Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,194
- 12,689
Ukiangalia kwa unfdani utaona kuwa dini nyingi ni matokeo ya maisha magumu. Kisaikolojia mtu akiwa frustrated na ugumu wa maisha huanza kuota ndoto za mchana na kufantasize maisha yasiyo na taabu. mifano mingi inaonyesha hivyo.
1. Kuanzishwa kwa dini ya kiyahudi: Kuna mtaalamu anasema kuwa Wayahudi waliishi maisha mazuri sana wakati wa mfalme Daudi. Anadai kuwa baadaye mambo yalivyokuwa magumu, wakitekwa na kufanywa watumwa huku na kule na wababiloni na waajemi wakaanza kukumbuka enzi za Daudi. Mwishowe wakaanza kuota kuwa kuna mzao wa daudi atakuja na kurudisha neema ya wakati wa Daudi. Ndiyo huyo wakamwita Messiah. Chanzo ni ugumu wa maisha na kukumbuka enzi za Daudi.
2. Musa mwenyewe utaona kuwa alianzisha dini baada ya kuona mateso wanayopitia Waebrania kule Misri.
3. Mababu zetu walianzisha dini ili kuiomba mizimu wakati wa njaa, magonjwa na vita.
4. Kuna wakati wahindi wekundu walikuwa wanasakamwa sana na wazungu huko Marekani. wWalikuwa wamenyang;anywa ardhi yote nzuri. Wamewekwa kwenye maeneo makame na hawatakiwi kutoka huko. Na wakipigwa vita na kuuwawa kama wanyama. Akatokea mhindi mmoja akasema kuwa ametokewa na Yesu. Akadai kuwa Yesu huyo ni mhindi na ameahidi kuja kuwakomboa wahindi kutokana na mateso. Wanachotakiwa ni wacheze dansi bila kupumzika. Ikawa hivyo, watu wakaanza kucheza dansi mfululizo hadi pale serikali ya wazungu ilipoingilia kati kikatili.
5. Nilikuwa namsoma Malcom X. Dini yao ya Nation Of Islam ilianzishwa kutokana na maisha magumu waliyokuwa wanapitia watu weusi wa Marekani. Dini hiyo inasema kuwa Mtu mweupe ndiye shetani. Kwamba alizalishwa miaka elfu sita iliyopita. Na kuwa baada ya miaka elfu sita watu weusi ambao ndiyo watu asilia watarudia utukufu wao. Ni ugumu wa maisha uliozaa dini hii.
6. Budhha mwenyewe alianzisha dini yake baada ya kuoana mateso wanayopitia watu.
7. Dini nyingi zinazoanzishwa leo na wakina Gwajima, Mwamposa, Mzee wa Upako nk, zinaanzishwa sababu ya maisha magumu. Sehemu kubwa zinahubiri utajiri, uponyaji, na mafanikio kwa ujumla. Ugumu wa maisha ndizo zimefanya uwepo. Watu wakienda huko wanapata ndoto zao za mchana na kuepuka matatizo yao kwa muda.
Sababu nyingine kubwa ya kuanzisha dini ni ya kisiasa. Dini kama Ukatoliki na Uislamu n i kwa ajili ya watu kujipatia nguvu za kisiasa. Hata mifarakano kwenye dini hizi. Mfano kutokea kwa kanisa la Orthodox, Anglicana nk, ni sababu za kisiasa. Kutokea kwa Usunni na Ushia ni sababu za kisiasa.
Dini nyingi ni uzushi.