MAISHA: Uzuri wa mke ni tabia. Je, uzuri wa mume ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAISHA: Uzuri wa mke ni tabia. Je, uzuri wa mume ni nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Dec 20, 2008.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huwa nasikia mara nyingi watu wakisema na hata kuimba ni nini. Msisitizo umekuwa kuweka vigezo vya kijumla kwa mwanamke, sijaona kukiwa na msisitizo wa vigezo vya jumla kwa wanaume.

  Ninajua kila mwanamke anakuwa na vigezo vyake binafsi vya kuchagua mume anayefaa.

  Naomba waungwana kujuzwa endapo kuna vigezo vinavyoweza kuangaliwa na wanawake kupima uzuri wa mume.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mwanaume, waume wa wake zetu, ni kama sisi. Tunaojua uzuri wa mke kuwa ni tabia. Tabia hapa ina maana ni pamoja na kumuelewa mmeo kwa namna zote.

  Kila mwanamme yuko tofauti, ndiyo maana hakuna kitu kama uzuri wa mme ni kitu fulani...! Mwanamke ni DEPENDENT parameters na mwanamme ni FACTOR (deciding).

  Kwa hiyo acha maneno yako kabisa ya uzuri wa mwanamme!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa mume ni upendo wa dhati kwa mkewe-na familia yake. Ni upendo ndio utamfanya awe na power to support familia.

  Ni upendo ndio utampa nguvu ya kuprotect familia yake.
  Ni upendo ndio utamfanya ampende mkewe na kumwamini.
  Ni upendo ndio utamshibisha mume kwa penzi la mkewe
  Ni upendo ndio utamzuia mume kumsaliti mkewe.
  Ni upendo ndio kila kitu na mengine yote yatafuata.

  Uzuri wa mke tabia na uzuri wa mume kupendwa.

  Ukipendwa wewe mke waweza lala njaa na furaha moyoni.
  Ukipendwa mwili wako unapata uwezo wa kutoa peenzi la shibe.
  Ukipendwa hata utongozwe vipi hutongezeki.
  Ukipendwa unapata furaha ya asili ambayo ndio esence ya life.
  Ukipendwa unapata nguvu za ajabu kumfanya mumeo afanikiwe.

  Hivyo amri kuu kuliko amri zote kwa wanandoa ni upendo.
   
 4. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2008
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa alitoa sifa hizi hapa hapa JF; mume shurti awe 1) hodari wa mapenzi (kujamiiana), 2) awe na pesa na amwachie mkewe apange namna ya kuzitumia na 3) awe mtu wa kumsikiliza mkewe.
   
 5. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli saikosisi. Nice and simple.
   
 6. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nafikiria wengi wetu hapa Tz huanzia na uzuri wa sura kwanza ndio tukaendelea kuangalia tabia uuri wa sura ndio unaomfanya mtu kuvutiwa na mpenzi kwanza halafu ndio tabia.

  Tofauti na nchi nyingine katika Bara la afrika kwa mfano Wanageria hawangali sura wao as long ni mwanmke au mwanamme inatosha kwao na ndio leo utakuta kuwa wasichana wa kinageria hawana tafauti kisura msichana anakuwa na sura la kiume hii inatokana na wao wakitafuta wapenzi hawangali yupe anamvutio wa kike
   
 7. u

  utu wangu Member

  #7
  Dec 21, 2008
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  As a man thinketh...so is he!!!

  As water reflects a face...so the man's heart reflects a man
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Uzuri wa mwanaume ni kuipenda familia yake kuliko nafsi yake.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  i salute you!
  Kama mume ni kichwa cha familia, hana budi kuweka familia mbele kabla a matakwa yake. Mwanaume wa namna hii atafanikiwa sana.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  nakubaliana nawe kuwa kila mwanaume ni tofauti kama ilivyo kuwa kila mwanamke ni tofauti.Wachangiaji wenzio nadhani wameelewa suali langu na wameweza kunionyesha baadhi ya sifa za mume mzuri!
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...huenda, 'anavyommudu' mkewe! (?).
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  kummudu?
  Ni swali au ni jibu?
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hilo ni jibu...
   
 14. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Unajua tatizo ni mila zinazowakandamiza wanawake. Wanawake wamekuwa 'defined' wanapaswa wavaaje, watembeeje na wawe na tabia gani etc.

