Maisha ya Daudi Balali: Kutoka Mchumi jadi hadi Mauti ya Upweke!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
49,274
19,609
*Wanasiasa walimtumia, mwishowe wakamtosa

*Mwisho wake ni somo kuu kwa wasomi Afrika

Na Hassan Abbas

MAISHA, siku na nyakati za Dkt. Daudi Ballali, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu hadi Januari 8 mwaka huu, yamehitimika kupitia kifo cha upweke, kilichomkuta akiwa ughaibuni huko Boston, Marekani.

Ukiangalia maisha yake ya mwanzo, kati na hatimaye mwisho, utakubaliana nami kuwa Ballali, aliyezikwa huko huko Marekani wiki hii, ameacha wosia wenye mambo mengi yenye mchanganyiko na mkanganyiko.

Na ndio maana hata kutokana na ukweli kuwa maisha yake ya mwisho yaligubikwa kwa kiasi kikubwa na kutajwa kwake kuhusika katika kashfa ya EPA, siku kifo chake kilipojulikana, baada ya kufichwa sana, wapo baadhi miongoni mwa waliokuwa wapinzani wake, walirudi nyuma na kumuomboleza.

Nafahamu kuwa Watanzania wengi, walistushwa na kifo cha Ballali, sisi tulioko katika vyumba vya habari ilikuwa ni hekaheka, kila mara watu walikuwa wakihoji kutaka kujua ukweli.Wapo waliojisahau kiasi hata cha kuuliza mambo ya hakika kama vile hivi amefia wapi, alisharudi nchini? Huku wengine wakihoji mambo magumu zaidi, nasikia kuna makachero walimfuata?

Wapo ambao baada ya kuthibitika kuwa ni kweli mauti yamemkumbuka Gavana Ballali, ubinadamu uliwajia, wakaanza kumueleza kwa staili yao, wakisema kuwa ni mtu ambaye taifa lilimhitaji sana kulisaidia katika kuusafisha ufisadi.

Katika kuonesha kuwa Ballali amekufa kifo kilichoacha upweke si kwake na familia yake tu bali kwa wengi, mwanasiasa machachari wa kambi ya upinzani, Zitto Kabwe, alipohojiwa kuhusu kifo hicho alikieleza kwa maneno ya busara kuwa kwa sasa siasa zikae pembeni, iachwe jamii na hasa familia ya Ballali ipate nafasi ya kuomboleza, kwa kuwa msiba katika utamaduni wa kiafrika ni jambo linaloenziwa kwa utulivu.

Tanzia hii haiandikwi kueleza kifo cha Ballali kilikuwaje na kama maswali mengi watanzania wanayojiuliza kuna haja yakapatiwa majibu, hapa yatapata majibu, lakini ikitokea kuna jambo litatolewa jibu, hilo halitakuwa lengo mahsusi, ni katika yatokanayo.

Si lengo la makala haya pia kumueleza Ballali kwa kina alikuwa mtu wa namna gani, mtiifu au vinginevyo, kama kuyajadili maisha yake hayo kutajitokeza, itakuwa ni kwa sadfa tu katika kufikisha ujumbe mwingine, lakini lengo moja muhimu la tanzia hii ni kumuangalia Ballalli kama mhanga wa mfumo ambao yeye amekwenda sisi tumebaki nao.

Nitamuangalia Ballali katika mtazamo wa mhanga wa mfumo uliojificha, mfumo wa nguvu za kiza, mfumo ambao, ulimtafuna ukammeza. Mfumo huo wa kimamluki wa wanasiasa kupenda kuwatumia watumishi wa umma kwa faida zao na kuugeuza uaminifu wa vijana wetu wasomi kwa sababu ya matumbo yao, ndio ambao hoja yangu katika tanzia hii, itasimama.

Ninapoyafikiria maisha ya Ballali ghafla akilini mwangu inanijia fasihi ya nguli wa Afrika, Chinua Achebe "A Man of The People," ambayo kwa ustadi inaonesha namna wasomi wa kiafrika, walio makini kutumia taaluma zao, mwisho wao unavyokuwa mgumu hasa pale wanapokumbana na nguvu za kimtandao za mafisadi wa kisiasa.

Nasema hivi kwa sababu gani? Nitakuwa wazi kadiri ya ufahamu wangu, ni jambo la hakika kwamba Ballali amekufa akiigawa jamii kutokana na ufisadi mkubwa uliotokea kwenye taasisi aliyokuwa akiiongoza, lakini jambo moja lililo sahihi sasa ni kwamba ufisadi uliofanyika BoT umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa.

