Maisha ni fumbo kubwa, unawezaje kuishi mitihani?

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Mwenyezi MUNGU tunusuru waja wako,

Tunahitaji huruma yako na ututie nguvu ili tuwe na mwisho mwema. Iko hivii, Jana ilikuwa ni siku ya furaha kiasi, nimemaliza kazi zangu ndogo ndogo ofisini kwangu. Nikaona ni muda sahihi wa kuondoka zangu hasa ukizingatia ni weekend kwahiyo masaa manne kwa Jana yalitosha kabisa.

Basi, wakati najiandaa kutoka Kuna Mmama aliingia, ni mgeni machoni pangu,ni mrefu wastani anaonekana ni mtu anayeutunza mwili wake huku akivisaliti vipodozi vyote. Tukasalimiana,huku nikimkaribisha kiti akae,wakati nikimtazama kwa umakini mama wa makamo (wengine humu ni bibi yenu kabisa)

Akaniuliza habari fulani zinazohusiana na kampuni yetu, Huku akiwa hakwepeshi macho. Yanayonihusu nilimjibu,makubwa nikamuelekeza sehemu husika,kwamba Kama yupo serious basi aje jumatatu.akajibu sawa.

Cha ajabu, Akatoa, bahasha fulani kwenye mkoba wake ,na kunikabidhi. Niligwaya kidogo maana ni kitu ambacho sikukitarajia,akasisitiza nipokee huku akitabasamu. Safari hii nikagundua yule mama ni mzuri,Tena mzuri sana.sijui usichana wake alikuwaje ni mweusi, lakini weusi flani mtamu.

Wakati hayo yakiendelea,mlango uligongwa tena, Safari hii akaingia secretary wetu,lakini nilishangaa yule secretary alivyoangaliana na yule mama,wote walitabasamu mno,bila kuongea chochote, Nikavunja ukimya,baada ya kumkaribisha naye akae,lakini akanijibu nilikuja kukuaga tu

Mimi sinaga subira ,yule dada alivyoondoka nikatamani kuona Nini kipo kwenye bahasha nilopokea, Kuangalia nikakuta pesa taslimu TSH laki mbili yaani zile noti za elfu mbili mbili ,kale kamkanda hakajachanwa lakini pia karatasi yenye namba za simu pamoja na kadi ya mualiko,

Kabla sijamuuliza chochote yule mama,nilijiuliza haya,

Huyu mama ni nani?

Anataka nini?

Pesa za nini

Kadi ya mwaliko je,naalikwa wapi?

Tumezoea tukipewa kadi sisi ndiyo watoaji wa pesa,

Inaendeleaa.....
 
Inaendeleaa.....

Nikainua uso kumtizama,alionekana kachukia,pengine ni zile papara zangu za kufungua vile vitu.

Pasi na kuchelewa nikamuuliza hivi vitu ni vya nini,nikimkazia USO kwa umakini, akajibu kwa sauti ya upole,

Baba Roziii (siyo jina halisi) weka basi hizo pesa mfukoni,unataka yeyote akiingia hapa akute hela zipo mezani.

Kwanza niliguna,moyo ukaanza kudunda kwa mbali,ndiyo kanijuaje naitwa baba fulani,ujue kama mtu Ana lengo la kukudhuru.

Halafu akawa anakufahamu kiundani una kuwa katika hatari zaidi,mbaya zaidi yeye simjui,

Baada ya hapo nikaongeza umakini,
Sikutaka kuuliza maswali ya kibwege Tena

Swali likawa moja,

UNATAKA NINI KWANGU?
 
Huu ni mkasa wa kweli umenipata Jana tu,nimeamua kushare na ndugu zangu hapa ili Kila mmoja wetu,

Ajifunze na kuchukua tahadhari hapa mjini.
 
Inaendeleaa....

UNATAKA NINI KWANGU?

Ni swali ambalo pengine hakulitarajia ,akanyoosha kidole kunionyesha ile karatasi yenye namba za simu.

Huku akiinuka kutaka kuondoka,wapi wewe,nikamuuliza,

Unaniachaje njia panda kuniletea vitu vyako bila maelezo ya kutosha mbaya zaidi sikufahamu.unadhani nitakufikiriaje,nilihoji kibabe.

