MAISHA: Uzuri wa mke ni tabia. Je, uzuri wa mume ni nini?

...Bak, by the time mwanaume huyo anagundua 'anapendewa pochi,' mwanamke wa aina hiyo anakuwa keshambwaga, mwanaume anapukutisha vumbi tu mifukoni.

Labda kama kalishwa limbwata, vinginevyo ni rahisi sana kumgundua mwanamke anayekupenda kwa ajili ya pochi lako nono. Huyu ni mwizi tu anaweza hata kuuza mwili wake ndani ya ndoa kutokana na tamaa aliyokuwa nayo na kukutia aibu.
 
Ndugu yangu,
Umesema la maana kabisa.Hakuna apendaye tabia mbaya.Awe mwanamke au mwanamme, tabia ndio itakayowezesha watu kukaa pamoja iwe inanyesha au jua linawaka.Tabia mbaya ni kero na hupelekea migogoro katika mahusiano.Kuna vijitabia vidogovidogo vinavyoweza kuvumilika ila kuna tabia nyingine hazivumiiki kamwe.
Kuna waliosema kuwa uzuri wa mwanaume ni kummudu mwanamke- sasa kummudu huko kama hakutaenda na tabia njema sijui itakuwaje.Sura nayo isipoendana na tabia njema, itafikia siku itachusha au kukinaisha sijui itakuwaje.Wengine hufikiri uwezo wa kifedha na mambo kama hayo.Siku fedha itakapokwisha na huku tabia ni mbaya sijui itakuwaje!

Wale wanafiki ndio wenye hayo masharti wanayowawekea wake zao as if wanawafuga kama mifugo. Kweli kama mtu mnaheshimiana na mnashirikiana kwa kila jambo sheria kandamizi zinakuwa za nini? Mbona sisi wengine hatuna hizo sheria na maisha yetu yanaenda vizuri?

Wenye matatizo kwenye familia ndio haohao wenye masharti magumu kwa vile wanafikiri watu wote wanahusiana kama wao. Sisi hatuna sheria nyingi kwenye uhusiano wetu na tulizonazo zinatubana wote sawa bila kumu'excuse' mtu fulani kwa vile ni mwanaume na kumkandamiza mwingine kwa vile ni mwanamke.

Mimi nikichelewa kufika nyumbani lazima kabla ya kuchelewa nawasiliana na mke wangu na yeye anafanya hivyo pia. Hii inapunguza 'suspicision' na according to me kila mmoja akiwa fair kwa mwenzake maisha yatakuwa mazuri zaidi na matatizo yatapungua hata kama hamna fedha kuliko wale wanaoishi 'by convinience'. Kuishi kwa namna hii ni afadhali ya kuachana ili kila mtu ajue lake.

Hivi ni kwa nini tunaogopa kutenda mema na tunaendekeza tabia za kinafiki, uongo na ujanjaujanja usiotupeleka popote?
 
Ndugu yangu,
Umesema la maana kabisa.Hakuna apendaye tabia mbaya.Awe mwanamke au mwanamme, tabia ndio itakayowezesha watu kukaa pamoja iwe inanyesha au jua linawaka.Tabia mbaya ni kero na hupelekea migogoro katika mahusiano.Kuna vijitabia vidogovidogo vinavyoweza kuvumilika ila kuna tabia nyingine hazivumiiki kamwe.
Kuna waliosema kuwa uzuri wa mwanaume ni kummudu mwanamke- sasa kummudu huko kama hakutaenda na tabia njema sijui itakuwaje.Sura nayo isipoendana na tabia njema, itafikia siku itachusha au kukinaisha sijui itakuwaje.Wengine hufikiri uwezo wa kifedha na mambo kama hayo.Siku fedha itakapokwisha na huku tabia ni mbaya sijui itakuwaje!

Wale wanafiki ndio wenye hayo masharti wanayowawekea wake zao as if wanawafuga kama mifugo. Kweli kama mtu mnaheshimiana na mnashirikiana kwa kila jambo sheria kandamizi zinakuwa za nini? Mbona sisi wengine hatuna hizo sheria na maisha yetu yanaenda vizuri?

Wenye matatizo kwenye familia ndio haohao wenye masharti magumu kwa vile wanafikiri watu wote wanahusiana kama wao. Sisi hatuna sheria nyingi kwenye uhusiano wetu na tulizonazo zinatubana wote sawa bila kumu'excuse' mtu fulani kwa vile ni mwanaume na kumkandamiza mwingine kwa vile ni mwanamke.

Mimi nikichelewa kufika nyumbani lazima kabla ya kuchelewa nawasiliana na mke wangu na yeye anafanya hivyo pia kama akiona atachelewa. Hii inapunguza 'suspicision' na according to me kila mmoja akiwa fair kwa mwenzake maisha yatakuwa mazuri zaidi na matatizo yatapungua hata kama hamna fedha kuliko wale wanaoishi 'by convinience'. Kuishi kwa namna hii ni afadhali ya kuachana ili kila mtu ajue lake.

Hivi ni kwa nini tunaogopa kutenda mema na tunaendekeza tabia za kinafiki, uongo na ujanjaujanja usiotupeleka popote?
 
kila nikisoma swali naona mleta hoja anaulizia "uzuri wa mume" lakini majibu lukuki yanaelezea uzuri wa mwanaume!

wikiendi njema
 
Labda kama kalishwa limbwata, vinginevyo ni rahisi sana kumgundua mwanamke anayekupenda kwa ajili ya pochi lako nono. Huyu ni mwizi tu anaweza hata kuuza mwili wake ndani ya ndoa kutokana na tamaa aliyokuwa nayo na kukutia aibu.