Ni wanasiasa waliokiona kipaji cha Ballali 'enzi za ujana wake,' na kuvutiwa na kipaji chake katika taaluma ya uchumi, ambao 'walimpora' kutoka kwenye kazi zake za kitaaluma alikokuwa mtiifu anayekubalika na kumuingiza kwenye pembetatu chafu; ya siasa, matumaini ya watu na ufisadi.

Kwa ustadi wao wa kubaini vipaji (unaweza kuiita 'political star search'), ili badae wavitumie kwa faida yao binafsi au za kimakundi, ndipo sasa tunapaswa kuangalia mwanzo wa mwisho wa Ballali katika dunia hii.

Akiwa mmoja wa wachumi jadidi kutoka barani Afrika, Ballali 'enzi za ujana wake' anakumbukwa kwa ubobevu wake kitaaluma na mtu aliyezitumia vyema nadharia za kiuchumi alizozisomea darasani katika kutafuta majibu halisia ya kiuchumi kwa viumbe wenzake wa dunia hii.

Katika kufikia mafanikio hayo, wakati vijana wenzake wakikimbilia pale Mlimani kupata shahada zao, Ballali alilazimika kusafiri kwa boti katika safari iliyokuwa na misukosuko kuivuka bahari kubwa ya Atlantiki kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Howard, Marekani alikopata udhamini. Ni Marekani huko huko alikoendelea na masomo yake ya shahada za juu zaidi.

Kusoma kwake Marekani, ulikuwa ni mwanzo wa urafiki wake wa muda mrefu na nchi hiyo na labda, si ajabu, kwa namna alivyokuwa akienziwa huko kama mwanafunzi wa uchumi na baadaye mchumi makini, ndio maana, alichagua, ni heri azikwe ugenini asikofahamika kuliko nyumbani alikochafuliwa.

Baada ya masomo nchini Marekani alirejea nchini mwishoni mwa miaka ya 1960 ambapo, tofauti na aliporejea mwaka 1998 kushika wadhifa wa Ugavana Mkuu, wakati huo aliikuta Tanzania iliyokuwa na wasomi wachache, kazi kibao, lakini mara nyingi ikiwa ni ngumu kuchagua ufanye kazi ipi kati ya nyingi zilizokuwepo.

Wakati taasisi za Serikali zilikuwa na kazi bwerere, Chama nacho (TANU na baadaye CCM ya nyakati hizo) kilikuwa katika hekaheka ya kunyanganyana wasomi na Serikali yake, kila moja ikitaka kuwa imara.

Hivyo wakati yeye akichagua kujiunga na BoT, wasomi wasomi wenzake wa uchumi, waliotaalimika baadaye kidogo hapa hapa nchini kama Jakaya Kikwete na Ditopile Mzuzuri waliamua kushikamana na Chama.

Wakati Ditopile yeye alitangulia kuingia kwenye chama, akianza kazi siku moja na kapteni George Mkuchika, Kikwete yeye naye ilikuwa aungane na Ballali Benki Kuu, lakini katika uamuzi ambao watafiti wa historia watahitaji kuzama kuona msingi wake, Kikwete aliitosa ofa ya ajira BoT na kujiunga na TANU.

Vijana hawa wasomi wa aina ya Ballali, Kikwete na wengineo wa miaka ya mwishoni mwa 1960 na mwanzoni mwa 1970, walipokutana na wasomi waliotorokea kwenye siasa (nikichukua maneno ya Prof Haroub Othman:Nyerere An Intellectual in Power) wa aina ya Mwalimu Nyerere, lengo la kuyafikia maendeleo ya, lilipata msukumo mkuu.Utiifu ukawa dira, misheni na visheni kuu ya kufikia maendeleo ya jamii.

Akitumia nadharia na mbinu mpya za kiuchumi alizozifuna kutoka 'dunia mpya,' Ballali chini ya utendaji ulioongozwa na uongozi wa juu Serikalini uliokuwa na dhamira safi na ya wazi, alikuwa mhimili wa BoT na mfumo wa uchumi wa taifa kiasi cha kufikia wadhifa wa Mkurugenzi wa Utafiti.

Kipaji chake hicho kilionekana kwa wataalamu wa kusaka vipaji na wanaoheshimu vipaji hivyo na hapo ndipo sehemu ya kati ya maisha ya Ballali ilipoanza zama mpya alipochukuliwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kuanza safari ya utumishi unaoheshimika wa miaka 21 katika taasisi hiyo, akiishi tena, mahali alipopaenda enzi zake za uanafunzi; Washington, Marekani. Jiji la Washington yakawa si tu ndiyo makazi yake aziz bali pia mahali ambapo familia yake ikapazoea zaidi hapo kuliko hata Dar es Salaam, Tanzania.

Miongoni mwa miradi aliyoiongoza akiwa IMF na wakati fulani wakishirikiana na Benki ya Dunia, ilimfikisha hadi katika nchi za Kenya, Ghana, Lesotho, Somalia, Swaziland, Ethiopia, Sierra Leone na Afrika Kusini.

Mwanzo wa mwisho

Nimegusia awali kuhusu mkono wa wanasiasa katika maisha ya Ballali. Tuliangalie hilo kwa kina sasa. Mwaka 1998 Ballali akiwa anashughulikia kurekebisha uchumi nchini Ghana na Ethiopia katika kilele cha kulitumikia Bara la Afrika akiwa mmoja wa wachumi waandamizi wa IMF,aliyekuwa Rais wa wakati huo wa Tanzania, Bw. Benjamin Mkapa alikibaini kipaji chake.

Kama Mkapa alipanda dau, au Ballali mwenye ndiye aliona wakati umefika wa kurejea nyumbani baada ya mazungumzo yao ya kina, si la msingi sana hapa, lakini cha msingi tu ni kwamba wito wa Rais Mkapa wa kumtaka Ballali arejee nchini na kuongoza taasisi hiyo kuu ya BoT, ndio hasa ulioasisi mwanzo wa mwisho wake wa gavana huyo.

Bila yeye kujua, tofauti na alivyofanya kazi chini ya watu wanaoheshimu maadili na kanuni za kisomi pale IMF, kukubali kwake kwenda BoT, asasi kuu ya kusimamia na kuendesha uchumi wa nchi na taasisi za umma na binafsi za kifedha, lilikuwa kosa kuu, kwani pale tena si IMF, maagizo ya vijibarua, simu za vitisho, mitego na kutegana ni sehemu za kanuni kuu zinazoiendesha taasisi hiyo. Naam naye akaingia mtegoni.

Bila kujua mwisho wake ulivyokuwa ukikaribia taratibu, akiwa BoT Ballali alianza kwa kasi, akiboresha uchumi, kizalendo kabisa. Kitu kimoja ambacho wabaya na hata wazuri wake, wanakubaliana hata sasa ni kwamba kama kuna watu waliochangia katika kuuimarisha uchumi enzi za utawala wa Awamu ya Tatu, hasa baada ya uchumi wa taifa kuyumba sana enzi za Awamu ya Pili, ni Ballali.

Akizungumzia msingi wa kukua na kuimarika kwa uchumi wakati akiwa Gavana, Dkt. Ballali alipata kukaririwa akisema:

"Uchumi wetu umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6.7 hadi 7.1 sasa na haya ni mafanikio makubwa kwa Tanzania. Kama mtu angetaka kuona kiwango kama hiki basi angebidi kurejea hadi miaka ya 1950 na 1960, kwa hiyo hii ni rekodi ya kihistoria kwetu."

Kumbuka pia ni katika kipindi hiki ambapo pia Tanzania ndipo ilifikia hatua ya juu zaidi ya kufuzu kwenye vigezo vingi vya mataifa makubwa vya kuimarisha uchumi, kukuza pato la taifa na kuusimamia uchumi ukue kwa kasi zaidi kiasi cha kufaidika na nafuu nyingi ikiwemo msamaha wa madeni karibu yote.

Jinamizi la EPA, mauti ya upweke

Mwisho wa Ballali hatimaye ukaja kupitia jinamizi la EPA ambalo kwa hakika kama lisingetokea, labda leo, kifo chake, kingekuwa kikiombelezwa kwa namna nyingine kabisa; akitukuzwa zaidi kuliko sasa ambapo ubinadamu tu wa kumheshimu mfu, ndio walau umewafanya wachache, wasahau ya ufisadi na kujisikia unyonge walipopata taarifa za kifo chake.

Kuna masuala si ya kuuma maneno. Nyaraka nilizonazo, taarifa za ndani zaidi, kwa pamoja, vinajenga kile wataalamu wa sheria wanachokiita ushahidi uliovuka shaka ya kawaida (evidence beyond reasonable doubt) kuwa Ballali ameangushwa na vijimemo vya wanasiasa, ambao waliifanya BoT kimbilio la shida za fedha za kutimiza maslahi yao ya kisiasa.
Fedha zilizochotwa EPA, kwa ushahidi uliopo sasa, hata kama zilikwenda pia matumboni mwa watu binafsi, zilikuwa na malengo mahsusi ya kisiasa na ndio maana hata Serikali ya CCM kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mama Zakia Meghji, ilifikia hatua ya kuzitetea kuwa zilitumika kwa shughuli mahsusi ya kitaifa.

Kama Ballali leo akiwa yu kuzimu tunamlaumu kwa yote yaliyofanyika huku yeye na wasaidizi wake wakisaidia kuyafanikisha, twende mbali zaidi pia kwa kubaki na wosia mkuu aliotuachia kwamba suala hili, kama tunataka kuitibu kansa ya ufisadi inayojitokeza kwenye maeneo zinakotunzwa fredha za masikini, walioacha kula na kulipa kodi za Serikali, basi tunapaswa kuwakaba makoo wanasiasa wetu pia.

Katika suala la EPA tutamlaumu Ballali daima, kwa sababu alikuwa na mbinu za kuliepusha taifa na hayo hata kama alishinikizwa na wakubwa zake. Kwangu moja ya makosa yake makuu, kama alikuwa mzalendo kweli ni kwamba hata kama alikuwa akitishiwa na mtandao wa kiza afanye walichokuwa wakikitaka, ni heri angechukua uamuzi ambao kwake si mgumu, kwa sabababu hadi anakuja BoT, hakuwa mtu wa njaa;anavijisenti vya miaka 21 IMF, angelisaidia taifa kwa kuyapinga ya EPA kwa kujiuzulu.

Ukirejea uchunguzi wa kampuni ya Delloite & Touche ambao walikuwa wakaguzi wa ndani wa BoT, umejaa ushahidi wa namna nguvu za kiza zilivyokuwa zikimsukuma Ballali kusimamia uchotaji wa fedha za EPA.

Katika sehemu moja, ripoti hiyo inaonesha kuwa, Ballali aliwahi kubanwa na kwa kuwa huwa ni muaminifu wa asili, nguvu tu za kiza zinamzidi nguvu, alifikia mahali akakiri kuwa Serikali ilikuwa ikijua kufanyika kwa malipo hayo kitu ambacho kwa kubanwa sana Serikali nayo ilikiri lakini ikadanganya kwa kudai eti yalikuwa matumizi mahsusi ya kitaifa.

Neno hilo 'matumizi mahsusi ya kitaifa,' likaja kugeuka kuwa aibu kuu ya kitaifa, kwani fedha hizo baada ya kupitishwa kupitia makampuni yaliyofungua akaunti za haraka haraka, ziliishia matumboni mwa watu ambao wanafahamika, lakini miezi inakwendasasa,siku hazigandi, Serikali inadhani kwa 'kununu muda,' watu watasahau.Siamini kama itakuwa hivyo.

Ni kwa sababu hii na mwenendo huu, ndio maana katika tanzia hii, nimeamua kumuaga Ballali kwa kumlaumu lakini pia kumshukuru kuwa makosa yake, yametuachia mwanga mkubwa juu ya namna nchi yetu inavyoendeshwa na mateka wa nguvu za kiza lakini wanaotaka tuwaamini kuwa ni malaika wa mwanga, nuru na matumaini. Nenda Ballali.
 
Ugumu wa kutekeleza taaluma unatokana na mfakarno wa kuwajibika kati ya taaluma na chombo kilichomteua(wanasiasa).

Mara nyingi mteuzi hushinda hivyo kupotea kwa heshima, hekima na umaana wa taaluma ya mhusika japo huko alikotoka alikuwa moto wa kuotea mbali. Je wataalmu wetu hawaoni ukweli huu na kuwa pioneers wa kuziokoa nchi zetu changa kutoka kwa wanasiasa wanaojali kura tu?

Ni wazi kutakuwa na kuumia lakini vizazi vijavyo vitasonga mbele kwa uhakika zaidi. Japo familia ni msingi wa taifa mkazo unaowekwa sasa na viongozi wetu kuimarisha familia zao at the expense of the mass ni hatari baadaye.

Gavana mpya tuliyenaye pia amepita njia inayofanana na hiyo ya marehemu Balali, je naye atacapitulate? Yu tayari kuwaambia wateuzi wake hapana pale ambapo ndio jibu pekee muafaka ili kuiinda nchi?

Ni kweli sasa hivi nchi imesheheni wasomi na wataalamu ambao nje hujituma kishenzi lakini wapewapo hizi political posts nyumbani utaalamu hutoka kichwani na kwenda miguuni.
 
Ndugu yangu mwandishi Hassan Abbas.

Vipi na wewe leo ni msemaji wa serikali vipi unasimamia taalumana maadili yako kama ulivyomnanga Dr. Balali ama nawe unatumika na wanasiasa???

Usinipe jibu ila tafakari!
 
