyezaa naye watoto wawili na kuanza uchumba na Josephine Mushumbusi.

Dk Slaa, ambaye ametangaza hadharani suala la kuachana na mwanamke ambaye alizaa naye watoto wawili na kuanza uchumba na Josephine, alisema: "Tukisema tuanze kutaja nyumba ndogo za kila mwanasiasa hapa, nani atabaki? Sasa naanza na Makamba. Namtaka anieleze kwa nini alifukuzwa nafasi ya ualimu mkuu katika shule ya msingi?"

Dk Slaa hakutaja sababu iliyomfanya Makamba afukuzwe ualimu mkuu wa shule ya msingi, lakini akaahidi kuwa atatoboa siri hiyo iwapo katibu huyo mkuu wa CCM hataueleza umma ukweli.

"Nyinyi wananchi hamjui kama Makamba alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi... mimi najua sasa anieleze kwa nini alifukuzwa kama mwalimu mkuu? Asiposema mimi nitamaliza," aliahidi Dk Slaa huku umma ukimsikiliza kwa makini.

Makamba, ambaye ni luteni wa zamani wa jeshi, hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
Kuhusu mwandani wake, Dk Slaa alisema: "Ni kweli niliishi na mwanamke na kuzaa naye, lakini sikufunga naye ndoa. Nilipotaka kufunga ndoa nilimtaka huyu. Kwani nani anamchagulia mtu mke."

Taarifa zinaonyesha kuwa Dk Slaa alikuwa anaishi na Rose Kamili ambaye alikuwa diwani wa CCM Karatu. Diwani huyo wa zamani wa CCM sasa amekihama chama hicho na kujiunga na Chadema.
Dk Slaa alisema baada ya kukutana na Josephine, walipendana na kuamua kufunga ndoa.

"Sasa namuuliza Makamba ni ndoa gani hiyo inamtesa Dk Slaa," alihoji mgombea huyo urais kwa tiketi ya Chadema ambaye amebobea kwenye sheria.

Kuhusu madai ya Makamba kuwa aliasi dini kwa kuamua kuachana na uaskofu, Dk Slaa alisema Chadema haitafuti uaskofu wala ushehe kwa sababu kama wangekuwa wanatafuta uaskofu, angekwishaupata miaka 20 iliyopita.

Baada ya hapo, Dk Slaa alimgeukia aliyekuwa mbunge wa Babati Mjini, Omar Kwaangw' kwamba CCM inasema Dk Slaa ananuka ukatoliki.

"Babati ni nyumbani na ndio maana nimeamua kulisemea hili hapa kwa sababu nawapenda watu wa Babati na pia nilipopata upadri mlikuja Karatu kusheherekea," alisema Dk Slaa.

Alisema wakati akiwa padri na mkurugenzi wa Maendeleo ya Jimbo Kuu la Mbulu, alijenga Shule ya Sekondari ya Singe na kumwajiri Omar Kwaangw' kwenye shule hiyo ya kanisa lakini hakuambiwa kuwa si mkatoliki.

"Nilipokuwa mbunge wa Karatu wakasema nitawezaje kuwachunga watu wa Karatu kwa madai kuwa nimeshindwa kuchunga upadri. Je nawauliza watu wa Babati nimeshindwa kuwachungwa watu wa Karatu?" alihoji na kujibiwa: "Hukushindwaa baba."

Alisema aliyoyafanya Karatu hayakuchagua Mkatoliki, Mlutheri wala Mwislamu bali kila mtu alifaidika na ubunge wake baada ya kuishinikiza serikali kushusha kodi ya kichwa nchi nzima na kufuta michango ya Mwenge wa Uhuru wilayani Karatu.

"Tukiingia Ikulu ili kulinda heshima ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwa sababu aliuwasha juu ya Mlima Kilimanjaro ili umuilike Afrika nzima, tutauchukua na kuuhifadhi katika jumba la makumbusho Dar es Salaam ili uwe maonyesho," alisema Dk Slaa.

"Pia tutafuta kodi zote za manyanyaso kwa Watanzania sambamba na kurudisha rasilamali zote za umma chini ya serikali ya Watanzania."

