Maisha: Ukikukatana marafiki wa "high class" usikimbilie kuomba hela, kutangaza shida zako ama kuwalaumu pindi mnakutana

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Shikamooni wakubwa zangu wa hapa JamiiForums.

Mimi mdogo wenu (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Hii issue niliwahi kuambiwaga na mama yangu nikiwa mdogo sana ya kwamba watu wengi wa hali ya juu kiuchumi huanza kuwakwepa wale wenye uwezo wa chini kwa maana hawa wenye uwezo wa chini wakikutana na hawa wenye pesa cha kwanza kukimbilia ni kuwaomba hela, kutangaza shida walizonazo pamoja na kuwalaumu mbona siku hizi hawawatembelei kama zamani.

Aliniambia ukitaka marafiki wa high class, kwepa sana kuwalaumu na kuomba omba pesa. Keep your problems in your heart. Sio umeenda kwenye msiba au harusi umekutana na mjomba wako anafanya kazi UN au ni katibu mkuu katika Wizara fulani baada tu ya salamu ushaanza kutiririka shida zako. Mtachokwa mapema.

Jamani mbona kuna mambo mengi sana yanayohusu maisha, siasa za ndani na nje ya nchi mnaweza kuzungumza pamoja na masuala ya kijamii badala ya kukimbilia kutangaza shida na kuomba omba pesa?

Kama kuna jambo linaloweza kumjengea heshima mtu wa kipato cha chini kisha akapendwa na kupata marafiki wale wa high class basi ni kujiwekea mipaka ya mazungumzo na kujua ni kipi cha kuongea na kipi si cha kuongea mbele ya watu wa namna fulani. Hiyo inajenga sana heshima and they won't feel bored around you.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Upo sahihi kabisa, ila inategemea na mtu na mtu, binafsi kama wewe ni mtu wangu rafiki ndugu nakujua umekwama sisubiri uniombe eti nitakupa channel yoyote na hizo sh 2 tatu nitakupa hata kabla hujaniomba.

Siwezi kukuacha mtu wangu unadharirika au nikukimbie.

Tujitahidi kuwa na cycle nzuri kwa akiba yetu ya baadae, maana kikweli maisha hayana formula,manual wala prospectus useme utafungua kurasa huu usome.
 
82 Reactions
Reply
Back
Top Bottom