Hii ni michezo tu michafu ya kisiasa ya kujaribu kuwaaminisha wadanganyika kwamba Daudi Balali kafa.Hatudanyiki,Daudi Balali is alive and well.Nimeshawahi hata kuona tweet yake.
 
Mwandishi wa makala haya leo hawezi kuyaandika haya hata kidogo. Amejisahau kabisa amegeuka Kibwangai wa kwenye diwani ya Kimbunga. Hakika unafiki, uchumia tumbo vinaliangamiza taifa hili sana.
 
Ndugu yangu mwandishi Hassan Abbas.

Vipi na wewe leo ni msemaji wa serikali vipi unasimamia taalumana maadili yako kama ulivyomnanga Dr. Balali ama nawe unatumika na wanasiasa???

Usinipe jibu ila tafakari!

Anasimamia tumbo lake soni imewekwa kisogoni weledi tupa kule tunaganga njaa tu kwa sasa
 
aliefuata alipitisha ESCROW....
Ugumu wa kutekeleza taaluma unatokana na mfakarno wa kuwajibika kati ya taaluma na chombo kilichomteua(wanasiasa).

Mara nyingi mteuzi hushinda hivyo kupotea kwa heshima, hekima na umaana wa taaluma ya mhusika japo huko alikotoka alikuwa moto wa kuotea mbali. Je wataalmu wetu hawaoni ukweli huu na kuwa pioneers wa kuziokoa nchi zetu changa kutoka kwa wanasiasa wanaojali kura tu?

Ni wazi kutakuwa na kuumia lakini vizazi vijavyo vitasonga mbele kwa uhakika zaidi. Japo familia ni msingi wa taifa mkazo unaowekwa sasa na viongozi wetu kuimarisha familia zao at the expense of the mass ni hatari baadaye.

Gavana mpya tuliyenaye pia amepita njia inayofanana na hiyo ya marehemu Balali, je naye atacapitulate? Yu tayari kuwaambia wateuzi wake hapana pale ambapo ndio jibu pekee muafaka ili kuiinda nchi?

Ni kweli sasa hivi nchi imesheheni wasomi na wataalamu ambao nje hujituma kishenzi lakini wapewapo hizi political posts nyumbani utaalamu hutoka kichwani na kwenda miguuni.
 
Jamaa anaandika utadhani hiyo bank kuu,watu walikuwa wakitaka hell ya bia wanaenda kuchota tu,
EPA ilikuwa siasa ile,hata mfuko wa EPA ni hella za watu ambao hawakuwa nazo time,wenye access na information hiyo ndo wakaingia kuzikopa
 
Hii ni michezo tu michafu ya kisiasa ya kujaribu kuwaaminisha wadanganyika kwamba Daudi Balali kafa.Hatudanyiki,Daudi Balali is alive and well.Nimeshawahi hata kuona tweet yake.
Nilipita kwao Mafinga mwaka jana yawezekana jamaa alikufa au wamefreez kila kitu chake.
Pamechakaa kama sehem iliyohamwa yaan pamechoka mbay
 
Daah! kweli pata pesa / cheo tujue tabia yako, abbas ndio alikua anaandika hivi, leo hii ni uharo mtupu, kutwa kucha kutetea ujinga na ujambazi wa awamu ta tano.
Atarequest admn huu uzi ufungwe watu wasichangie
 
Kwenye Msiba wa Prof Benno Ndulu Jk amenena

Huyu Benno Ndulu nilimpendekeza amsaidie Daud Balali baada ya Balali kiniomba nimtaftie Msaidizi, na kweli alimkubali sana

Leo nipo hapa kuzika 'Maktaba' ya Uchumi Tanzania, hakuna Mchumi bingwa nchini kuwahi kutokea kama huyu!
 
So Ndulu alikua zaidi ya Balali...means Balali aliharibu kazi.
Na kwa kazi kama zile zenye mitego tamaa.michezo mibaya ya kisiasa umafia mwingi ni ngumu mtu kuomba msaidizi.

Means serekali haikuona mpaka mwenye ofisi aseme?
 
Kwenye Msiba wa Prof Benno Ndulu Jk amenena

Huyu Benno Ndulu nilimpendekeza amsaidie Daud Balali baada ya Balali kiniomba nimtaftie Msaidizi, na kweli alimkubali sana

Leo nipo hapa kuzika 'Maktaba' ya Uchumi Tanzania, hakuna Mchumi bingwa nchini kuwahi kutokea kama huyu!
Huyu JK nae ni bora akatulia zake tu huko Msoga. Ametuletea balaa kubwa sana huyu tangu aondoke madarakani 2015.

Yaani amesababisha tuishi kama mashetani! Jambo hili halikubaliki hata kidogo.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom