Masoud Kipanya, Mmoja wa waanzilishi wa Maisha Plus
Wakuu, lile shindano la Maisha Plus ndio linaelekea ukingoni.
Nani unabashiri ataibuka kidedea?
Washiriki hawa ambao wapo katika kijiji kilichotengenezwa na kina Masoud maeneo ya Geza Ulole, Kigamboni wanazidi kuonekana wakali zaidi huku Wengi wakielekea kuwakubali wakali watatu na wa nne akiwa anawanyemelea kwa karibu kabisa. Wakali wanaoangaliwa kwa karibu ni:
Wengine kama Maulid na Steve si wa kubeza!
- Abdul (Kutoka Zanzibar)
- Charles (Kutoka Arusha)
- Upendo (Kutoka Mwanza)
- Teddy (Kutoka Dar)
Mie wakati wa usahili kuna wakati sikufurahia namna bwana masoud,Bonda na yule dada..walivyo kuwa wanauliza maswali...mengine yalikuwa si ya kujenga,mengine ni ya kiudalilishaji..na wakati kwa kuwa wao walikuwa wamechoka walikuwa wanafanya kama hawataki.Hii ni ubunifu wa masoud lakini haikuwa fair kuwafanyi vijana wale ambao walionekana wengine hawana kazi wanategemea bahati nasibu ya pale.Na kupata audiance.
WanaJf,
Maisha Plus ni mbadala wa Big brothers kwetu wtz. Namshukuru Bw. Masood Kipanya kwa ubunifu wake wa kuleta show inayoonyesha maisha halisi ya mtz na kutuondolea aibu zilizokuwa zinafanywa ndani ya big brothers ambazo ni kinyume na maadili ya jamii ya ki-tz.
WanaJf,
Maisha Plus ni mbadala wa Big brothers kwetu wtz. Namshukuru Bw. Masood Kipanya kwa ubunifu wake wa kuleta show inayoonyesha maisha halisi ya mtz na kutuondolea aibu zilizokuwa zinafanywa ndani ya big brothers ambazo ni kinyume na maadili ya jamii ya ki-tz.
Mnasema hamjui madhumuni ya show ya Maisha Plus. Nilivyoona mimi ni kwamba, vijana wa ki-tz ambao wengi wao kwa sasa hawajui maisha halisi ya kijijini sasa wamewekwa kijijini ili kufahamu ni namna gani baba zao, mama zao na babu zao walivyoishi kijijini bila kuwa na simu, umeme, jiko la umeme/gas la kupikia, maji ya bomba na kulala kwenye nyumba duni ambazo nyoka na wadudu wengine kuingia ndani ya nyumba ni jambo la kawaida. Kumbukukeni, siku hizi vijana wanaoenda JKT ni wachache, kule ndiko vijana wangejifunza maisha ya kujitegemea lakini kwa sasa Jkt haipo, sasa Masood kabuni utaratibu huo ni mzuri na anastahili kupongezwa kwani haya ni matunda ya ubunifu wa mtz masood. Jambo lingine ambalo nimeliona ndani ya maisha plus, ni washiriki ku-demonstrate tabia zao halisi walizonazo. Mtu mpole utamuona pale, mmbea utamuona, mtukutu utamuona, mbunifu, mwenye busara, kiongozi anajionyesha wazi wazi kuliko ule uozo tunaoushabikia ndani ya big brothers. It is high time kupenda vitu vyetu wenyewe. I like that show.
Ubunifu pekee niliouona katika zile auditions ni kuonyesha ujinga wa Watanzania hasa kizazi kipya.Ilikuwa inatia aibu.I hope hii siyo reflection ya mwelekeo wa watanzania.Maswali yalikuwa ya kipuuzi lakini yalidhihirisha umbumbumbu wa Taifa ( vijana taifa la leo na kesho) .Tutafika?
WoS
Unakumbuka swali lolote waliloulizwa hao vijana, just curios..iwapo unakumbuka naomba tuwekee. Thanks
Mie naona kile kinaweza kuwa kipindi kizuri tu kikiboreshwa,
Lakini Masudi ameonyesha upendeleo wa wazi kwa baadhi ya washiriki huku wengine akiwakandamiza LIVE! Nadhani TBC1 ikiwezekana watafute mwendeshaji mwingine ambae anaupeo kwani inaonekana Kipanya kunawashiriki wanamzidi upeo matokeo yake anawapiga vita. Angalia baadhi ya madudu aliyofanya:
1. Washiriki waliwapendekeza Charles na Stev watolewe na sms za watazamaji zikawaangukia kuwa watoke, badala ya kuwatoa kama ilivyofanya kwa wengine huko nyuma akawapeleka kula maisha hotel na kuwarudisha ili watazamaji wapige tena kura kuatoa watu wengine, kweli akafanikiwa kawabakisha watu waliokwisha kutolewa!
2. Abdul ametuhumiwa na washiriki wa kike kuwa ni mshirikina kwani baadhi yao walimuona akiwasha moto kimazingara.....Masoud amemyamazia wala hajamuuliza! kinyume chake anawauliza waomtuhumu!
3. Abdul alikutwa choo cha kike, then baadae ikakutwa hirizi, Masoud wala hajajisumbua kumuuliza abdul alikuwa anafanya nini choo cha kike alfajiri? alikuwa akioga!? angeulizwa.
Badala yake Masoud eti anawauliza watoto wa kike tu,... na baadae wanaume bila kumgusa Abdul.
4. Abdul alitaka kumpiga Upendo kwa kumtuhumu ushirikina, ilitakiwa atolewe kabisa kwenye kijiji kwani kudhuru mwili ni kosa la jinai, vipi ingetokea kweli akampiga na kumletea madhara? Abdul alionyesha kukosa uvumilivu hapa kabisa, basi angeonywa ili washiriki wajue kupiga mtu ni kosa, wala hakuna mtu mwenye haki ya kumpiga mwenzie.
Mwisho kabisa, wale vijana ni wadogo zetu, watoto wetu, wenzetu, n.k. Tuwe wazi tu kuchagua kijana aneonekana kweli anafaa kuwa mshindi, sio kuchagua mchekeshaji, mrembo n.k. Wale woote ni watanzania, tusiwabague kwa lolote lile.
Napata tabu sana mtu anapozungumzia maadili ya ki-tz. Unamaanisha nini hasa? Maaadili yetu ni yapi? Kuvaa vibwaya na magome ya miti, kutembea uchi kama wabarbaigi? Please naomba ufafanuzi....