Maisha ya kustaafu magumu sana kwa kada hizi

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
1. Polisi - Kwanza katika watu ambao wanaishi maisha yasiyo na stress hasa katika umiliki wa vyombo vya moto ni askari polisi, wanabebana mno, kuna askari ambao tangu wanunue gari hawajui bima, wala kukamatwa barabarani.
Pia mambo yao mengi yanaenda vizuri kwa sababu wamepewa dhamani kubwa sana katika nchi hii.

2. Wafanyakazi bandarini, tanesco, tra tanroad na mashirika ya umma hawa jamaa hawaishi kwa kutegemea mshahara
Yaani kazini ndio mipango inafanyika yaani haiwezekani usipate hela, kila wiki itapatikana mishe tu, wanapiga pesa vilakilaki hivi vya mafuta ya gari ni kawaida sana.

3. Wanasiasa hususani kama anatamani kupata madaraka akikumbuka mil 11 kila mwezi na posho za kamati hatari

Maisha ya kustaafu uyasikie tu ndugu yangu mtafute mtu aliyekuwa na mamlaka muulize akupe story usijidanganye.

Watu wa aina hii wako wengi sana unaweza kuongeza list na shida yao inakuja wakistaafu wanaanza kuishi maisha halisi

1. Heshima hakuna tena vyeo hakuna nani atakuheshimu eti ulikuwa trafki?
2. Pesa za rushwa zinakoma.
3. Wanaanza kuishi kwa pension

Mahitaji yao yako juu kipato kidogo wanaishia kufa mapema.
Na wengi wao licha ya kula sana pesa haramu maisha yao ni ya kawaida.

Nimeshuhudia afisa mstaafu mwezi 1 baada ya kustaafu hali tete.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah serikali iwe inatoa pension wa wastaafu mapema. Hizi taasisi za mikopo hizi zimeachwa zinaumiza wastaafu.
Just imagine mstaafu mmoja kaenda kukopa kwenye hizi taasisi kiasi cha 500k ampeleke mwanae shule, ameambiwa pamoja na riba jumla atarudisha 2.3M ambao ni mkopo wa mwaka mzima.

Hapo utaona riba ni 1.8M. Mtu huna namna inakubid uchukue.

Serikali waangalieni hawa wastaafu jaman, hiyo pension inapokua imekuja inatapanywa wananufaika wengne huyu mstaafu anaendelea kuishi kweny umaskini.
 
Wajinga huwa wapo tu, wanashindwa kuweka misingi ya baadae, tunawaona hao wazee mitaani walio endekeza starehe na mambo yasio ya msingi
Baadhi yao wanakuwa na miradi mizuri ya kuongeza kipato.
 
Ila kama umekua nyumbani kwenu wanafanya biadhara hata ukiajiriwa ule msingi wenu wa awali wa biashara hauwezi kufa..maisha yanaenda vizuri tu..ila wale ambao wazazi wao walikua ni watumishi halafu wakastaafu na wao wenyewe ni watumishi maisha yao hua ni mabovu sana..ila mkuu kizazi cha sasa hivi kimebadilila sana vijana wengi wakiingia kazini wakisha nunua magari mazuri, kujenga nyumba nzuri, kuoa wake wazuri, kinachofuata ni kutafuta uwekezaji wa pembeni, wale wa zamani tu ndo walikua wanafeli vipengele vya maisha baada ya kustaafu
 
Polisi ndio huwa wanazingua sana imagine mtu ametoka kwenye mshahara wa 600k+300k ya posho apo bado izo Rushwa umo road akishapewa kiinua mgongo ana jenga nyumba mana askari wengi wana stafia kota akijenga nyumba mpaka iishe Mpunga umekata anaenda kwenye kampuni za Ulinzi anakuwa hired na anaanza kulipwa 180k kwa mwezi hakuna lupu lupu ata moja afu askari elimu kwao sio kipaumbele hata kusomesha watoto kwao shida wanachojua ni kuwa na familia nyingi kila mahali then Starehe Haswa pombe na wanawake sijui swala la kukosa elimu pia linachangia wanatia huruma sana wakiingia mtaani mana biashara hawawezi
 
mnawajua askari sababu ni wengi na ni sehemu ya jamii mnazoishi.
 
Back
Top Bottom