Baada ya hapo, Dk Slaa alimgeukia mgombea ubunge wa Babati Mjini (CCM), Kisyeri Chambiri akimtuhumu kuwa ni fisadi na hafai kuwa mbunge kwa sababu alitimuliwa kazi alipokuwa mkandarasi wa barabara ya Galapo-Kimotorok wilayani Simanjiro.

"Dk Slaa hasemi kwa kuropoka bali ana data (ushahidi). Katika jibu la swali namba 103 bungeni linasema 'baada ya kuona mkandarasi wa barabara ya Galapo kupitia kampuni ya Weasons anasuasua amefukuzwa kazi rasmi'. Hivyo mtu akifukuzwa kazi ya umma hafai kuwa mbunge," alisema Dk Slaa.

"Lakini pia Chambiri amepata nafasi ya kugombea ubunge wa Babati kwa rushwa, hivyo hawezi kupiga vita rushwa na atazidisha rushwa katika halmashauri."

Dk Slaa aliongeza kusema: "Chambiri anadai kuwa aliondoka Tarime kwa hiari, muulizeni alikutana wapi na Dk Slaa? Maana Dk Slaa ni miongoni mwa waliomfukuza Chadema mwaka 2005 tulipokwenda kumuona marehemu Chacha Wangwe."

Chacha Wangwe alikuwa mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema na alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea nje kidogo ya mkoa wa Dodoma wakati akisafiri kwenda Dar es salaam.
Dk Slaa alimtaka Waziri wa Fedha, Mustapha Mkullo aeleze ni lini bunge gani lilithibitisha na kupitisha nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa umma katika bajeti ya serikali ya 2010/11.

"Kama makamu mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni, nimepitia kifungu kwa kifungu katika bajeti yote ya serikali ya 2010/11, sikuona kipengele cha nyongeza ya mishahara, lakini wameongeza mishahara kinyemela baada ya rais kusema hahitaji kura 300,000 za wafanyakazi," alisema Dk Slaa.

Alikuwa akizungumzia taarifa za nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa umma ambazo zilibainika siku chache baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kutaarifu kuwa lingemtangaza mgombea urais anayeungwa mkono na wafanyakazi.

Tucta ilisema kuwa mgombea ambaye angetangazwa ni yule ambaye "anataka pilau lao" baada ya Rais Kikwete kueleza kwenye kikao na wazee wa Dar es salaam kuwa serikali haiwezi kuongeza kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa sekta ya umme hadi Sh315,000 na kwamba "kama ni hizo kura za wafanyakazi, basi sizitaki".

Dk Slaa aliwataka wananchi wa Babati waachane na ushabiki wa chama na wajadili maisha na maendeleo yao ili kumpata mtu atakayewaongoza vizuri.

Dk Slaa aliwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya Babati Mjini Pauline Gekul na Babati Vijijini Francis Qamara pamoja na wagombea wa udiwani wa kata za majimbo hayo.

Akiwa wilayani Kiteto, Dk Slaa alieleza mikakati yake atakapoingia Ikulu kuwa ni pamoja na kufumua mikataba yote iliyoingiwa kati ya serikali na wawekezaji na kuiunda upya ili imletee faida Mtanzania wa kawaida.

Dk Slaa alisema serikali yake itahakikisha rasilimali za Watanzania zinatumika kwa maslahi yao wenyewe na si watu wachache.

"Ndugu zangu mkitupa ridhaa yenu, naahidi kwamba tutafumua mikataba yote kati ya serikali na wahisani, ili tuondoe upotevu mkubwa wa fedha unaotokana na mikataba mibovu iliyosainiwa na serikali," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kila mwaka Tanzania inapoteza zaidi ya Sh700 bilioni kutokana na mikataba mibovu iliyoingiwa kati ya serikali na wawekezaji.

"Fedha zipo za kutosha kuondoa hali mbaya ya maisha ya watanzania, kinachokosekana ni utashi wa kisiasa wa watanzania, upendo wao na imani yao kwa Chadema," alisema Dk Slaa na kuongeza:
"Inawezekana kabisa ndugu zangu na katika kufanikisha hili hatuhitaji fedha za kigeni. Wenzetu Kenya hivi sasa huduma zote za afya, elimu na jamii ni bure. Wamewezaje hata sisi tushindwe?" alihoji

Alisisitiza kuwa, "Wakenya hawana madini sisi tunayo, hawana gesi sisi tunayo, hawana uranium sisi tunayo, tuna mengi kuliko wakenya, kwa nini wao waweze na sisi tushindwe au tumelaaniwa sisi, la bali ni utawala mbovu wa Chama cha Mapinduzi."

Source: Mwananchi.

Mtazamo: mwaka huu CCM wameshikwa pabaya hawamuwezi Dr. Slaa wakitaka amani nchi wakubali matokeo tu ya uchaguzi ama sivyo Tanzania amani itabaki historia......
 
Ooh my God. Kwa mujibu wa sheria za nchi Makamba anatakiwa kuwa gela miaka 30 na viboko 12 for this defermation.
TAMWA MPO HAPO? Au mtakubaliana na kauli ya JK, kwamba kilikuwa ni kihere here cha yule mwanafunzi?
Wadau tunaomba data zaidi. Alimdanganya kwa pipi au ubuyu? Maana hii kali.

Tena wanafungwa kama sio kuozea jela kabisa
 
Huyu 1st Lady amekuwa mzigo mno mno! (ikwa vyovyote atakuwa anatumiwa/ana idhini ya mumewe + CCM camp). Bora hata akina Siti au Ana hawakutugharimu kama huyu

Tatizo la mama Salma anashindwa kusoma alama za nyakati. Wenzie walikuwa kimya huwaoni katika mihadhara ya siasa kwani wanafanya mambo ya kimya kimya!!!!
 
Unazi wako Junius hadi unakera;Upinzani ukisemwa kwa negativities zake ndiyo kwako inakuwa kampeni lkn CCM ikianikwa negativities zake ndiyo kwako inakuwa usanii;double standards for the same dude-shame on you Junius!

Siasa za kampeni ni pamoja na kuanikwa udhaifu wako,CHADEMA au CCM lzm watumie udhaifu wa upande ungine kujizolea wafuasi na hiyo sio usanii hata kidogo bali ni mbinu,tofautisha vitu hivyo 2 utagundua kuwa unazidi kutokota hapa JF!

Hatukukusikia kuita usanii wakati CCM ilipoamua kumuita kiongozi wa juu wa CHADEMA kama ni mbumbumbu kwa sababu tu ya darasa la elimu ya 7 lkn wakashindwa kusema viongozi wao kama Makamba wana elimu gani,pia wakasahau kuwa hata "wazee wetu" waliotuongoza kwenye uhuru hadi wakaja kuongoza dola kama vile Mzee Karume au Mzee Kawawa walikuwa na kiwango gani cha elimu!

Acha unazi wako usio na msingi Junius!
Unajua Junius huwa anaongelea upenzi zaidi kuliko facts kwa hiyo mimi huwa simchukulii serious.

Unajua CCM ni wajanja sana wanahubiri kampeni za kistaarabu at the sametime wanatumia issues za upadri na ndoa ya Slaa ingawa vyote vimefeli. Ila wao wakiguswa kidogo tu wanakimbilia kwenye media tunatukanwa sasa Slaa kagundua janja yao ameanza ku hit back.

Unakumbuka kampeni za US walivyombana Obama na issue ya Pastor Jeremiah Wright na statement yake ya 'God damn America' wakati hayo maneno hakuyasema Obama lakini kwa vile alikuwa ni muumini wa Wright akahusishwa. Kampeni ni pamoja na vitu vinavyoweza kum weaken mpinzani wako lakini viwe vya kweli.
 
Tatizo la mama Salma anashindwa kusoma alama za nyakati. Wenzie walikuwa kimya huwaoni katika mihadhara ya siasa kwani wanafanya mambo ya kimya kimya!!!!

Na ofcourse by so doing awe tayari kupigwa vijembe, kashfa, kuzushiwa etc. ndiyo siasa hiyo!
 
Na ofcourse by so doing awe tayari kupigwa vijembe, kashfa, kuzushiwa etc. ndiyo siasa hiyo!

