Maisha ya mazoea CCM ifikie kikomo ~ hapa kazi tu!

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
MAISHA YA MAZOEA CCM IFIKIE KIKOMO ~ HAPA KAZI TU!

Nasema hivi;

Hakuna kipindi ambacho wana CCM wanatakiwa kuwa makini na siasa kama kipindi hiki.Hakuna kipindi wana CCM wanatakiwa kuacha tabia zakimazoea km kipindi hiki.Hakuna kipindi ambacho chama na jumuiya zake kinapaswa kuajiri vijana na watu wenye uwezo mkubwa wakufikiria na kupanga mikakati ya iskasa inayokwenda na wakati kama kipindi hiki.

Tunaposema vijana, umri siyo tija ingawa ni jambo la maana kwa mustakabali wa taifa na chama.Bali tunahitaji vijana wanaoweza kuunganisha kasi yao ya mwendo huku wakitumia busara na hekima wanazochota kutoka kwa wazee na waasisi wetu.Sifa siyo, sifa iwe ni uwezo wa kutenda na kufanya, kuona na kuangalia, kusikia na kusikiliza na kufanya kuyafanyia kazi yote kwa pamoja, huyo ndiye kijana apewe nafasi kufika mikoani uko, Katibu anatoa takwimu za uongo za wingi wa wanachama ama utendaji kazi zake wakati hazina ukweli na anahali ngumu na tete ya kisiasa katika eneo lake ikome.

Tunapaswa kufanya kazi kubwa ya siasa kwa umakini ili chama kiwe imara na Serikali iwe imara na hatimae Ilani ya CCM itimizwe kwani nilazima tuwe shupavu ili itekelezeke kwa 99% kwani CCM ndio chama tawala na CCM ndio yajenga nchi.

Kwani mafanikio na mipango chanya itakayotekelezeka ndio haswaa itajenga mizizi imara itakayoifikisha CCM Miaka 50+ ijayo.

Swala la uwanachama nilazima sasa tuhakikishe wanachama wa CCM wanafanyiwa vetting na mafunzo yakikada kama huko awali ilivyokuwa lazima mwanachama apitie mafunzo miezi 3 tujiridhishe kuwa kafuzu na yuko sawa ki Itikadi "NILAZIMA TUWE NA WANACHAMA WA ITIKADI NA SIO WANACHAMA WA KADI" hawa wanachama wa kadi ndio wanaotuyumbisha leo CCM kesho NCCR na ultimuamini tukampa cheo bila kujua ulaji ndio ulimleta CCM.

Wakirudisha kadi za vyama CDM na vyama pinzani vingine basi tutawapokea kisha watakaa kupewa darasa la itikadi kwa miezi 3 ili tujiridhishe kuwa anania na amekwiva.

Pia nikuhakikisha tuna Team inayochunguza mienendo ya wanachama hawa na tena iwe fear isije ikasema uwongo.

Tunahitaji mabadiliko ya kweli kama tulivyoimba katika kampeni.

Naamini kuwa tunapoelekea kumkabidhi M/kiti mpya chama basi haya yawe ni vipaumbele pia vya mambo yakushughulikiwa ndani ya chama.

Naitwa Peter Dafi

Mtetezi wa Wanyonge.
09/07/2016
huyo ndiye kijana apewe nafasi......
 

Attachments

  • 13606613_1165502916841188_6347967532382150252_n.jpg
    13606613_1165502916841188_6347967532382150252_n.jpg
    72.2 KB · Views: 35
Back
Top Bottom