MAISHA: Umewahi fikiria kujiua? Nini kilikuzuia?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,645
2,000
Nimewahi tena mara nyingi na bado mawazo hayo hunijia, hali inakuwaga mbaya hadi nafiikiriaga kutumia unga sema hizi coctail za bongo ni kujiongezea matatizo, mwisho naamua kupiga gambe tu.

Ila nikifikiria watu kama nabii Daniel na Ayubu naona yanayonipata si kitu ukilinganisha. pia naona kujiua ninakuwa kama msaliti kwa ndugu zangu (kwa sisi ambao ndugu wanatuangalia kwa macho ya matumaini).

Kama na wewe mwana MMU umewahi fikiria hivyo tuhabarishe kwanini hukujiua na mbinu gani ulitumia ku cope? (hakuna haja ya kusema kwanini ulifikiria kujiua)
 
Baraka Roman

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
692
0
Du sijawahi kufikilia,nasababu kubwa nikifikilia picha yakabuli uwiii,kuwekwa mule then mfuniko unawekwa juu.daa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
badiebey

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
5,876
1,500
Nshafikiria once,kuna kitu nlikifanya kw bidii sana af hakikufanikiwa kw muda nliodhania,af at th same tym nimeachwa,moyo uliumaje,i wanted to give up everythn,.nashukuru Mungu alinisaidia,nilikuwa ssiwezi kula wala kulala nalia na kusali,baada ya km mwez lile jambo likafanikiwa,nilishindwa nieleze vip kw watu kuomba msaada,shetan azidi kushindwa na alegee,
ukiwa na shida mueleze Mungu he wl surely take care of it better than anyone
 
gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,851
2,000
Sijawahi kufikiria kujiua na ni kwasababu i have strong belief and suicide is against my belief....I have been through a lot of misery in my life but i believe i am gifted this life for some reasons so i wouldn't give it up in return for anything...ONLY THE ONE WHO GAVE ME THIS LIFE CAN TAKE IT!!...
Even when i am so down,i want something so bad I´LL DO MY BEST,try every safe option available for me so that i wont have regrets later that i could do something better or try harder...And its incredible who much i might be to willing sacrifice just to achieve my goals...That ideology keeps me strong!And i always pray and thank my god for everything even if its pain or misery....Cause GOD knows whats best for me!!!
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,876
2,000
mi nimewahi tena mara nyingi na bado mawazo hayo hunijia. Hali inakuwaga mbaya hadi nafiikiriaga kutumia unga sema hizi coctail za bongo ni kujiongezea matatizo, mwisho naamua kupiga gambe tu.

Ila nikifikiria watu kama nabii daniel na ayubu naona yanayonipata si kitu ukilinganisha. Pia naona kujiua nnakuwa kama msaliti kwa ndugu zangu (kwa sisi ambao ndugu wanatuangalia kwa macho ya matumaini).

kama na wewe mwana mmu umewahi fikiria hivyo tuhabarishe kwa nini hukujiua na mbinu gani ulitumia ku cope?(hakuna haja ya kusema kwanini ulifikiria kujiua)

una hitaji msaada mkubwa wa kisaikolojia. Hapo kwenye red unaonesha una hali mbaya sana.
 
Chujio

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
804
225
umenikumbusha miaka mingi mno iliyopita.... kipindi tupo watoto, mdogo wangu alipewa kichapo na bi mkubwa, kwa hasira hahahahaaa...!! alichukua uzi wa kushonea nguo na kutishia kujinyonga ..watu wote tuliishia kucheeeeka!! hiyo ilikuwa tukio la kwanza... kwa kuwa alikuwa mkorofi sana, suala la kugombana lilikuwa kawaida na alikuwa akigombezwa sana..siku moja akadai amechoka kufokewa fokewa akafungasha mizigo yake ati anataka kuondoka, alivyoona watu hata hatujisogezi kumbembeleza akahamia plan B ya kumeza vidonge viwili vya panadol akikusudia kujiua! ....hahahahaaaaa!! aiseeee! dogo alituacha hoi!!!! mwaya...kemea hiyo roho ya kutaka kujidhuru na roho mauti inayo kunyemelea, mwombe Roho Mt. akupe maarifa
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,645
2,000
Sijawahi kufikiria kujiua na ni kwasababu i have strong belief and suicide is against my belief....I have been through a lot of misery in my life but i believe i am gifted this life for some reasons so i wouldn't give it up in return for anything...ONLY THE ONE WHO GAVE ME THIS LIFE CAN TAKE IT!!...
Even when i am so down,i want something so bad I´LL DO MY BEST,try every safe option available for me so that i wont have regrets later that i could do something better or try harder...And its incredible who much i might be to willing sacrifice just to achieve my goals...That ideology keeps me strong!And i always pray and thank my god for everything even if its pain or misery....Cause GOD knows whats best for me!!!
\
nimependa comment yako. sometimes huwa najiuliza is there anything worse than death? najipaga moyonkwamba hakuna and as long as i still alive , i have a chance. may be tommorow.........
 
gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,851
2,000
\
nimependa comment yako. sometimes huwa najiuliza is there anything worse than death? najipaga moyonkwamba hakuna and as long as i still alive , i have a chance. may be tommorow.........
Believe me i know PAIN...and i won't let that take me down cause i know my life is worth something!!What i have been through make me the person i am today!!It defines me in every single way!!
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,645
2,000
una hitaji msaada mkubwa wa kisaikolojia. Hapo kwenye red unaonesha una hali mbaya sana.
niliona kweli nahitaji msaada wa kisaikolojia, nikaanza kusoma sana vitabu vya psychology. vimenisaidia sana. mfano wanasema watu wenye suicidal ideation huwa wakiangalia historia ya hukazia fikra vitu hasi tu hivyo huona hata future yoa itakuwa hasi na chungu. kuanzia hapo nikawa najitahidi kukazia fikra the positive side of my past.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,645
2,000
umenikumbusha miaka mingi mno iliyopita.... kipindi tupo watoto, mdogo wangu alipewa kichapo na bi mkubwa, kwa hasira hahahahaaa...!! alichukua uzi wa kushonea nguo na kutishia kujinyonga ..watu wote tuliishia kucheeeeka!! hiyo ilikuwa tukio la kwanza... kwa kuwa alikuwa mkorofi sana, suala la kugombana lilikuwa kawaida na alikuwa akigombezwa sana..siku moja akadai amechoka kufokewa fokewa akafungasha mizigo yake ati anataka kuondoka, alivyoona watu hata hatujisogezi kumbembeleza akahamia plan B ya kumeza vidonge viwili vya panadol akikusudia kujiua! ....hahahahaaaaa!! aiseeee! dogo alituacha hoi!!!! mwaya...kemea hiyo roho ya kutaka kujidhuru na roho mauti inayo kunyemelea, mwombe Roho Mt. akupe maarifa
hehehe! mdogo wako alikuwa ni attention seeker.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,645
2,000
Believe me i know PAIN...and i won't let that take me down cause i know my life is worth something!!What i have been through make me the person i am today!!It defines me in every single way!!
unajua watu wengi huwa tunafikiria pains and suffering are not for us!!. huwa tunakuwa very optimistic, sijui ni kwa nini. tunakuja kujua kwamba kumbe hili hata mimi linaweza kunipata ikiwa kuchelewa tayari. wengi tunajua life is not fair but we don't accept the fact!
 
Luv

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
1,791
2,000
Aisee me nshawahi kufikiria na kutenda mara mbili lakini ilishindikana.

Mara ya kwanza nilitumia sumu, nikajikuta nipo hosp nilifikaje sikujua.

Mara ya pili baada ya km miaka mitatu ya ile ya kwanza nilijinyonga, siku hiyo nilihakikisha nipo pk yangu nyumba yote ilikuwa saa nane mchana. Hata mimi sikuamini kilichotokea, nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa bt Mungu hakutaka saa mbili usiku nilipata fahamu kamba niliyoitumia ikawa imezama kabisa kwenye shingo, shingo ilivimba sana pamoja na maeneo ya usoni, ile nataka kurudia mama akawa anarudi ananiita nimfungulie geti ikashindikana. Mama aligundua baada ya siku tatu kupita. Alilia sana, aliumia sana, sitamuumiza tena mama yangu, ananipenda na tuko wawili tu me na kaka yangu, sitarajii kuwaumiza tena.

Mawazo ya kujiua yaliendelea kwa muda mrefu lakini yaliyeyuka mara tu nilipopata mtoto. Siwezi kurudia tena. Now kila nachofanya nafanya huku nikiwaza hiki kitamsaidia mwanangu? Nifanye nini ili ikitokea nimekufa mwanangu awe na maisha mazuri. Nimekuwa namuomba Mungu anipe maisha marefu ili nimtunze mwanangu hadi atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea. Ana miaka mitano sasa mwanangu. Nampenda sana.

Nimekuwa nawaogopa sana wanaume. Baadhi yao wanaweza kuharibu kila ulichopanga maishani mwako. Lakini namshukuru Mungu nimeweza kusimama tena japo bado nachechemea i hope kila kitu kitakuwa sawa.
 
APMS

Senior Member
Feb 16, 2013
106
195
nmewahi ila nikifikiria ndugu zangu naishiwa poz kabsa. kikubwa tumshirikishe mungu kwenye matatzo yetu na dawa ya tatzo ni kulitatua sio kulikimbia.
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
28,139
2,000
Sijawahi kufikiria hivyo, naamini Mungu aliyenileta duniani ndiye mwenye uwezo wa kuichukua nafsi yake.. Nayafurahia maisha yangu, uwepo wangu duniani una sababu, sikuumbwa bure kwa hiyo sitaweza kuchukua nafsi yangu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom