Asante mkuu nltaka kujua hiloUnaruhusiwa kusali au kuswali na si tena mihadhara kama uraiani
Unaamini kuna watu wanamaliza zaidi ya hiyo miaka wakiwa uraiani!?hivi kwa mfano mtu amefungwa miaka 3 ndio kusema anamaliza hiyo miaka yote bila kufanya mapenzi?
Mkuu maisha ndivo yalivo.Daah,we jamaaa umefanya nkumbuke visivyokumbukika daah . .MAISHA SAFAR NDEFU Aiseee..
Hapo sawaAmebisha kuwekwa kwenye ofisi na jinsia pinzani
Kisha kukaguliwa zaidi ya saa nzima
Wadau wameelezea hapo juu
Kwamba kuna kuwa na jinsia moja na ni tukio la dakika 2/3
Huu ni ukweli mtupu.Umesaidia sana kuwafungua baadhi ya watu ambao wamekuwa na mtazamo hasi juu ya Magereza.Ni kweli si mahali pazuri pa kuishi kwasababu unaenda huko ukiwa ni amri ya Mahakama kwa makosa fulani na kwa muda specific au maisha kabisa au kifo kulingana na hukumu yenyewe.Lakini wapo wengi tu ambao kwa kuishi hayo maeneo wametoka na mengi mazuri na kusahau yale yasiyo mazuri hukohuko na hilo ndilo ambalo wengi limewasaidia kuishi tena uraiani.
Kikubwa ambacho wengi huwa kinawauma ni ule muda waliokuwa kule ndani kwasababu huku nje kuna mengi yamefanyika kwahiyo mara nyingi hilo ndilo ambalo huwa linaumiza sana kwasababu maisha na muda hausimami mtu akiwa gerezani.
Stori na kumbukumbu yako kuhusu hayo maisha ni funzo kubwa kila mmoja anayesoma habari yako na kuondoa dhana potofu juu ya maisha gerezani pamoja na changamoto zake.
We dogo mbona nakufahamu kama Ni wewe kwenye avatar?Soma miongozo ya kimataifa ambayo Magereza yetu yanafuata
Kwa asilimia kubwa hili linaukweliAROON UKIONA MFUNGWA ANATATULIWA MARINDA BAS UJUE AMETAKA MWENYEWE MAANA SYO LAZIMA, NA UKIBAINIKA MIAKA 30 INAKUHUSU.... UKIWA MKOROFI UTAPEWA ADHABU MPAKA UPATE ADABU..
Lakini ilikuwa kipindi kilefu mwaka 2002
Kabisa unachokisema na ndiyo maana hata Nelson Mandela alipofungwa mwaka 1962 huko South Africa katika Gereza la Robben Island alikuwa anaandika sana barua kwa mkewe Winnie Mandela za mapenzi na hasa kutaka kujua watoto wake wa kike aliowaacha wakiwa wadogo sana wanaendeleaje....na inasemekana aliandika barua mamia na kwa mara ya kwanza rundo la barua zilizochambuliwa kama 250 zitawekwa hadharani July 2018.Huu ni ukweli mtupu.
Kuna tulio wengi tumetoka huko na faida kubwa kuliko muda wenyewe wa kuwa huko,
Adhabu ya kutumikia jera ukijitambua ukaacha kujitetea baada ya hukumu ukaamua kupanga namna ya kuishi jera hakika huwezi umia kiasi ambacho mtu wa nje anawaza.
Tatizo
Adhabu unayokutana nayo nje magereza sasa hasa uliyopewa na jamiii inayokuzunguka aseee huwa kubwa. Unarudishwa nyuma mpaka umri, aseee
Hili tatizo la watu kufikiria jera ni jehanam ndilo linalosababisha mfungwa kuteseka nje ya jera amalizapo kifungo chake
Watu wakisikia umefungwa wanaanza kugawana mali zako mpaka mke wako kana kwamba umekufa hili jamii hailioni kama ni mateao zaidi kuliko jera lenyewe
Hawajui ya kuwa unakuwa jera huku ukiutuma moyo wako na kuukabidhi katika familia hasa pale ubapokuwa na watoto ambao walikuwa wamefikia pahala ambapo baba huwa anatengeneza historia katika vichwa wanae
Wao kirahisi tuu wanakuja wanawafanyia maajabu, mke anashindwa na changamoto mpaka anaamini katika kupotea kwako mwisho watoto waweza geuka kuwa wa mitaani huku taswira yako ikiwa haiwaishi machoni hasa pale unapofungwa mtoto anapewa taarifa lakini hajui maana yake.
Hakika ukiwa jera amini usiamini nafsi yako huwa haiko mle kwani kunawakati moyo unauma bila sababu hapo unajua tuu wanangu wako katika magumu, ukikumbuka uliwaacha kipindi ambacho bado wanaamini baba anaweza piga dunia nzima na suruhisho la kila tatizo ni baba yao sasa leo hawakuoni na jamii inayowazunguka inachukua nafasi ya kuwafinyia vile wapendavyo
Mimi huwa naamini mateso ya mfungwa hayapo jera huwa yapo nje kulingana na jamii inayomzunguka
Huduma za malazi na chakula ni haki kila mfungwa wala hakuna mfungwa special.shavu dodo ni kuridhika tu na hali halisi ya maisha.Huku kwetu Kwamtogole Juma kijana aliua akapelekwa mahabusu. Ndugu walijenga sana kesi iishe lakini wa kuambiwa anashtakuwa na Jamhuri.
Amekaa ndani miaka 10 sasa, wanaolwenda huko wanasema amenenepa shavu dodo. Familia ina contract na mkuu wa gerezani kumhudumia. Tunaambiwa chakula chake kinatoka kwa mkuu wa gereza, amepewa chumba, godoro, shuka, blanket hata mswala cha kuswalia.
miaka ya 90 mvua zilikua za shida hadi ilipokuja el nino..labda kama kwake tu mvua zilikua nzuri..na akapata pembejeo za kilimo,ambazo zilikua juu na yeye akiwa tu katoka jela..
Anafikiri nyumba ni zile za vyumba vinne
Ramani kwa archtecture
Tiles
Gypsum
Nyumba tofali linapigwa na wasela kijijini linachomwa nyumba inapandishwa na udongo siyo simenti na inakalika.
Kweli mkuu juzi kati nimenusurika, hatari sana.Ahsante kwa kutupa mawili matatu juu ya maisha ya gerezani sisi wafungwa watarajiwa maana awamu hii chochote kinaweza tokea kwa yeyote.
Hiyo ndiyo hali halisi ya ujenzi wa baadhi ya vijiji si vyote wengine wako makini na ujenzi kwa kufuata kanuni bora za ujenzi kama mjini.Kijijini watu hawacomplicate maisha, kule mtu anafyatua tofali mwenyewe ananunua tumifuko twa cement kwa ajili ya Msingi na kona pamoja na sakafu anamalizia na bati,mbao,frame za madirisha,milango maisha murua. Hapo Plasta anaweka kiporo kwa mbeleni huko!