Kapeace
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 20,269
- 50,076
Misenyi ni wilaya inayoongoza mkoani kagera kwa uhaba wa chakula,, kilimo chenye tija huko ni miti tu lakini miwa!!! Yaani unalima kwa machungu halafu bei anapanga mnunuzi ambae ni mmoja tu kagera sugar ukijitia mgumu unabaki na miwa yako kaikamue utie kwenye chai sasa hivyo wakulima wanalazimika kukipa kiwanda tu kishingo upandeMkuu hayo uliyoyasema nimeyasikia leo.
Naifahamu Missenyi sana nadhani kuna kitu ulilenga kukipata huko ulipokikosa ndo ukaja na haya, lakini nikukumbushe kuwa.
1) Missenyi ina sehemu nyingi na aridhi kubwa sana ya kilimo na yenye rutuba na mvua za kutosha. Wana misimu miwili ya kulima kwa mwaka. Tofauti na maeneo mengi hapa nchini.
2) Aridhi ya huko mbali ya kwamba kwa mwaka inalimwa mara 2/ lakini huwa hawatumii mbolea hata kidogo( aridhi ina rutuba ya kutosha)
3)Mashamba ya miwa ya Kampuni ya Kagera Sugar, yanaeleweka na yana ukomo wake, ukiingia kwenye vijiji ukakuta kuna mashamba ya miwa jua haya ni mashamba ya watu binafsi tu.
4) Wanachi wa eneo hilo kwa asilimia kubwa hawategemei Kiwanda cha Sukari hata kidogo, yaani namba kubwa ya wafanyakazi wa kile kiwanda si wenyeji wa Missenyi, wafanyakazi walio wengi hutoka Wilaya ya Ngara, mkoa wa Kigoma pamoja na Mkoa wa Morogoro pia na wilaya ya Ukerewe.
5) Furusa Missenyi ni nyingi sana mbali na hicho kiwanda cha Kagera sugar pia na kiwanda cha Kahawa cha OLAM(ambacho kilifanya kazi kwa mda mfupi na kikafungwa japo sijui kama kimeshafunguliwa). Maisha ya wakaazi wa eneo hili hutegemea sana kilimo, ufugaji, uvuvi ndani ya mto Kagera, hutegemea sana biashara zinazofanyika kwenye mipaka ya Mutukula pamoja na mipaka ya Minziro, Bubare na Bugango yote mipaka hii inapakana na Uganda,
7) Pia katika shughuli za kiuchumi bado biashara zinafanyika sana hasa za mazao ya chakula ambazo mazao mengi hupata soko kwa wafanyakazi wa kiwanda cha Kagera . Vilevile mazao mengi hupata soko Bukoba mjini, na Uganda.
6) Mashamba ya miwa ya Kagera yaliyo mengi sana yako upande wa Magharibi mwa Wilaya hii na asilimia kidogo sana ni mashariki mwa Wilaya haswa kilipokuwa kiwanda cha Sukari cha zamani kabla hakijalipuliwa kwenye Vita ya Idd Amini. Hivyo sehemu za watu kulima ni nyingi sana na sidhani kama kuna mwananchi alishaingiliwa na kiwanda kuhusu aridhi ya kulima.
7) Lakini karibia mazao yote ya chakula hupatikana kwenye wilaya hii isipokuwa Mchele tu ndiyo haulimwi katika Wilaya ya Missenyi.
8) Haipo siku utasikia Missenyi ina njaa labda yatokee majanga mengine ya asili kama ilivyo ada kwa mkoa wa Kagera.
# Ni wilaya ambayo maisha yake yako chini sana na siyo gharama labda kwa mtu anayetaka mterezo tu.
# Naomba nikosololewe pale nilipoweka jambo ambalo halipo#
Misenyi chakula inakitegemea kutoka karagwe hasa ndizi,
Hiyo wilaya ngumu mnapamba kwa kuangalia kyaka na bunazi tu na sehemu za mipakani tu nendeni buyango, luzinga bwanja na kwingineko huko muone hali ya kiuchumi ilivyo, tuna roho ya choyo sana siku tukiacha hii nayo itasaidia kupambana na changamoto hizi