Maisha + Mahusiano yanavyoweza kujenga au kubomoa maisha ya mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha + Mahusiano yanavyoweza kujenga au kubomoa maisha ya mtu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by M'Jr, Sep 17, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Jana nimesikiliza simulizi ya dada mmoja kwenye kipindi cha njia panda cha Clouds Fm. Sababu hasa iliyonifanya nikisikilize ni yale matangazo yaliyokuwa yakikitangaza kipindi hicho kuhusu mwanamke kufanya mapenzi na mbwa (Nakumbuka nikiwa mdogo hivi bado niko shule ya msingi kuliwahi kutokea tukio la namna hiyo maeneo ya mikocheni na nakumbuka nilikuwa namjua huyo mbwa mwenyewe kwasababu kama ilivyo desturi ya watoto hupenda sana kuchokoza mbwa hasa wale walioko magetini kwasababu wanajua hawawezi kutoka. So nilipolisikia lile tangazo nikapata hamu ya kusikiliza simulizi yenyewe kamili.

  Sasa niliposikiliza kidogo ikanifanya niwe na mixed feelings (sympathy, sadness, anger) lakini pia ikanifanya niwe na maswali kadhaa ambayo nikaona ni busara kama tutayazungumza kwa pamoja;
  1. Je wanawake wana nguvu gani katika kuamua matumizi ya kinga (condoms) kwenye tendo?
  2. Je ni kwa kiasi gani mtu anaweza kuwa pressed na maisha kiasi cha kuingia kwenye maisha kama aliyoingia yule dada (Umalaya) au mengine yoyote yasiokubalika na jamii?
  3. Je mahusiano yana nafasi gani katika kumfanya mwenza asiingie kwenye maisha ya namna hiyo (kwasababu katika kusikiliza simulizi nzima hakuna sehemu aliyosema alikuwa hata na mpenzi) na mi nilikuwa najiuliza sana kama alikuwa na mpenzi je role yake ilikuwa nini kwenye kuhakikisha mpenzi wake haingii kwenye maisha aliyokuja kuyaingia? Maana kimsingi sababu kubwa iliyomfanya yule mdada aingie kwenye maisha hayo ni kutokuwa na mahali pa kuishi lakini kubwa kabisa ni kukosa ushauri na encouragement.

  Hebu tujadili kidogo hili ili baadhi ya watu wajue nini cha kufanya kwenye situations kama hizi.........
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  maisha na tabia ya mwanadamu inategema vitu vingi sana.lakini hakuna kitu kinaathiri maisha ya mtu kama upendo!ndo mana tunaambiwa tuwaonyeshe watoto wetu kuwa tunwapenda toka wakiwa wadogo sana,maana inawajenga kujiamini na uwezo wa kujipenda na kupenda wenzao!
  angalia mtu liyekosa upendo utotoni mara nyingi huangukia kwenye hatari ya kutokupata mapenzi iwe ni kwa kupenda/kupendwa
  unapoexperience upendo utagain tu kujiamini na kujithamini utu wako,ni rahisi pia kuyaface matatizo hata yanapokukuta kwenye hali ngumu kiasi gani.
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mh, okay.....undertood
   
Loading...