Tatizo je anaziweza siasa inataka mtu kama mama Hilary Clinton kujitokeza katika majukwaa na sio yeye maana anamtia aibu mumewe. Last week alisema kampeni ziende mpaka shuka kwa shuka sasa unadhani anaweza kuhimili tsunami za kisiasa??? Na aliyosema Dr Slaa ni ukweli mtupu na ni mjadala umekuwa ukizunguka humu kuwa nani analipia gharama za huyu mama?
 
Tatizo la mama Salma anashindwa kusoma alama za nyakati. Wenzie walikuwa kimya huwaoni katika mihadhara ya siasa kwani wanafanya mambo ya kimya kimya!!!!
Nilisha wahi kusema huu ukoo ni limbukeni wameingia siasa kichwa kichwa itakuja kuwaumbua wote kwa mpigo kuanzia baba mama hadi mtoto wao wa mwisho. Hiyo kinga ya baba yao wanayoitegemea mambo yakisarambuka nchini wasifikiri itawasaidia labda kwa kupata hifadhi nje ya nchi.

Angalia familia za marais waliotangulia wengine hata watoto wao hatuwajui, mwangalie Maria Nyerere kila mtu anampenda na kumheshimu, mwangalie Mama Sitti ingawa aliifanya ikulu kama valanda la duka lake lakini kuna ka heshima kake, njoo kwa mama Anna naye ingawa aliitumia Fulsa sawa kwa wote kama shirika lake lakini hakujihusisha na mambo ya siasa.

Sasa huyu Salma kama anataka heshima imshukie aendelee na siasa, maana siasa haina aibu itamvua nguo zote abaki uchi asianze kulalamika kuwa wanapiga ngumi za chini ya belt, na anavyoonekana ni mwepesi sana wa kurusha ngumi i mean kukimbilia kwenye vyombo vya sheria kuwa anachezewa faulo.
 
“Nyinyi wananchi hamjui kama Makamba alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi... mimi najua sasa anieleze kwa nini alifukuzwa kama mwalimu mkuu? Asiposema mimi nitamaliza,” aliahidi Dk Slaa huku umma ukimsikiliza kwa makini.

Wana JF hivi hawa viongozi wa CCM wanapokuwa wanalipuliwa hivi halafu kesho yake wakikutana kwenye vikao vyao vya ndani ya chama hivi mioyoni mwao huwa wanafikiria vitu gani? Mi nadhani kwa nafsi zao huwa wanasema Mh,nafuu mimi nina madhambi amchache mwenzangu fulani(Makamba) kazidi au huwa wanataniana wakikutana maana hii nia aibu kweli kweli. Hebu fikiria mtu kama Makamba anavyoongea kwa nyodo na kejeli vile halafu kumbe moyoni anayajua madhambi sasa ndo kaumbuka na bado, Usiwanyooshee wenzako kidole wakati vidole vyote vilivyosalia vitaku-point wewe. Tutasikia mengi mwaka huu,ila hili ni fundisho kama kuna mwingine atakayejifanya kumnyooshea kidole Dr.Slaa awe ni msafi kweli kweli kushinda hata uchafu wa Makamba maana tayari discipline ilishatembea hapo. Go Doctor go!


USIPOKUWA TAYARI KULIWA KIDOGO HULI, SASA WEWE UNATAKA KULA TU BILA KULIWA HAIWEZEKANI, HILO NALO NENO!:lol:
 
Wana JF hivi hawa viongozi wa CCM wanapokuwa wanalipuliwa hivi halafu kesho yake wakikutana kwenye vikao vyao vya ndani ya chama hivi mioyoni mwao huwa wanafikiria vitu gani? Mi nadhani kwa nafsi zao huwa wanasema Mh,nafuu mimi nina madhambi amchache mwenzangu fulani(Makamba) kazidi au huwa wanataniana wakikutana maana hii nia aibu kweli kweli.

Mama wa Mipasho Mh. Sophia Simba alishasema kwamba ndani ya CCM hakuna msafi, wakianza kunyoosheana vidole hakuna atakayesimama ... kuanzia kwenye ufisadi mpaka maisha yao binafsi (ndoa na mahusiano).

Kwa hiyo sidhani kama huwa wanashangaana maana wote wanajijua wako kwenye dampo la uchafu unaonuka, wanachojidanganya ni kwamba waanaamini watanzania hatujui kama wao wanaongoza kwa uchafu, ndio maana wakiambiwa wao ni wachafu wanakuwa wepesi wa kung'aka. Huwezi kuwa-fool wananchi wote muda, kuna kipindi inafika inakuwa ngumu kuficha uovu.
 
09_10_85xahe.jpg

Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa
akiwahutubia wakazi wa Babati Mjini mkoani Manyara katika mkutano wa kampeni jana.
 
Scandals za kila aina zitaendelea kuibuliwa wakati huu wa uchaguzi hakuna mtu safi kwa 100%.Ni vizuri vyama vya siasa vikajikita zaidi katika kunadi sera za vyama vyao na kuachana na mipasho.Kwani muda wa kampeini ni mfupi kuuza au kunadi sera za chama chako na kujibu mipasho,stay fucused on big picture SERA ZAKO.
 
Scandals za kila aina zitaendelea kuibuliwa wakati huu wa uchaguzi hakuna mtu safi kwa 100%.Ni vizuri vyama vya siasa vikajikita zaidi katika kunadi sera za vyama vyao na kuachana na mipasho.Kwani muda wa kampeini ni mfupi kuuza au kunadi sera za chama chako na kujibu mipasho,stay fucused on big picture SERA ZAKO.
Kwenye siasa haya mambo yapo huwezi kuyatenganisha, angalia nchi zinazotuzidi kidemokrsia zinazozipa umuhimu wa kwanza sera kama US na UK lakini personal attachs huwa hazikosekani sembuse sisi. Kwa taarifa yako wasikilizaji wengi kwenye mikutano ya kampeni hupenda kusikia vitu kama hivi mipasho, miziki nk ndiyo maana CCM hutumia muda mwingi kusikiliza bongo flava zaidi ya kuelezea sera. Kwenye mikutano ukienda bila muziki, bongo flava kidogo mipasho kidogo hupati mtu.
 
Malafyale,
Call me any name you want...nasimama hapo hapo kuwa kampeni za matusi hazimfawi mgombea au chama chochote, kwani mwisho wa siku si matusi, kwa wale wanaopiga kura kwa malengo, watakayochaguwa bali sera.

CCM wanampotezea mda na malengo Dr. Slaa, nayeye ameacha kampeni anaendekeza bwabwaja za akina Makamba na Kinana. Mtu akiacha mambo ya maana na kuzungumzia mambo binafsi ya watu anakuwa hana hoja huyo.

Hayo mambo 'negatives'unayosema si matusi na kukashifiana au labda niwe sijuwi maana ya kampeni, naomba unieleweshe tafadhali.
Mkuu, huu si mda wa kutafuta wafuasi,nionanvyo , bali ni mda wa kutafuta kura ambazo nazo hazipatikani kwa matusi na kashfa zidi ya mgomnbea mwengine.

Mi mnazi lakini si mnafiki, msimamo wangu nimeweka wazi, kuna mnaofuata mkumbo wa watu hata kwa mambo ya kipuuzi kama haya yasiyokuwa na faida na unaona haya mtu kuyakataza kwa kuhofia kuambiwa eti wewe si chadema.

Na juwa kwa JF usipokuwa chadema unabambikwa U-CCM, mimi sijali msimamo wangu naujuwa na sijapata kuyumba kwa mambo ya kinafiki kama ya humu JF eti wanampinga JK halafu wanakiunga mkono chama chake, umeona wapi mambo hayo? kama hafai ni yeye na chama chake
 
Unajua Junius huwa anaongelea upenzi zaidi kuliko facts kwa hiyo mimi huwa simchukulii serious.
Mkuu nilichosema ni kuwa hapana kampeni ni mipasho tu, nilichomaanisha ni hatua hii ya CCM na Chadema kurushiana matusi katika vyombo vya habari imekuwa kama mipasho ya taarabu vile. Kama upenzi mimi nina mapenzi na CUF ambacho tumezinduwa kampeni zetu kwa utulivu na hatuna mda wa kujibizana na akina Makamba na Kinana wanaolipwa kwa kazi ya kusema ovyo tu.

Bado nasisitiza kama utaona ni upenzi au unazi sawa, CCM wanawapotezea mda chadema kwa kuwaingiza kwenye kampeni za matusi ambazo wao weshazizowea, wanavitengo vya propaganda vizuri vinachochea hiyo hali na yao yanawaendea, shauri zenu!!

 
Hata mimi nilishawahi kusikia story kama hizi lakini zikafichwa fichwa si unajua wenzetu walivyo na nguvu hadi kwenye media. Lakini sasa wameyataka wenyewe siye yetu macho na masikio. Ngoja tusubiri lazima kuna mwenye angalau data zake ama walifundisha pamoja au aliguswa na tukio kwa namna moja au nyingine. Mwenye data please.

Hizi ni kampeni za kuchafuana tu na ni uzushi. kama mtu anaushahidi kamili aulete
 
Dr SLAA kwa nini ameficha uovu wa Mkamba kwa muda wote huu mrefu bila kuwaeleza wananchi ukweli? Nadhani hata akiwa rais wa nchi hii ataficha pia uovu mbalimbali utakaofanywa na viongozi wake wa chini. Hatumtaki kiongozi anayeficha maovu ya watu katika jamii hii..Kwa msingi huo SLAA hafahi kuwa rais
 
Malafyale,
Call me any name you want...nasimama hapo hapo kuwa kampeni za matusi hazimfawi mgombea au chama chochote, kwani mwisho wa siku si matusi, kwa wale wanaopiga kura kwa malengo, watakayochaguwa bali sera.

CCM wanampotezea mda na malengo Dr. Slaa, nayeye ameacha kampeni anaendekeza bwabwaja za akina Makamba na Kinana. Mtu akiacha mambo ya maana na kuzungumzia mambo binafsi ya watu anakuwa hana hoja huyo.

Hayo mambo 'negatives'unayosema si matusi na kukashifiana au labda niwe sijuwi maana ya kampeni, naomba unieleweshe tafadhali.
Mkuu, huu si mda wa kutafuta wafuasi,nionanvyo , bali ni mda wa kutafuta kura ambazo nazo hazipatikani kwa matusi na kashfa zidi ya mgomnbea mwengine.

Mi mnazi lakini si mnafiki, msimamo wangu nimeweka wazi, kuna mnaofuata mkumbo wa watu hata kwa mambo ya kipuuzi kama haya yasiyokuwa na faida na unaona haya mtu kuyakataza kwa kuhofia kuambiwa eti wewe si chadema.

Na juwa kwa JF usipokuwa chadema unabambikwa U-CCM, mimi sijali msimamo wangu naujuwa na sijapata kuyumba kwa mambo ya kinafiki kama ya humu JF eti wanampinga JK halafu wanakiunga mkono chama chake, umeona wapi mambo hayo? kama hafai ni yeye na chama chake
Junius

Mimi nilimwelewa Malafyale anakwambia unapojudge kitu usiwe na double standards, wakati mlipokuwa mna m-attach Slaa kwa upadri na ndoa yake mlikuwa hamsemi mambo ya personal attach sasa yeye ame counterattach mnasema aache personal attach kwa nini.

Kitu kingine niseme usifikiri Dr. Slaa anatumia muda wake wote kwa negatives bila kuuza sera kati ya saa nzima anayohutubia ni dakika mbili au tatu tu anachomekea sentensi ambayo inasambaa kama cheche la moto.

Hebu niambie kusema Makamba alifukuzwa ualimu kwa kubaka ilimchukua Slaa dakika ngapi. There is no politics without negatives nenda popote labda hujafanya siasa. Hizo unazosema ni siasa za kitabuni kwenye field ni tofauti, unapopanda jukwaani ukiuona umati wote unakuangalia wewe kama si mzoefu unaweza kusahau hata jina lako.
 
Kwa dhati kabisa nasema kuwa makamba ni muongeaji na mropokaji mzuri sana. Hata Januari anajua hili. Makamba ni al sahaf wetu. Nasema ni mropokaji kwa kuwa nimemsikia wakati fulani tuko sehem nae akiwapo hapo. Stori zake yataka moyo kuzisikiliza. Haangalii anaongea na nani na wakati gani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom