Joel Johansen
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 242
- 319
Naombeni tu mrudi mikoani kwenu muwaachie waliozaliwa hapo maana hao ndio wenye Dar. Nyie ambao babu zenu walihamia Dar miaka ya 60 na mlioenda Dar kwa malori na treni, mna maisha magumu hakuna mfano. Tatizo ukizoea shida unakuwa 'Surviver' matokeo yake unaendelea na routine bila kuwaza.
Kuna raha gani kubanana kwenye basi la kutoka Mbagala hadi Kariakoo huku ukiamka saa 10 usiku eti uwahi siti na kuepuka jam kisa kuwahi kazini?
Kuna raha gani kupishana na magari ya kitajiri kila siku, kujambishwa na mitaa K.V. Masaki, Osterbay na Sinza huku wewe mvua ikinyesha tu amani inakosekana, mshahara wako unaishia kweny basic needs k.v. chakula na rent?
Sikatai kuwa mikoani hakuna matabaka, lakini kuna unafuu mkubwa kwa wazawa wa mji husika kuliko wahamiaji; yaani kama hawakuja na mtaji maisha yao ni changamoto.
Kuishi kwa kuona magorofa na kufatilia siasa au burudani ati kwasababu ndio mji wa biashara hivyo siku moja unaweza kubahatika ni ulimbukeni na ukosefu wa maono. Rudini mikoani kwenu mkaendeleze mashamba na kuwa karibu na wajomba zenu ili lolote likitokea ni rahisi kusaidika kuliko huko Dar ambapo mtu huwezi hata kuchat kwa amani kwa kuhofia simu yako kukwapuliwa dirishani.