Maisha ya Gerezani siku unapowasili na kuanza kutumikia kifungo

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ni kuwapokea na kuwahifadhi gerezani watu wote wanaoletwa gerezani kwa mujibu wa sheria za nchi na kuendesha program mbalimbali zenye kulenga kuwarekebisha wafungwa waliohukumiwa ili hatimaye watoke gerezani wakiwa raia wema. Katika kutekeleza majukumu hayo Jeshi la Magereza linawajibika kufuata na kuheshimu sheria zote za nchi pamoja na sheria mbalimbali za kimataifa zinazohusu haki za binadamu.

Unapowasili gerezani

Mtu anapowasili gerezani anahojiwa na kuchunguzwa ili; Kuelewa sheria na taratibu za gerezani
Kuelewa haki zake, pamoja na Kupata huduma za afya zinazostahili.

Halafu mfungwa anapewa namba ya Kifungo na mali zake zinaingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu na kutunzwa kwa usalama mpaka atakapomaliza kutumikia kifungo chake.

Huduma za Afya Magerezani

Wafungwa wanapewa huduma sawa za afya na matibabu kama anavyopata mtu mwingine yeyoto nje ya gereza. Matibabu ni bure ingawa ni lazima yaidhinishwe na Daktari wa Gereza

Mawasiliano
Wafungwa wanaruhusiwa kupokea wageni wa familia, marafiki na wawakilishi wa kisheria wanapokuwa gerezani.

Simu
Wafungwa hawaruhusiwi kuzungumza na kupokea simu za mkononi.

Barua
Wafungwa wanaruhusiwa kupokea na kupeleka barua. Barua zote ni lazima zikaguliwe ili kuhakikisha kuwa hazina vitu vilivyokatazwa/kupigwa marufuku au taarifa itakayohatarisha usalama na utulivu wa gereza.

Barua pepe, intaneti na mitandao ya kijamii.
Wafungwa hawaruhusiwi kutumia barua pepe, mitandao ya kijamii wala intaneti.
 
Siyo soft kama jamaa anavyosimulia.Ukifika unapelekwa kwenye ofisi ambapo unabadili nguo ulizonazo na kupewa za magereza.
Hali niliyoiona kwenye kubadili nguo ni udhalilishaji wa juu sana.Maana mtu anaambiwa avue nguo ofisini humo,kukiwa na wafungwa wengine na hata askari wa jinsia tofauti.Baada ya kuvua watachuchumaa Mara nyanyuka huku wakidhihakiwa.Nguo unaweza kuzivaa baada ya saa nzima ukiwa utupu.
 
Hii sio kweli nakataa na hilo ni gereza la wapi? Hakuna mfungwa anaebadili nguo hadharani au admission office anakopokelewa.. Na askari wa kike hawezi kuwepo ndani ya gereza hasa wanakobadilishia nguo wafungwa wa kiume,usiongee vitu vya kusadikika.
 
Kuna mshikaji mmoja alibambikiwa kesi na jirani yake akapelekwa gerezani kufika kule akakutana na kigogo mzito, akamuhoji yule kigogo akamwambia bado mdogo sana kuishi maisha ya huku, jamaa hakuamini siku anatoka alikaa wiki mbili tu, hapa tunavyoongea anasomeshwa na mke wa huyo kigogo maana kigogo bado yupo gerezani.

Nadhani kuna funzo mmejifunza hapa ila ni true story sio chai... lol.
 
Samahani mkuu! Inaonekana kuna ujumbe mzuri hapo! Fafanua, wengine ni wagumu kuelewa.
 
Hii sio kweli nakataa na hilo ni gereza la wapi? Hakuna mfungwa anaebadili nguo hadharani au admission office anakopokelewa.. Na askari wa kike hawezi kuwepo ndani ya gereza hasa wanakobadilishia nguo wafungwa wa kiume,usiongee vitu vya kusadikika.
Labda gereza la kwenye movie ndiyo wanafanya hivyo...maana kiuhalisia hicho kitu haliwezekani.anatuletea story za mtaani
 
Back
Top Bottom