Maisha ya Gerezani siku unapowasili na kuanza kutumikia kifungo

labda kibanda..siyo nyumba..gunia 30 kwa bei ya sasa ni shilingi ngapi?.. nashuku kwa kuwa kajua vingi akiwa jela..kulima kisasa,uhodari wa umeme,useremala


Kama unamiaka walau 40 hivi basi unaelewa hali ya Chakula vijijini ilikuwaje miaka ya tisini na ukichukulia value for money kwa bei ambayo angeuza hayo Mahindi na aina ya Nyumba ambazo wanajenga vijijini.
 
Naemcheka mfungwa ni sawa na anaemcheka mgonjwa na kumzomea marehemu kwa uzembe wake wa kupumua.


Mahabusu nimekaa miaka mitatu mkuu kusubiri uchunguzi,
Hukumu kutoka nikapigwa sita.

Ila ukikichukulia kila kitu katika mlengo chanya amini usiamini hutopata taabu
Kwenye kesi yako ulisingiziwa au ulitenda kweli?
 
Hata mm naingiaga hilo gereza la Isanga kurelease wafungwa wa kutumikia kifungo chao nje.. Hupewa nguo za kubadilisha na kwenda kubadilishia kwenye chumba na kurudi admission office already changed.. Mwaka wangu wa 8 huu katika hiyo kazi na sijawahi kuona mtu anabadilishia nguo humo humo ofisini. So sibishi naongea kitu nachokijua na nakiona almost every day in ma daily job
Magereza ni mengi mkuu
 
Mm mwezi wa kumi na mbili nimeenda ongea na client wangu, nimekaa nawasubiri client wangu naona watu wanabadilisha nguo mbele ya ofisi, hizo taratibu unazosema zipo kwenye makaratasi uhalisia hakuna vitu kama hivyo, mm nimeshamnunulia client dawa mara nyingi, wanapimwa ila dawa watajua namna ya kuzipata na hata ukipeleka muda mwingine dawa hazimfikii kabisa,
So sad
 
Mfano umefungwa na fani huwa unafanyaje mfano Mwalimu,ENGN ,MTU Wa logistic au procurement,Account na n.k huwa wanapewa tempo
Kuna Fundi kkoo gerezani alifungwa vimeo vyote vya mageleza vikafufuka akawa anakuja kununua spea peke take bila mlinzi Jamaa alipiga pesa kuliko alivyo kua uraiani maboss wakawa was Na jiuzia vimeo kwa bei poa alikua Na mwilimkubwa anashusha engine peke take Na kufunga
 
nyie acheni utani wacha jela iitwe jela.... kama hujawahi ingia kule unaweza simulia story nyingi sana za kusadikika ... lkn ukiingia kule na kutoka japo wiki tu hautasimulia kitu... ndugu yako akiwa kule alafu ukaenda kumtembelea unaweza kulia... kuna watu wale ambao wamezoea maisha magumu mtaani wao huwa wanaona simple lkn wewe umetoka kota brazameni uingie kule hakufai...
Standard za namna ya kuishi gerezani zilivyowekwa anaishi mtu yoyote yule.Siku ya kwanza ataona shida ni kweli kwasababu anaanza maisha mapya ambayo hakuyazoea lakini siku zinavyosonga akili na mwili unaanza kuzoea na ndivyo Mungu alivyomuumba mwanadamu kuweza kuishi kila aina ya mazingira ilimradi uhai wake hautishiwi kutoka kutokana na mazingira hayo then ataishi tu.Hata kama uliishi Ikulu miaka yote kwa gerezani utaishi tu na kutoka salama.
 
Hahaha huko nako pakuombea kuingia? si bora kifo aisee.
Anapenda kuzijua huduma za Magereza nyingine nyingi atazisoma lakini kuna zingine mpaka ukutane nazo mubashara ndiyo utazijua vizuri zaidi maana si zote za kusimuliana.
 
Kama unamiaka walau 40 hivi basi unaelewa hali ya Chakula vijijini ilikuwaje miaka ya tisini na ukichukulia value for money kwa bei ambayo angeuza hayo Mahindi na aina ya Nyumba ambazo wanajenga vijijini.
miaka ya 90 mvua zilikua za shida hadi ilipokuja el nino..labda kama kwake tu mvua zilikua nzuri..na akapata pembejeo za kilimo,ambazo zilikua juu na yeye akiwa tu katoka jela..
 
Haya mm nimeyajua sasa unadhani hizi ni stori za kijiweni? Narudia tena nachoandika nimeshuhudia na bado nashuhudia unayosema mm sijayashuhudia kwann niongope sasa, client wangu hawana ndugu Dodoma kila wanapoumwa napigiwa simu nikanunue dawa niwaletee
Kwahiyo wafungwa wote wa Dodoma wakiumwa ndugu zao wanapigiwa simu wakanunue?
 
Mm mwezi wa kumi na mbili nimeenda ongea na client wangu, nimekaa nawasubiri client wangu naona watu wanabadilisha nguo mbele ya ofisi, hizo taratibu unazosema zipo kwenye makaratasi uhalisia hakuna vitu kama hivyo, mm nimeshamnunulia client dawa mara nyingi, wanapimwa ila dawa watajua namna ya kuzipata na hata ukipeleka muda mwingine dawa hazimfikii kabisa,
Hali ingekuwa hiyo basi wafungwa wengi sana wangepoteza maisha....sio wote wanatembelewa na ndugu au wana ndugu...
 
Back
Top Bottom