Maisha ya Kenani Kihongosi ni somo; hii ndiyo safari yake Kiongozi

Nakubaliana na wewe. CV huwa inaonyesha achievements by merit! Kwenda kwenye mkutano China is not by merit, alishindana na Nani akapata hiyo achievement......
Umenena vyema sana....kuna ushabiki mwingi wa kipuuzi kabisa. Hakuna lolote hapo...
 
Kuna kipi cha kujifunza hapa.....hamna chochote acheni ushabiki vijana fanyeni kazi. Ujinga mtupu kusifia sifia tu. what is so special hapo? Tuna kazi ya kukuza uchumi wa nchi tukafanye kazi.
Huyu Kenan ni sehemu ya kukuza uchumi wa nchi maana nafasi aliyopata ni ya kuhakikisha Ilani ya Chama chake inatekelezwa. Kikubwa tumpe ushirikiano lakini pia kiongozi yeyote hawezi kufanya kazi akiwa pekee yake.
 
JE, WAJUA?

Maisha ya Kenani yanatupa Somo

- Amekuwa Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa

- Amekuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya vyuo vikuu Tanzania TAHLISO

- Amekuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa Tawi.

- Mjumbe wa Kamati ya siasa Kata.

- Mjumbe halmasahuri Kuu ya Wilaya.

- Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa.

- Mjumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa.

- Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa,

- Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa

- Amegombea udiwani akakosa

- Akagombea uenyekiti UVCCM wilaya akakosa

- Akagombea uenyekiti wa UVCCM mkoa akapata

- Akaenda China kuwakilisha mkutano wa kiuchumi wa Vijana 2018

- Akateuliwa kukimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa

- Akateuliwa kuwa DC Wialaya ya Arusha, baadae Akateuliwa tena Wilaya ya Iramba

- Leo Mwenyekiti wa CCM TAIFA Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Kamati Kuu ya CCM wanamteua kuwa katibu mkuu UVCCM Taifa.

Usikate tamaa, kuwa muadilifu, kuwa mzalendo, penda kujitolea na ishi kwa kuheshimu wengine. Wakati wa Mungu ukifika utainuka. Kazi iendelee

Hivi ni mimi tu ambae nimeshindwa kuona somo lolote hapa? Si kila mtu huwa anajishuhulisha na interest zake za kimaisha? Sasa ni nini kilicho special hapa cha mtu kujifunza?
 
Ajirekebishe, aache kuropoka ropoka. Kwa ujumla sasa akue. Tatizo la UVCCM ni uuaji.
Tumuamini, uongozi ni kujifunza na kadri tunavyopata nafasi ndivyo tunavyozidi kukua na kuongezeka katika ufahamu wa mambo ya uongozi.
 
Kuna fungu la pesa, ulevi na ufuska nyakati za usiku!
Haya mengine ni utashi wako. Unapolipwa kwa kukimbiza mwenge hakuna atakayekupangia matumizi ya pesa yako, ukiipeleka Bar au kununua uwanja ni wewe, ukienda kuhonga au kununua shamba la mpunga ni wewe.
 
Tumuamini, uongozi ni kujifunza na kadri tunavyopata nafasi ndivyo tunavyozidi kukua na kuongezeka katika ufahamu wa mambo ya uongozi.
Aache mihemko, mara leo anacharaza bakora watu hawa, mara kesho anasema wapinzani wachinjwe na wauawe. Ujinga mtupu kijana mdogo huyu, mtena angefika mbali sana! Ulimbukeni wake ni mwingi mno!
 
Duh kumbe mtu unateuliwa kuongoza mbio za mwenge?Si adhabu hiyo?..

Sitamani mtu aniteue kwa ujinga huo
Nafasi za kuomba kukimbiza mwenge huwa zinatangazwa, ukiamua kuomba unaweza kupata, wala siyo za uteuzi. Ila inakujengea ukakamavu na uzalendo
 
Kila mtu anapambana kwenye nafasi yake.

Wengine wanapambana huku mitaani.

Nyie mnapambana kwenye siasa!

Ova
Bavicha ukiwaambia haya hawakuelewi!

Wao wanaamini Lisu akiwa rais ndio umasikini wao utaisha

Ukiwaambia Mbowe ni tajiri wakati Lisu hajawahi kuwa hata mjumbe wake wa nyumba 10 hakuelewi.
 
Back
Top Bottom