  Mimi huwa nakerwa na hii 'mindset'. Kwa mtazamo wangu kila mtu - mme na mke - anapaswa awe na tabia njema, amweshimu mwenzake na aone huyo mwenzake anastahili heshima kama yeye anavyoshtahili. Nje ya haya ni matatizo matupu!
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu,

  Umesema la maana kabisa.Hakuna apendaye tabia mbaya. Awe mwanamke au mwanamme, tabia ndio itakayowezesha watu kukaa pamoja iwe inanyesha au jua linawaka. Tabia mbaya ni kero na hupelekea migogoro katika mahusiano. Kuna vijitabia vidogovidogo vinavyoweza kuvumilika ila kuna tabia nyingine hazivumiiki kamwe.

  Kuna waliosema kuwa uzuri wa mwanaume ni kummudu mwanamke- sasa kummudu huko kama hakutaenda na tabia njema sijui itakuwaje.Sura nayo isipoendana na tabia njema, itafikia siku itachusha au kukinaisha sijui itakuwaje. Wengine hufikiri uwezo wa kifedha na mambo kama hayo.

  Siku fedha itakapokwisha na huku tabia ni mbaya sijui itakuwaje!
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Wanawake wa siku hizi ukitimiza hapo basi umemaliza...
   
 17. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2008
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo yoyo ulipo chukua five from me yani! Leo umenigusa mmpaka kumoyo. Maana unakuta jamaa majamboz haliwezi, pesa nayo anakuwa bahili nayo utafikiria utenda kujengea kweni ili hali mijumba tunayo kedekede. Ukija kwenye kumsikiliza mke yeye ndo mbishi kama shipa! Kweli hapo kuna mume au statue!
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Dec 22, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lorain, wewe umeolewa, umechumbiwa, una boyfriend, au unatafuta?
   
 19. BrownEye

  BrownEye Member

  #19
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi, Mwanamume mzuri ni yule MWENYE AKILI, Yaani yule awezaye kuishi na mkewe kwa akili. Mtamjua kwa matendo yake na katika mafanikio ya ndoa na familia yake
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Yah hii ndio yenyewe kitu tulishazungumziaga kipindi fulani tulikuwa tunampeleka jando kwa mara ya mbili kijana mmoja aliyekuwa akizinguliwa na mahaba.

  Ni sifa tatu zinazotakiwa kuwa kwa mtu mmoja ili kuweka uhusiano stable.
  1.Good in bed :kama alivyosema mjumbe hapo juu uhodari katika mapenzi ( pia match with her uniqueness maana si anajopenda binti kondo na zaituni anapenda )

  2.Financial Fit : Hii inahusisha security/uhakika nadhani kila binadam anakuwa ame settle kama anajua likitokea tatizo lolote kuna mtu atasaidiana naye au atachukua jukumu la ku resolve.Kama kidume unatakiwa kuweza kulinda falimila yako ili mkeo awe na amani na ule tunda kwa nafasi.Kwa sababu hizi vinapelekea kuwa uwe financial fit mpe mama pesa za kufanya atakavyo hata akijenga kwao shega tu.

  3.Care: hii inahusisha kumsikiliza mke inamfanya ajione mnajali na unajali hisia zake,kipindi kingine wankuwa unreasonable basi ww fanya wanvyotaka once in a while ili mradi hakina madhara makubwa.Mnunulie zawadi na kadharika ,kwa wanume wengine haina tofauti mtu akupatie zawadi asikupatie most of us we 're indefferent about that kwa hiyo tunajisahau kama kwa wenzitu inaweza kuwa na maana kubwa.

  Haya ndio mafiga matatu yanayoinjika jungu bila taflani, si rahisi kwa mtu kwa na vyote japo wapo walijaaliwa.Ndio maana tunaomba wenzi wetu wawe na imani.Nasi tujitahidi kuflow na hivi mimi nimevipanga kwa priority, naamini katika namba moja kuwa ina overshadow vingine kwa kiasi kikubwa na pale tunaweza kuongelea kwa kirefu ila na assume mojority tunajua kinachotatikana .

  Make sure unakuwa na mtu mnaye randana /match na ndio maana inaitwa marriage/kuoana kama bolt na nut ili zitumike pamoja lazima zi match and by that they form so called marriage/vimeoana
   
Loading...