Hivi "limbwata" ni nini hasa?
 
Mke uliye naye ulimpata baada ya kuwashinda dau wengine waliye kuwa naye kabla yako. Hapo unategemea nini?

Nishaona watu wakinyang'anyana demu kwa mbinde.
Leo demu analala huku kesho analal kule sasa ukisha mpata unadhani huyo atatulia?

Sasa hata wewe mdada unaye changanya wanaume kama mseto wa mahindi na maharage wazo lako kuu ni nini?

Ung'ang'anizi katika hatua za kuchumbia ndo kosa la awali lipelekealo watu kuanzisha Songombinde ndani ya ndoa zao.
 
kila nikisoma swali naona mleta hoja anaulizia "uzuri wa mume" lakini majibu lukuki yanaelezea uzuri wa mwanaume!

wikiendi njema

Wewe ndo umekata mzizi wa fitnah..Mawazo yako yapo juu ya mawazo ya 'kawaida'..at least ktk hili..

Kila 'mume bora' ni mwanaume..lakini kinyume chake si kweli..
 
i salute you!
Kama mume ni kichwa cha familia, hana budi kuweka familia mbele kabla a matakwa yake. Mwanaume wa namna hii atafanikiwa sana.

Kumbe jibu ulikuwa nalo. Ulitaka kujua nani ana mawazo kama yako. Wanawake ndiyo wanaotakiwa kujua sifa za mwanaume ni zipi, si wanaume hao hao kutoa tena sifa zao. So women tupeni sifa zetu ni zipi!
 
aaahhh!!!! ebwan hilo swali tena????uzuri wa mwanaume ni kuwajibika na kutimiza majukumu yako kuanzia kitandani, cumbani, sebuleni hadi jikoni. kuhakikisha familia inapata kila hitaji ndio uzuri wa mwanaume.....
 
This is very very true
Hata mwanaume mwenyewe akijijua kuwa kameet mambo hayo hapo juu,anajua kabisa kuwa hamkosi mwanamke.

Kwa zama hizi nina hofu sana na BEDROOM FACTOR NA FINANCIAL FACTOR,

Unless mtu ushaanza kuishi naye then unaweza ukajaji uwezo wake wa kitndani (bed) kwenye zama hizi za ukimwi ni shida kidogo kwenda ukijaribujaribu hata kama ndomu haitoki kwa wallet au pochi.

Financial factor, sijajua vizuri how temporaly au permernent this one should be. kwa kamtindo ka ufisadi, wizi na rushwa zilivyokaa mazee hukawii kumkuta 'the very one' ( mtarajiwa) yupo na kandambili Keko, na hata kama mali bado zipo hatima yake haijulikani.

Kifupi niseme tu kwamba uzuri wa mume upimwe kwenye uwezo wake wa kichwa (KUPEVUKA KWA AKILI) ZAIDI VINGINEVYO TUKIANGALIA HIYO VIGEZO HAPO JUU MMM HATA HAPA JF ITAKUWA KAZI KUPATA PURE HUSBAND
 
Huwa nasikia mara nyingi watu wakisema na hata kuimba ni nini.Msisitizo umekuwa kuweka vigezo vya kijumla kwa mwanamke, sijaona kukiwa na msisitizo wa vigezo vya jumla kwa wanaume.

Ninajua kila mwanamke anakuwa na vigezo vyake binafsi vya kuchagua mume anayefaa.
Naomba waungwana kujuzwa endapo kuna vigezo vinavyoweza kuangaliwa na wanawake kupima uzuri wa mume.
Nawasilisha.

Ingawa kuna attributes nyingine, lakini kikubwa kwa mwanaume ni mkwanja! Asikuongopee mtu..kama mwanaume huna kitu mfukoni..hata ungekuwa handsome namna gani..ni wanawake wachache sana-if any, wanaoweza kukaa na wewe...Hizo slogani za uzuri wa mke/mume ni tabia..I am sorry to say..ni attributes za kina dada zetu. Kwa mwanaume..tabia, love, just mention them..come after the status of your pocket has been ascertained.

Najua wengi tuna maoni tofauti lakini hii inakuwa reinforced na ile mentality (which is true, partly) kwamba mwanaume ndo provider wa familia!

Masanja,
 
Uzuri wa mume ni mapenzi

Mkuu,
kweli kabisa..ila mapenzi ni dhana pana....inahitaji ufafanuzi.Nadhani kila binadamu ( awe mwanamke na mwanamme) anahitaji kupendwa.Mapenzi pekee bila vikorombwezo vingine....mhhh!Sijui.
 
Huwa nasikia mara nyingi watu wakisema na hata kuimba ni nini.Msisitizo umekuwa kuweka vigezo vya kijumla kwa mwanamke, sijaona kukiwa na msisitizo wa vigezo vya jumla kwa wanaume.

Ninajua kila mwanamke anakuwa na vigezo vyake binafsi vya kuchagua mume anayefaa.
Naomba waungwana kujuzwa endapo kuna vigezo vinavyoweza kuangaliwa na wanawake kupima uzuri wa mume.
Nawasilisha.
uzuri wa Mume pesa tu
 
Kuna jamaa alitoa sifa hizi hapa hapa JF; mume shurti awe 1) hodari wa mapenzi (kujamiiana), 2) awe na pesa na amwachie mkewe apange namna ya kuzitumia na 3) awe mtu wa kumsikiliza mkewe.
Mwanaume akiwa hivi mbona ndoa inakua tamu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom