Maisha wilayani Missenyi ni magumu

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,041
10,456
Lengo si kudharua Bali ni uhalisia.

Kwa wasio ifahamu Missenyi ni moja kati ya wilaya zinazopatikana mkoani kagera imepakana na wilaya ya karagwe, Bukoba vijijini na nchi ya Uganda pia ni eneo ambalo linapatikana kiwanda kikubwa cha sukari KAGERA SUGAR.

1. Ni wilaya ambayo uchumi wake mkubwa unategemea mwekezaji(Kagera sugar) Trust me wewe kama sio mwajiriwa wa serikali au mwajiriwa wa kampuni ya sukari uwezi kutamani kuishi wilaya ya Missenyi

2. Ni wilaya ambayo haina mazingira rafiki kwa kilimo sababu asilimia kubwa ya eneo lake ni mashamba ya miwa ya mwekezaji(kagera sugar) maeneo yaliyobaki ni hifadhi za maliasili na tetesi zilizopo ni kuwa mwekezaji anakula njama na serikali ili wananchi wengi wasijiajili kwenye kilimo waende kufanya kazi kwenye mashamba ya miwa kama vibarua.

3. Biashara. Mzunguko wa pesa unachanganya mwisho wa mwezi na mwanzo wa mwezi tu kutokana na kuwa na wakazi wengi ambao ni waajiriwa kwenye kampuni. Kama wewe ni mfanyabiashara inabidi ujiandae kufanya biashara ndani ya vipindi hivyo tu au ukubali kufanya biashara ya kukopesha. Pia wakazi wengi bado wanakasumba ya kununua vitu gulioni ambalo ufanyika jumamosi ya kila wiki hapa mtu yupo tayari kutofanya manunuzi yoyote ndani ya wiki mpaka ifike siku ya gulio kitu ambacho ufanya maduka ya rejareja kuwa na hali mbaya.

4. Fursa za ajira ni chache kuna viwanda viwili tu vikubwa cha kahawa na sukari bahati mbaya kiwanda cha kahawa kimefugwa kutokana na masharti na sheria nyingi za serikali kitu kilichofanya kubakiwa na kiwanda kimoja tu cha sukari.

Kama wewe ni mtafutaji na unatamani kuja wilaya ya missenyi kutafuta pesa huu ni ushauri wangu kwako jiandae kisaikolojia.
 
Kuna fursa Fulani kubwa naijua iko misenyi hivi nikitaka eneo eka Moja naweza pata kwa shilingi ngapi kwa wenyeji?
Muulize Kyaka ipo wilaya ipi? Kwa bibi yake na January Makamba ni wilaya ipi? Pote huko ni miwa tu? Huyo ana yake
 
Usiniite mwongo tuheshimiane hunijui. Watu wanafukuzwa na viboko mazao yao yanafyekwa afu unajifanya unaijua missenyi sana wakati hujui kinachoendelea

BabaMorgan hebu elezea vizuri hao watu wanafukuzwa kwa viboko kutoka wapi na kwa sababu zipi wanafyekewa mazao yao? halafu hapo Missenyi ni mpakani na Uganda je hakuna uwezekano wa kupeleka Kahawa mpakani?
 
BabaMorgan hebu elezea vizuri hao watu wanafukuzwa kwa viboko kutoka wapi na kwa sababu zipi wanafyekewa mazao yao? halafu hapo Missenyi ni mpakani na Uganda je hakuna uwezekano wa kupeleka Kahawa mpakani?
Watu walitolewa kwenye mashamba wakidaiwa wamevamia misitu na kigezo kingine ni kuwa sio raia waTanzania kitu ambacho sio kweli afu kuhusu kahawa kwenda Uganda kimagendo ni kweli lakini kwa nini serikali ishindwe kuzuia usafirishaji wa magendo na kuja kudai kwamba kiwanda cha kahawa hakifuati utaratibu kitu kilichopelekea kiwanda hicho kufungwa mwaka wa pili mfululizo.
 
Muulize Kyaka ipo wilaya ipi? Kwa bibi yake na January Makamba ni wilaya ipi? Pote huko ni miwa tu? Huyo ana yake
Kwa hiyo we unapajua kwa bibi yake January Makamba tu. Inahuzunisha sana mwenzako napajua Minziro, igayaza, kabwoba, missenyi center Bubale kilimilile, Nsunga, kasambya we baki kupajua kwa bibi yake January Makamba.
 
Kama uliyoelezea ndiyo unadhani ni ugumu wa maisha basi huyajui maisha magumu, Kama watu wanapata Kazi kwenye makampuni ya miwa wewe unataka wapate Kazi zipi tofauti na hizo?

Popote maisha huwa magumu tu, kikubwa Kazi na uvumilivu tu!
 
Back
Top Bottom