Maisha ya mtanzania wa kipato cha chini ni mbaya mno viongozi tafuteni jawabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya mtanzania wa kipato cha chini ni mbaya mno viongozi tafuteni jawabu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anacletus, Feb 2, 2012.

 1. A

  Anacletus Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia hali ya maisha ya mtanzania wa kawaida kwa kweli ni mabaya sana na yanatisha. Yanatisha zaidi unaposikia kwamba kunawengine wanajiongezea kama posho za waheshimiwa wabunge. Inawapasa waelewe kwamba ni kazi ngumu sana kubeba mzingo ambao unaongezeka uzito kila siku mwisho wa siku mubebaji atashindwa hapo ndipo janzo cha mzigo huo kuanguka. Tanzania miaka therasini iliyopita ilikuwa na hali nzuri sana ya maisha, lakini ilikuwa na watu wachache kama milioni nane hivi. Tulikuwa na viwanda hali ya mapato ilikuwa nzuri kwa kila mtu. Sasa hivi viwanda vichache vilivyokuwepo vimekufa au kuuzwa wakulima hawalimi tena kama zamani kwa sababu ya kutoangaliwa kwa maslahi yao. Matokeo mapato yamepungua sana watu wameongezeka na wanazaliwa kila siku yaani mzigo unaongezeka kila siku VIONGOZI tutafute jawabu ya swala hili.
   
Loading...