Maisha ya Ndoa (mahusiano) ya Wanasiasa wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya Ndoa (mahusiano) ya Wanasiasa wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Sep 2, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa vigogo wa CCM hawana ubavu wa kumnyooshea kidole kuhusu maisha yake binafsi.

  Akihutubia wananchi katika mji wa Babati, mkoani Manyara, Dk. Slaa alisema iwapo wataendelea kuacha masuala ya kitaifa na kujihusisha na maisha yake binafsi, naye atawavaa na kuwavua nguo mmoja baada ya mwingine, kwani anawajua.

  Na kwa kuanzia, alimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, awaeleze Watanzania kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi.

  Dk. Slaa alisema yeye hakufukuzwa upadri, kama Makamba anavyodai; bali aliamua kuacha kwa kufuata sheria za kanisa, na akapewa kibali kutoka Vatican kinachomruhusu kuwa mlei na kuoa.

  Alisema iwapo Makamba atadanganya wananchi kuhusu kilichosababisha afukuzwe ualimu, Dk. Slaa atamuumbua. Wajuzi wa mambo wanajua kuwa Makamba alifukuzwa ualimu (mkuu) wa shule kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mtoto wa shule.


  [​IMG]
  Dr. Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Babati jana

  Naye Mkuu wa msafara wa Dk. Slaa, Suzan Kiwanga, alimtolea uvivu mke wa rais, Salma Kikwete, akisema anatumia pesa za umma kuzunguka nchi nzima anafanya kampeni huku akijua kuwa hatambuliki katika ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Kauli ya Kiwanga iliongezewa uzito na Dk. Slaa aliyesema: "Nchi hii ina rais mmoja, ni Kikwete. Mke wa rais si rais. Anatembea kwa msafara wa magari 21 huku akilindwa na kupewa heshima zote na viongozi wa serikali; kama nani?

  Na raisi mwenyewe atatumia magari mangapi? Lakini hii yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, na huu ni ufisadi," alisema huku akishangiliwa na umati iliokusanyika katika uwanja wa Kwaraha mjini babati.

  Ilisemekana kwamba, asubuhi ya leo, kabla ya mkutano wa Dk. Slaa, Salma alitaka kuuteka uwanja huo na kuutumia kwa mikutano yake ya hadhara, lakini wananchi wa Babati wafuasi wa Chadema walimtolea macho na kumfukuza uwanjani hapo.

  Hali hii ndiyo ilisababisha kauli ya Kiwanga, ambaye alisema: "Laiti ningekuta hapa, sementi hii (sakafu) ingeheuka vumbi." Akasisitiza kwamba kama Salma anataka kufanya siasa, angechukua fomu agombee urais kama mumewe ili apate fursa ya kuzurura na kufanya mikutano. Lakini si vemam kutumia pesa za Ikulu au za WAMA kufanya siasa.

  Source: Ansbert Ngurumo blog
   
 2. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua: Slaa amrudi Makamba
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Ooh my God. Kwa mujibu wa sheria za nchi Makamba anatakiwa kuwa jela miaka 30 na viboko 12 for this defermation.

  TAMWA MPO HAPO? Au mtakubaliana na kauli ya JK, kwamba kilikuwa ni kihere here cha yule mwanafunzi?
  Wadau tunaomba data zaidi. Alimdanganya kwa pipi au ubuyu? Maana hii kali.
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  duh hili ni soo kubwa ... kwa mwendo huu naona huko mbele kuna kiza. lakini CHADEMA wasihangaike na Makamba, maana anajulikana kwamba ni msema ovyo/mropokaji na amewekwa hapo purposely ili kuwaondoa watu kwenye hoja za msingi.
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahaaaaa labda Makamba alimwambia Mkwere kuwa wanafunzi wanaviherehere na kuwa kubakwa kwao au kupewa mimba ni kutokana na hivyo so mkwere akachukua bila kuchanganya na za kwake akaropoka .

  Haya katibu mkuu wa CCM BAKAJI ,ROPOKAJI DUH KWELI MDOMO ULIPONZA KICHWA.
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilishawahi kusikia story kama hizi lakini zikafichwa fichwa si unajua wenzetu walivyo na nguvu hadi kwenye media. Lakini sasa wameyataka wenyewe siye yetu macho na masikio. Ngoja tusubiri lazima kuna mwenye angalau data zake ama walifundisha pamoja au aliguswa na tukio kwa namna moja au nyingine. Mwenye data please.
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyu 1st Lady amekuwa mzigo mno mno! (ikwa vyovyote atakuwa anatumiwa/ana idhini ya mumewe + CCM camp). Bora hata akina Siti au Ana hawakutugharimu kama huyu
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa wakina January ni watoto wa ndoa au ndio product za kubakwa ?
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nasubiri kanusho au aende mahakamani kabisa.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Ting-a-ling-a-ling......let's get ready to ruuumbleeeeeeeeee.....the gloves are off y'all.

  Ningependa kujua huyo mtoto aliyezaliwa (kama alizaliwa) ni nani? Januari au Mwamvita.....

  Na vipi kuhusu statutory rape? And what's the statue of limitations for such cases? Does anybody know? Coz if there isn't then he needs to face the music in the court of law
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hizi kampeni zimeanza kupoteza maana au mnaonaje? Kwasababu kama Dr. Slaa kaowa au hajaowa, kafukuzwa upadri au la, au kama Makamba kafukuzwa ualimu kwa kubaka au vipi...hii itawasaidia nini hawa wapiga kura hohe hahe?
  Jamani eeeh, hebu tafanyeni kampeni, hii mipasho tuwachie akina Khadija Kopa na Mzee Yussuf kwenye majukwaa yao, tupeni sera...wagombea, hatuna haja ya kusikia mambo yenu ya ujana yalikuwaje...kila mtu kapitia mambo ya ajabu kwa wakati wake, hakuna ulazima wa kuyafanya kama ajenda za kisiasa.
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hapana kampeni hapa mipasho tu!!
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  It not mipasho it is for real hizo rumours zilikuwepo ila nani wa kumfunga paka kengele mbele ya msema ovyo. Ninavyojua Makamba atakataa na hapo ndipo muziki utakapoanzia.
   
 14. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndio maana huyu mzee Yusufu makama mpaka hivi sasa na uzee wake hobi yake ni SAITI YA KATI (kitamtam cha mwili) Lana buk ,lakini halaumiki huyo mzee kwani mijajike ya mrima huko inavuvumka mapema na kufurika kila sehemu
   
 15. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  sasa wewe unamsema Kikwete kumtumia Mkewe au?maana kweli anakuwa kama ni MIPASHO TUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
   
 16. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  kaka SILAHA ni noma lazima pachimbike....kalikologa mwenyewe MAKAMBA sasa atakuwa MANYUZI kwa slaa..
   
 17. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Kikwete hana uchungu na matatizo ya uchumi wa nchi hii, ndio maana anatumia raslimali kidogo iliyopo kama Louis IV wa Ufaransa. Bi Salma naanza kumfananisha na Mary Attoinette ambaye hakuelewa kwa nini watu waandamane eti wamekosa mkate, kwa nini wasile keki basi! Salma anataka nini, tulia mwanamke kama Maria Nyerere, ndio upate kuitwa uje mbele, upewe kiti cha enzi, namna gani!
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Unazi wako Junius hadi unakera;Upinzani ukisemwa kwa negativities zake ndiyo kwako inakuwa kampeni lkn CCM ikianikwa negativities zake ndiyo kwako inakuwa usanii;double standards for the same dude-shame on you Junius!

  Siasa za kampeni ni pamoja na kuanikwa udhaifu wako,CHADEMA au CCM lzm watumie udhaifu wa upande ungine kujizolea wafuasi na hiyo sio usanii hata kidogo bali ni mbinu,tofautisha vitu hivyo 2 utagundua kuwa unazidi kutokota hapa JF!

  Hatukukusikia kuita usanii wakati CCM ilipoamua kumuita kiongozi wa juu wa CHADEMA kama ni mbumbumbu kwa sababu tu ya darasa la elimu ya 7 lkn wakashindwa kusema viongozi wao kama Makamba wana elimu gani,pia wakasahau kuwa hata "wazee wetu" waliotuongoza kwenye uhuru hadi wakaja kuongoza dola kama vile Mzee Karume au Mzee Kawawa walikuwa na kiwango gani cha elimu!

  Acha unazi wako usio na msingi Junius!
   
 19. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Kumbe hatujajaliwa viongozi waadilifu tangu! Jamani Makamba kweli? Kama ni kweli kwa nini unajipeleka kimbelembele hivi! Mungu wangu utamweleza je Januari na Mwamvita, wakikuuliza utasemaje, ni nani kati yao! Hapana najua, watu wa namna hii huwakimbia hao waliowapa mimba, na kuwatupilia mbali, labda kama watathubutu kama yule housegirl wa IGP wa zamani, jamanniiiiiiiiiiiiiiiiiii it is too much......

  Sasa huyu kwa kashfa hii si lazima aachane na kazi za Uma, Nyerere alishasema jamani, serikali (na chama) lazima wawe na miiko....
   
 20. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  jibu: Ujizaniye umesimama angalia....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...