Kinyooonge akakaa Tena, akatoa kitambaa fulani kidogo akipangusa jasho lake,huku nikimuona kabisa ana hofu , ndiyo.alikuwa na hofu mi mwenyewe sinaga masihara kabisa,

Dunia imeharibika hii,mtu anakuwekaje roho juu,

Cha ajabu yeye akasisitiza,aondoke ili nimtafute kwenye simu namba si kaniachia,ndugu msomaji,

Jana nilijivika ukamanda,nikamwambia simama,nyoosha mikono juu,

Ndiyo,ungekuwa wewe ungefanyaje ,kama ana kisu, pistol,venom spray ?

Hujadhurika mtu wangu,

Kwanza hakuamini,akawa anatetemeka nakuniambia kwa sauti ya upole,

Nitakuelekeza Kila kitu,sikutarajia Kama upo hivi Mimi si mtu mbaya.

Nikamsachi kuanzia utosini hadi unyayo,kama atanishitaki kwanini nimegusa mwili wake,afanye hivyo

Nilikuwa natafuta kitu chenye ncha kali,kwa usalama wangu nisije dhurika,

Baada ya kumaliza zoezi hilo, nikatoka nje kuangalia mazingira ,sikuona chochote zaidi ya kuwaona walinzi wakimgombeza dada mmoja aliyekuwa na beseni lenye matunda,

Inaendeleaa....
 
Then Ikawajeee
Inaendeleaa....

UNATAKA NINI KWANGU?

Ni swali ambalo pengine hakulitarajia ,akanyoosha kidole kunionyesha ile karatasi yenye namba za simu.

Huku akiinuka kutaka kuondoka,wapi wewe,nikamuuliza,

Unaniachaje njia panda kuniletea vitu vyako bila maelezo ya kutosha mbaya zaidi sikufahamu.unadhani nitakufikiriaje,nilihoji kibabe.

Kinyooonge akakaa Tena, akatoa kitambaa fulani kidogo akipangusa jasho lake,huku nikimuona kabisa ana hofu , ndiyo.alikuwa na hofu mi mwenyewe sinaga masihara kabisa,

Dunia imeharibika hii,mtu anakuwekaje roho juu,

Cha ajabu yeye akasisitiza,aondoke ili nimtafute kwenye simu namba si kaniachia,ndugu msomaji,

Jana nilijivika ukamanda,nikamwambia simama,nyoosha mikono juu,

Ndiyo,ungekuwa wewe ungefanyaje ,kama ana kisu, pistol,venom spray ?

Hujadhurika mtu wangu,

Kwanza hakuamini,akawa anatetemeka nakuniambia kwa sauti ya upole,

Nitakuelekeza Kila kitu,sikutarajia Kama upo hivi Mimi si mtu mbaya.

Nikamsachi kuanzia utosini hadi unyayo,kama atanishitaki kwanini nimegusa mwili wake,afanye hivyo

Nilikuwa natafuta kitu chenye ncha kali,kwa usalama wangu nisije dhurika,

Baada ya kumaliza zoezi hilo, nikatoka nje kuangalia mazingira ,sikuona chochote zaidi ya kuwaona walinzi wakimgombeza dada mmoja aliyekuwa na beseni lenye matunda,

Inaendeleaa....
 
Inaendeleaa....

Wakati narudi ndani,wale walinzi walinita, niliwajibu kwa kutingisha kichwa kukubalina nao nikaona huku ndani ni muhimu zaidi.

Nikamkuta yule mama kajiinamia huku akitoa miguno flani ya kilio Cha kwikwi,sikujali

Najua wanawake ndivyo walivyo anaweza kuchokoza jambo,ukimbana anakimbilia kulia.

Nikarudi nje nikawasikilize walinzi

Si huyu,mlikuwa mnakataa nini,lengo lenu nisiuze au,Mimi na nyinyi tunatofauti gani !? Mimi naungua jua ndiyo ,mbona na nyinyi mnang'atwa na mbu usiku,

Tukijiuza mnatudharau,tukifanya kazi napo nongwa, maneno haya yakawa Yanamtoka dada muuza matunda .mtu anayeongea huku akitoa lugha ya matusi yaani haongei maneno matatu bila kuweka tusi la mama mzazi, ni hatari

Lakini nilipokaribia zaidi aligundua siyo Mimi anayemuuziaga matunda, akawa kanyongea ,walinzi wakapata point maana alilazimisha kuingia ndani ya geti wakati Hana uhakika huyo anayemuuziaga yupo au la.

Bosi huyu alisema anakufuata wewe unanunuaga matunda toka kwake .

