Maisha ya Duniani ni makumi saba tu ( 70 yrs); Ukizidi ni Bonus.

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,635
37,844
Wana Nzengo, Kamwene?

Leo nawaambia, mkubali ama mkatae maisha ya haya ya duniani ni makumi 7 tu, kama ukizidi miaka 70 basi ni hiyo ni Bonus na wewe ni kidume.

Lakini hata huo muda wa bonus unaweza kuuchukia maana itafikia sasa unatamani yale maisha uliishi ukiwa miaka 30 - 55 lakini hutaweza kuyapata tena regardless wewe ni maskini kiasi gani ama tajiri kiasi ganii, sana sana unaweza kuwa mzigo kwa familia na hata kwa jamii inayokuzunguka because your not productive... yaani wewe ni mtu wa kulala lala, kutuma tuma, hata kwenda benki kuchukupa pesa zako hadi usindikizwe...pia, uwezo wa akili unapungua mno.

Maamuzi utakayoyafanya baada ya miaka 70+ bila kuwashirikisha wana famillia hasa watoto na mke mara nyingi yanaweza kuwa hatarishi kwa familia na mara nyingi kuleta mvurugano hasa pindi ukiondoka hapa Duniani.

Maamuzi haya uliyoyafanya ukiwa 70+ kama hayajawapendeza wana familia wako hasa watoto ama Mke wako, basi kwa umoja wao wanaweza kuyapinga mahakamani na mahakama ikawasikiliza. Sasa Mwana Nzengo elewa kwamba kumbe hata Serikali za Duniani zinatambua kabisa ukifika miaka 70+ Maamuzi yako yanaweza kuuhojiwa.

Sasa baada ya hiyo miaka 70 na ushee utaondoka hapa duniani, cover ya Nafsi ambayo tunaita ni Mwili wa Marehemu unazikwa - hauna kesi ule yoyote ile, chenye kesi kubwa ni Nafsi yako.

Marehemu anapokufa, NAFSI yake hutoka muda huo huo Marehemu anapokata roho, nafsi hii inakwenda moja kwa moja KUZIMU na si MBINGUNI kama wana Kwaya na Wainjilisti wanavyotudanganya wakati wa ibada zetu za mazishi - Mbinguni ni mahali pataakifu hakuna Nafsi ya mwanadamu yoyote yule iliyokwisha kwenda kule Hizi Nafsi zetu zote zitasubiri hukumu kwanza na zitakuwa KUZIMU tu, kwa hiyo wana Nzengo wenzangu huko KUZIMU ni kama chumba cha kusubiri daktari ama chumba na kusubiri kusafiri pale Airport.

Maisha ya kuzimu ni tofauti kidogo na maisha ya hapa duniani, kule hakuna Kula, Kuvaa, Kuugua, Kuzeeka, Kuoa ama Kuolewa - Kule ni kusubiri hukumu tu... ..kule hakuna kujipendekeza kwa wakuu wa kuzimu uli upate uteuzi ama kupandishwa cheo...kule ni haki bin haki na Nafsi yako itaishi huko hadi siku ya hukumu itimie hapo sasa ndipo utajua kama unakwenda Mbinguni kuimba na kusifu na Malaika ama unakwenda Jehanam kwa kuungana na Shetani kwenye mateso ya milele.

Kuzimu hakujai kama watu wanavyofikiri, na hesabu za miaka ya hapa duniani si kama ya kuzimu, lets say miaka 100 ya duniani yaweza kuwa ni siku mbili ama tatu za kuzimu... kwa hiyo nafsi yako itaishi huko ikusubiri hukumu ya mwisho - ile hoja kwamba itakuja kujaa hiyo sahau sababu Nafsi haina Space.

Sasa wewe mwanadamu jeuri utahukumiwa kulingana na matendo yako hapa duniani... na ni LAZIMA kila nafsi ihukumiwe hutakwepa.

Ukifikiri sana unaona haya mambo ni kweli kabisa sababu yaani maisha ya hapa duniani ukae miaka 70 tu then huna maana tena, laah na hata ukiwa kinganganizi bado akili itachoka, mwili utachoka, huwezi kufanya kitu peke yako mpaka uombe msaada....na hata kama ukiendelea kuishi hautakuwa productive, akili inarudi utotoni na hata kama ki force kufanya mambo vijjana watasema lah aisee hiki kibabu nacho kinganganiziii balaa... nk

Ewe mwanadamu mwenye kiburi miaka ya kuishi ni michache sana, jitahidi kutenda mema kadri ya mapenzi ya Muumba wako, Usiue, narudia Usiue, narudia tena USIUE. Maana hii ni dhambi kuu kuliko zote.
 
Nilimuona mzee wangu mwinyi kwenye huu msiba wa Mzee wetu mengi wakati anaamka kusalimiana na makamu wa rais Mama samia akapepesuka nadhani mama Samia alimkaza mkono asije akaanguka saa ya Mzee wetu mwinyi inasoma saa 12:58 PM.

Hii hali niliiona pia wakati wa uzinduzi wa kitabu cha I CAN I MUST ikimtokea mzee mengi kidogo nae aanguke akashikiliwa
 
"Umma wangu utaishi duniani miaka 63 basi watakao vuka hapo ni wachache sana" S.A.W
 
Wana Nzengo, Kamwene?

Leo nawaambia, mkubali ama mkatae maisha ya haya ya duniani ni makumi 7 tu, kama ukizidi miaka 70 basi ni hiyo ni Bonus na wewe ni kidume.

Lakini hata huo muda wa bonus unaweza kuuchukia maana itafikia sasa unatamani yale maisha uliishi ukiwa miaka 30 - 55 lakini hutaweza kuyapata tena regardless wewe ni maskini kiasi gani ama tajiri kiasi ganii, sana sana unaweza kuwa mzigo kwa familia na hata kwa jamii inayokuzunguka because your not productive... yaani wewe ni mtu wa kulala lala, kutuma tuma, hata kwenda benki kuchukupa pesa zako hadi usindikizwe...pia, uwezo wa akili unapungua mno.

Maamuzi utakayoyafanya baada ya miaka 70+ bila kuwashirikisha wana famillia hasa watoto na mke mara nyingi yanaweza kuwa hatarishi kwa familia na mara nyingi kuleta mvurugano hasa pindi ukiondoka hapa Duniani.

Maamuzi haya uliyoyafanya ukiwa 70+ kama hayajawapendeza wana familia wako hasa watoto ama Mke wako, basi kwa umoja wao wanaweza kuyapinga mahakamani na mahakama ikawasikiliza. Sasa Mwana Nzengo elewa kwamba kumbe hata Serikali za Duniani zinatambua kabisa ukifika miaka 70+ Maamuzi yako yanaweza kuuhojiwa.

Sasa baada ya hiyo miaka 70 na ushee utaondoka hapa duniani, cover ya Nafsi ambayo tunaita ni Mwili wa Marehemu unazikwa - hauna kesi ule yoyote ile, chenye kesi kubwa ni Nafsi yako.

Marehemu anapokufa, NAFSI yake hutoka muda huo huo Marehemu anapokata roho, nafsi hii inakwenda moja kwa moja KUZIMU na si MBINGUNI kama wana Kwaya na Wainjilisti wanavyotudanganya wakati wa ibada zetu za mazishi - Mbinguni ni mahali pataakifu hakuna Nafsi ya mwanadamu yoyote yule iliyokwisha kwenda kule Hizi Nafsi zetu zote zitasubiri hukumu kwanza na zitakuwa KUZIMU tu, kwa hiyo wana Nzengo wenzangu huko KUZIMU ni kama chumba cha kusubiri daktari ama chumba na kusubiri kusafiri pale Airport.

Maisha ya kuzimu ni tofauti kidogo na maisha ya hapa duniani, kule hakuna Kula, Kuvaa, Kuugua, Kuzeeka, Kuoa ama Kuolewa - Kule ni kusubiri hukumu tu... ..kule hakuna kujipendekeza kwa wakuu wa kuzimu uli upate uteuzi ama kupandishwa cheo...kule ni haki bin haki na Nafsi yako itaishi huko hadi siku ya hukumu itimie hapo sasa ndipo utajua kama unakwenda Mbinguni kuimba na kusifu na Malaika ama unakwenda Jehanam kwa kuungana na Shetani kwenye mateso ya milele.

Kuzimu hakujai kama watu wanavyofikiri, na hesabu za miaka ya hapa duniani si kama ya kuzimu, lets say miaka 100 ya duniani yaweza kuwa ni siku mbili ama tatu za kuzimu... kwa hiyo nafsi yako itaishi huko ikusubiri hukumu ya mwisho - ile hoja kwamba itakuja kujaa hiyo sahau sababu Nafsi haina Space.

Sasa wewe mwanadamu jeuri utahukumiwa kulingana na matendo yako hapa duniani... na ni LAZIMA kila nafsi ihukumiwe hutakwepa.

Ukifikiri sana unaona haya mambo ni kweli kabisa sababu yaani maisha ya hapa duniani ukae miaka 70 tu then huna maana tena, laah na hata ukiwa kinganganizi bado akili itachoka, mwili utachoka, huwezi kufanya kitu peke yako mpaka uombe msaada....na hata kama ukiendelea kuishi hautakuwa productive, akili inarudi utotoni na hata kama ki force kufanya mambo vijjana watasema lah aisee hiki kibabu nacho kinganganiziii balaa... nk

Ewe mwanadamu mwenye kiburi miaka ya kuishi ni michache sana, jitahidi kutenda mema kadri ya mapenzi ya Muumba wako, Usiue, narudia Usiue, narudia tena USIUE. Maana hii ni dhambi kuu kuliko zote.
Nani kakwambia kwamba kuua ni dhambi kubwa kuliko zote? Weka reference mkuu.
 
Back
Top Bottom