Maisha ya mtanzania kitendawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya mtanzania kitendawili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MWananyati, Mar 11, 2011.

 1. M

  MWananyati Senior Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ilikua leo ndo mara ya kwanza kutumia daladala baada ya ongezeko la nauli zilizotangazwa na SUMATRA kwa jiji la dar es salaam. kwa kweli nimejisikia kuumia sana kwa sababu kwa mizunguko kadhaa niliyofanya nikakuta nimetumia 3,500/- wakati wiki iliyopita ilikua takribani 2,050/- kwa route hiohio. Basi nikawa natafakari na kuwaza maisha ya Mtanzania halisi ambaye kwa sasa anaishi kwa sh. 750/- kwa siku (Nusu Dola), ataweza vipi kumudu gharama hizi zinazoongezeka bila kuwa na chanzo kingine cha kuingiza kipato?
  Kwa siku moja tu, chukulia familia ya watu wa tano kwa jiji la dar es salaam;

  1. Mchele kilo 1 ----------------------- 1,500
  2. Maharagwe (soya) kilo 1 ------------ 1,700
  3. Unga kilo 1 ------------------------- 1,100/
  4. Sukari kilo 1 ------------------------ 2100/- (itatumika kwa siku 6 maximum)
  5. Mishumaa 3 (hakuna umeme) ------- 750/-
  6. Mkaa (asubuhi hadi jioni) ----------- 2,000/
  7. Sabuni mche (jamaa soap)1 -------- 2, 500/- (itatumika kwa wiki mbili)
  8. Maji ya kutumia (ndoo 5) ----------- 1,500/-
  9. Usafiri ----------------------------- 2,000/ (kukadiria tu)
  10. Mengineyo ----------------------- 2,500/- ( simu, panadol, rb polisi nk.)

  JUMLA 17,650/-

  nini cha kutegemea kutoka kwa mtu huyu?
  1. msongo wa mawazo
  2. afya mbovu na maradhi mbalimbali (lishe duni)
  3. Hasiri kwa jamii (wakati mwenye kosa serikali)
  4. kujiingiza ktk vitendo viovu km kuvuta bangi, wizi, kuuza miili(changudoa), kuuza viungo vya binadamu, lugha chafu, madawa ya kulevya nk
  5. Kuchanganyikiwa

  HALAFU waziri anaibuka na kusema 'kama watanzania wana matatizo , serikali itayashughulikia' (mh. sophia simba) kwa maana ya kuwa hadi sasa serikali haioni kama watanzania wana-matatizo makubwa sana. Aliye kivulini hamjui wa kwenye jua jamaniiii!

  TAFAKARII!!!:angry:
   
 2. a

  african2010 Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Natoa Mikopo nione
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  HIVI TUMESAHAU YALE MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA TULIAHIDIWA 2005...Kwa kasi mpya,ari mpya,nguvu mpya??????????
  HIVI HAWAKURUDIA TENA KUTUAHIDI MAISHA MAZURI..kwa nguvu zaidi,kasi zaidi, na ari zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  HAYO NDO MAISHA YENYEWE SASA!!!
   
 4. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  hapa nahisi pressure inashuka, nikisema kwenda kwa babu nauli tu kwenda na kurudi ni kamshahara kangu kwa mwezi!! du

  kweli tunakufa tunajiona!!

  nimependa sana hapo kwenye blue!!!
   
Loading...