Maisha unayopaswa kuishi baada ya kuachana na mpenzi wako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,905
6,691
Kweli hakuna anayefurahia kuachwa. Mapenzi yanauma, wakati mwingine hasira zinaweza kutuongoza katika kufanya maamuzi lakini suala la msingi linalopaswa kuzingatia ni kujidhibiti. Lazima tujifunze kudhibiti hasira zetu.

Kuachwa au kuachana siyo mwisho wa maisha. Kweli mnaweza kuwa mmewekeza nguvu, ndugu na hata marafiki katika uhusiano wenu lakini endapo imetokea mmeshindwa kuendelea na safari kwa namna moja au nyingine basi hakuna budi kushukuru na kuliacha lipite.

Usimuone mwenzako kama adui bali chukulia kama changamoto katika maisha yako kwani hujui pengine ni nini kingetokea kama ungeendelea na safari hiyo. Yawezekana Mungu amekuepusha na jambo lingine zito huko mbeleni.

Mshukuru yeye, usiwachukie marafiki, usiwakasirikie ndugu zake wala yeye mwenyewe. Mchukulie kama tu alikuwa mpenzi wako. Mheshimu maana pia anazo siri zako nyingi. Anakujua vizuri hivyo kama itakupendeza pia muombee mafanikio.

Muombe naye akuombee pia wewe katika safari yako. Kama una shida ambayo unaona yeye anaweza kuwa msaada kwako, mueleze. Kama atakuwa ni muungwana anaweza kukusaidia. Zungumza na marafiki na ndugu zake kama vile hakuna kitu chochote kilichotokea.

Yawezekana hili likakushinda katika kipindi cha awali lakini jipe moyo. Baadaye utaweza. Msalimie ukimuona barabarani. Hii inakufanya uonekane mstaarabu hata kwa ndugu zake hivyo itakuwa jambo jema pia kwao hata kuweza pia kufufua upya penzi lenu.

Kuna fursa ambazo anaweza kukupa au wewe ukampa hata kama mmetengana. Weka uhusiano pembeni, ruhusu moyo wako uwe katika hali ya urafiki. Urafiki utakupa fursa nyingi na endapo yeye au wewe utampata mwenza basi mtaambizana.

Kila mmoja atakuwa huru na hapo kidogo mawasiliano yanaweza kupungua ili kuepuka migogoro na wenza wenu wapya lakini inapowezekana mnaweza kusalimiana. Hayo ndiyo maisha na hakuna sababu ya kuwekeana chuki katika dunia hii iliyojaa nafasi nyingi maishani.
 
Kata kamba mazima, hakuna cha kumpigia ndugu yake wala mandugu yake....labda apige yeye..sina muda mchafu. Namba nilishafuta kitamboo..wanini sasa kwani anayo yeye tu akhaa..
 
Umeachana na mtu,eti unampigia simu ili?
SIkumjulia hali kipenzi cha zama jamani...watoto wako??...kwani kuachana ugomvi??...unaweza kukumbuka mambo yetu yale yalivokuwa yana noga...kuna ubaya kwa hilo akilijua??? ...unamtania kidogo michezo yenu ile!!.....na siku hizi unavo li misss hilo!...basi ni afyaaa tuuu!
 
Back
Top Bottom