Maisha ni kujifunza,tafakari yangu ya miaka 25

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Maisha ni fumbo la akili na imani,kuna wakati maisha ndio hutufundisha nani wa kwenda naye na nani wa kumwacha nyuma.

Miaka 25 hapa duniani ina mengi niliyojifunza na naamini pia kila mtu anajifunza na ananendelea kujifunza haya ni miongoni mwa machache niliyojifunza.

-Nafasi za kufanikiwa hazijitokezi hivi hivi, inabidi uzitengeneze

-Njia pekee ya kufanya kazi nzuri ni kupenda kazi yako. Kama hujapata kazi unayoipenda, endelea kuitafuta. Usiridhike.

-Mtu asiyewahi kukosea baai hiyo hajawahi kujaribu kitu kipya.

-Kama kila kitu kingekuwa kimekamilika, tusinge jifunza chochote.

-Ndoto ni kitu kizuri. Ila, ni ndoto tu. Ndoto hazitafanikiwa kuwa kweli kwa kuwa umeziota. Kuchapa kazi ndio inafanya ufanikiwe. Kuchapa kazi ndio kinachosabibisha mabadiliko.

-Labda hautashindwa kama mimi nilivyoshindwa, ila, mara nyingine kushindwa hakuepukiki. Haiwezekani kuishi bila kushindwa kufanya kitu mara moja, labda uwe unaishi kwa tahadhari kwa kiasi kikubwa kusema kwamba bora usingeishi kabisa sasa na hapo, tayari utakuwa umeshindwa..

-Simjui mtu yoyote aliyewahi kufika ngazi za juu bila kuchapa kazi. Hiyo ndiyo kichocheo. Na labda hili halitatufikisha juu kabisa, ila angalau tunakuwa tutakaribia

-Kufanikiwa kwa kishindo, inabidi ujaribu kufanya vitu vikubwa.

-Bora uwe na marafiki waliokuzidi. Chagua marafiki wenye tabia nzuri kuliko ya kwako na utaishia kuwafuata.

-Tunaweza tukashindwa mara nyingi, ila tusikubali kushindwa kabisa kabisa.


JE! NI NINI UMEJIFUNZA KATIKA MUDA WAKO WOTE ULIOISHI HAPA DUNIANI?
images(4).jpeg
 
Ushauri ni mzuri... sema kikubwa hapo cha kuongezea ni maisha hayana formula...
 
Back
Top Bottom