Alisisitiza mmojawapo huku akionekana mwenye hasira,akimtoa kwa nguvu yule dada ambaye anaonekana ni mtu wa Pwani kuanzia haiba yake mpaka maneno mdomoni

Lakini nikawazuia....

Haya mmeniitia nini,niliwauliza

Ah bosi samahani,Kuna gari lipo nje hapo kwahiyo tulikuwa tunaomba liingie ndani kwa usalama zaidi.

Ni la nani? Niliuliza.

Wakajibu ni la mama mmoja hivi,kaingia humo ndani alisema anamtaka dada (jina kapuni) ni yule secretary.nikawaambia liacheni
Mwenyewe anatoka siyo muda

Nikaelewa kitu,kumbe secretary anajua ujio wa huyu mama,Sasa mbona wananichezea akili, nikatoa simu yangu mfukoni nimpigie lakini namba zake zote hazikuwa hewani

Mmmmh balaa hili,njaa inaniuma pia maana muda niliopanga kutoka umepitiliza kutokana na ujio wa mgeni ambaye hadi muda huo sikujua anataka nini kwangu.

Sasa bosi huniungishi matunda,aliuliza yule dada,nikacheka kicheko flani huku nikijiwazia , nyumbani kwangu Kuna shemeji yangu wa kike ambaye baada ya masomo kumshinda aliniomba mtaji wa kuuza hayo matunda ambapo kwa Sasa anafuata mzigo na pikipiki ya matairi matatu

Anauzia pale pale mtaani kwangu , kwahiyo Mimi na familia yangu matunda ni Kama tumepanda.

Nikatoa elfu moja awape wanachotaka wale walinzi .si lengo nimuungishe?

Wakati nageuka nirudi ofisini nikamuona yula mama anatoka .

Inaendeleaa.....

Jamani jina"BOSI"

Halina maana upo vizuri kimaisha ni jina tu tunaitana,
 
Hii chai ukimaliza nitakuja.
Nadhani mpaka Ijumaa itakuwa imeisha.
Mambo ya "Itaendelea" ya nini?

Any way to yeye akimaliza mapema ni tag.

#YNWA
 
True story.

Inaendeleaa..

Baada ya yeye kugundua narudi ndani,akasimama kunisubiri,nikamkaribisha ndani nikiwa na hofu kiasi ila yeye safari hii akawa kachangamka sana,

Mwenzangu mbona umeniacha muda mrefu sana nikajua unawapigia polisi ,nikamjibu muda wa kuwaita polisi utafika ikiwa utashindwa kuniambia Nini unakitaka toka kwangu huku nikitabasamu ili nisimkazie sana

,nikamuuliza lile gari ni lako pale nje akajibu ni lake,

Eenhee haya nambie,nilihoji kirafiki maana nilimuona ana kauwoga flani,

Akasisitiza, nichukue zile namba nizisevu,pia nipokee zile hela nikamkatalia, nikamwambia tu kuhusu namba nachukua
Kwakuwa Nina shauku ya kutaka unalotaka kuniambia.

Basi akaweka hela katika mkoba wake tukatoka kwakuwa muda ulienda ikabidi tuachane licha ya yeye kusisitiza nipande kwenye gari lake nilikataa wakati yeye akiingia kwenye gari lake,

Nanukuu alivyosema,

Ila utanisamehe Mr.

Akawasha gari na kusepa,nikaduwaa nimsamehe Tena,nimsamehe kwa lipi ?anyway labda kwa usumbufu alionipa muda mrefu.

Nikatoka nikaita usafiri wangu nikaomba nipelekwe baa moja maarufu hapa mjini maana Kuna vyakula vizuri na pia Kuna TV's nzuri sana maana sijazoea kuangalia mpira nikiwa nyumbani hasa dabi ya Yanga na Simba

Basi dakika 5 nyingi nikawa nishafika pale mahali huku nikisikia makelele watu wanashangilia,kuangalia saa mbona saa kumi bado ,

Ratiba ya mpira si tuliambiwa saa kumi? Kuna jamaa fulani anayeonekana mjuaji anaongea kuliko wote akanijibu,

Unajua kaka hii mechi ni ngumu ni lazima watu watoke sare,Mimi Simba na Yanga nawajua,nawajua sana, yaani Yanga ana historia ya kutofungwa kirahisi pale kirumba Mwanza ,halafu Simba Hana uhakika wa kuchukua ligi kuu,

Kwahiyo kombe pekee lenye kumpa heshima msimu huu ni hili la ASFC nakwambia hi mechi sare lazima wafike matuta,na ndiyo maana wameanza mapemaaaaaa

Huku akinikazia macho kuonesha ana uhakika na anacho kizungumza

Waswahili bwana

Ghafla simu yangu ikaita,namba ni ya mke wangu,nikaipokea

Bila hata salamu akawa anaongea kwakuhema ,shemeji yako haonekani tangu jana (yaani mdogo wake tunayekaa naye pale nyumbani)

Mbaya zaidi simu yake haipatikani

Kifupi nikamjibu nakuja mke wangu.

Inaendeleaa...
 
Niliondoka pale baa,nikaita usafiri haooo mpaka home,

Nikakuta majirani kadhaa wakiwa wanamfariji wife maana mambo hayakuwa mazuri wakati huo

Sikutaka mazungumzo mengi nikafanya utaratibu wa kuripoti kituo kidogo kilicho karibu na pale home,

Taratibu zikafuatwa Kila kitu kikawa shwari japokuwa ni mtihani sana kwanini majanga juu ya majanga,

Nikajiuliza maisha ya mtu huharibika hivi hivi ,mtu kapotea ,wazazi wake wanajua yupo na Mimi,namtafutia wapi Sasa ,huu si msala huu?

Ndiyo,

Lazima niwajibike,kwahiyo shughuli zangu zote zinaenda kusimama na hizi kazi za kubembeleza awamu hii

Maana waajiri wanasubiri ukosee tu, au uombe ruhusa ya muda mrefu ili wapate sababu ya kukuachisha kazi,

Anyway Kila kitu kitakaa poa.nikiwa narudi ili nilete mrejesho kwa wife nikakuta pale nyumbani watu wameongezeka wakiwemo wanaume wenzangu nikapata faraja kidogo kuwa Sasa mambo yatakuwa mazuri tutashauriana Nini Cha kufanya.

Weweeeeeeee kumbe niliwaza tofauti,nikasikia tu sauti za chini chini Mara ooh mtu unawezaje kutembea na shemeji yako,yaani Dunia Kuna mabazazi sijapata kuona,

Yaani mtu kaenda kumfungia shemeji yake lodge sijui wapi halafu mnasingizia kapotea,huyu aoneshe shemeji yake yuko wapi, hakuna mjadala ,akiongeza mama mmoja hivi kuwa Mimi ndiye niliye mficha shemu wangu,

Hiyo ni saa ngapi mjue!

Saa moja usiku,moyo ukanidunda nikajihurumia nikamwangalia mke wangu nikamuona yupo nusu kwa nusu,awaamini wageni ama aniamini Mimi ,na nikifanya mchezo atawaamini wao jumla.

Nikaingia ndani pitiliza Hadi chumbani,ujue wanaume tumeumbiwa mateso kwahiyo ni kupambana na Kila majaribu na siyo kukaa chini kulialia haikusaidii

Wakati huo wife anakuja chumbani analia huku akisema ,mume wangu kwanini umenifanyia hivii,we wa kutembea na mdogo wangu kweli,

Aisee nilikasirika mno,nikamwambia nyamaza Tena NYAMAZA hebu punguza ujinga basi maana hauwezi kukutoka wote....

arrrghh ni Nini hiki? Nikatoka nje nakutana na kundi la watu mmojawapo akanihoji,

Jana ijumaa ulirudi saangapi?

Nikamjibu,nilirudi mida ya saa nne usiku,

Akauliza,kwanini Leo uende kazini na mkeo anasema jumamosi kwako ni weekend huwa unatoka labda kukagua miradi yako binafsi,

Dada mmoja akarukia,did ndiyo alienda kumpelekea moto shemeji yake?

Na karudi baada ya kupigiwa simu vinginevyo wangekaa wiki nzima,

Watu vicheko hawana mbavu.

NILIUMIA SANA lakini maneno Yale nahisi mke wangu aliumia zaidi

Kengele zikalia nikahisi mbona Kuna kitu naanza kuelewa,yule mama aliyekuja ofisini kwangu ana maana gani, secretary wetu mbona Kama anaijua ishu hii,?mbona hii ishu naiona ndogo tu,nikarudi kituo Cha polisi.

Inaendeleaa...
 
Back
Top Bottom