Binti mmoja raia wa Saudi Arabia, Rahaf Mohammed, miaka 18 amewekwa kizuizini uwanja wa ndege wa Bangkok Thailand alipojaribu kuikimbia familia yake na mateso nchini Saudi Arabia. Kwa maelezo yake ni kwamba matukio yaliyomtokea ni pamoja na kukata nywele zake na familia yake kumpa adhabu ya kukaa chumbani kwa miezi 6. Ameamua kukana dini yake ya Kiislamu na hajajiunga na dini nyingine yoyote. Amekimbia kuolewa. Rahaf anadai kuwa maofisa wa Saudi Arabia nchini Thailand walimpora passport yake, na wapo watu wasiojulikana ambao wanakaa nje ya mlango wa chumba cha hotel aliyomo ili asitoroke. Anadai kuwa akirudi nchini kwake, maana wanataka kumrudisha saa chache zijazo atauawa na familia yake kwa kuwaaibisha. Wataalamu wa code of honor wataelewa maana yake na huwa wanauawa vipi kulingana na imani ya nchi aliyotoka. UPDATES. Rahaf amechukuliwa na Umoja wa Mataifa, UNHCR ambapo atatunzwa kwa siku chache huku akitafutiwa hadhi ya Ukimbizi. Inasemekana baba yake pia amewasili nchini Thailand. Serikali ya Thailand imeahidi kumpa ulinzi hadi atakapoondoka nchini humo. Vyombo vya habari na haki za binadamu vimejitahidi sana kumtetea.