Maisha si marahisi hivi, ukitaka uchapiwe mke/mpenzi shindwa kumuhudumia

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,351
40,225
Maisha si marahisi hivi,ukitaka uchapiwe mke/mpenzi shindwa kumuhudumia.

Kuna dada mmoja tuko naye mtaa mmoja alikuwa anajiheshimu kweli kwenye ndoa yake, pamoja nakujaliwa sifa zote zinazoweza kumshawishi mwanaume yeyote.

Kutokana na mambo ya kiuchumi kuyumba ndani ya familia, mzee mwenye mali ameshindwa kuhudumia kwa asilimia zote mahitaji ya familia. Na mbaya zaidi kuna haina fulani ya maisha alikuwa alishayatengeneza, cha kushangaza zaidi siku za karibuni huyu mdada amebadilika na kama una dau la kueleweka, anakusikiliza. Mume amekuwa hana sauti ndani, zaidi ya kushindia pombe na ugoro ili kuondoa mawazo.

Kwa hali hii, mabaharia wenzangu nawashauri tupambane kweli kweli hata kubeba zege ili warembo wetu waendelee kutupa heshima ndani.
 
Kumhudumia ndo atoke nje?
Alipokuwa anaishi Kwa wazazi wake alipata kila kitu?
Waliposhindwa kumpa kila kitu akatafuta mabwana?

Walimsomesha ili iweje?
Anafanya kazi ili iweje?
Mumewe akifa itakuaje?Ndo ataenda barabarani kuuza kabisa?
 
Katika maisha yangu siwezi na sito kuja kuweza kuji overdose katk kujituma kwangu ili tu et nisije kuishiwa na mke wangu akatoka nje ya ndoa Never

Kuna wanawake wengi sana dunia hii yeye nanii kwa kipi labd cha maana

Sina baki kama utaki Get u'r ass out of here
 
Hivi kipi ni kipimo cha kuhudumia.. Yaani unatakiwa ufanye yapi ndo uwe na uhakika kwamba ulienae hatachepuka? We umejuaje kwamba anachepuka kwa kuwa hali ya mzee imeyumba sio kwa kuwa ni tabia yake ya kila siku!

Wanaume tunajitengenezea theories vichwani tunaziamini na baadae zinatutisha wenyewe.. Wote hatuna vipata sawa so hata level ya huduma tunazotoa kwa hawa wenzetu zinatofautiana..

Hii haimaanishi kuwa wake wa Mengi(RIP), Mo au Bakhresa hawachepuki na wake wa machinga, wapiga debe, wachuuzi wa samaki na wakulima wote ni wachepukaji..

Mapenzi ni hisia na zinaweza kukupeleka kwa yeyote na muda wowote so tupunguze kugeneralize na kuwageuza bidhaa hawa watu.. Tukumbuke hawa ni mama zetu, dada zetu, mabinti zetu na wapenzi/wake zetu..

Akishindwa kuheshim ndoa yake kisa uchumi basi ni huyo na tabia yake mbaya sio wote wana akili za hivo.. Mi nazijua familia kibao ambazo baada ya wazee kukumbwa na misukosuko ya uchumi na magonjwa ma maza mjengo ndo wanasimamia show na kila kitu kinaenda fresh..

So wa hivi akiona bandiko lako linalosema mzee ukiishiwa mama anakuwa mgawa papuchi hovyo atasikitika sana na kukudharau
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom