Maisha kuanza kubana baada ya Pasaka, wajumbe wa nyumba 10 ndo wakati wao wa kujitambua

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,396
Wajumbe wa nyumba 10 ndo wawakilishi wa kwanza wa serikali katika maeneo yetu.

wajbe wa nyumba kumi wanatambua watu wao na kazi yao ya kutambua watu wao ni rahisi kuliko askari alieko katika kituo cha polisi.

Wakati serikali imeanza kuchomoa makucha yake kidogokidogo kuelekeza kwa watu wanaokaidi amri ya kutokusanyika, polisi nao wamejiandaa kufanya doria katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivyo basi kitendo cha kuachia watoto wetu waanze kuzagaa mitaani bila uangalizi si jambo la afya.

Kama baba na mama mpo ndani ya lockdown basi kila mtu akae ndani na si mmoja wenu au wote mtoke kwenda kwenye mihangaiko.

Tkifanya hivyo,basi huku nyuma watoto nao wanatoka na wanaingia mitaani kukutana na watoto wenzao kucheza, kisha wanaelekea sehemu zingine mbali na nyumbani kwao kutafuta marafiki wenzao na mwisho wanapotelea sehemu zingine.

Sababu kubwa ni kwamba watoto wetu hawajapewa elimu na wazazi wao kwamba ni kwanjni tunakaa ndani,

Mtoto ukimwelimisha anaelewa na akikuona mzazi nawe upo ndani ndo anakuwa mwelewa mzuri na anatambua kuwa wazazi wanawajali watoto na wapo nao katika kipindi hiki kigumu.

Ugonjwa wa COVID -19 umeanza kuleta madhara katika sehemu mbalimbali nchini kutokana na wananchi kuanza kutekeleza hali ya lockdown.

Mahoteli yanafungwa, kweye mashule kuna baadhi yao walimu huenda wasilipwe mishahara kutokana na ukosefu wa fedha ambazo hutegemea ada za shule na sekta ya usafiri pia ambayo hutegemea wasafiri hali imeanza kubadilika.

Lakini tukirudi katika jamii zinazotuzunguka, wajumbe wanyumba 10 ndo sasa wakti wao wa kujidai na kunaza kujitambua na kujitambulisha.

Ni wakti wa kufahamu idadi ya watu wao kisha kutengeneza daftari la wananchi wao na mwisho kujikuta kwamba serikali za mitaa zina orodha kamili ya wanancu wa kata zao na hatimae kuwa na idadi kamili ya wananchi wa wilaya hadi mkoa mzima.

NI wakati wa kuelimisha jamii wanazoziongoza kuhusu umuhimu wa kufanya usafi kwenye maizngira yao na kuhimiza kuosha mikono.

Pia huu ni wakti wa kuimarisha doria miongozi mwetu maana wizi na vitendo mbalimbali vya kihalifu vitashamiri kwa wingi khasa kwenye maeneo ambayo yana watu wengi.

Kuna umuhimu wa wananchi kurudisha ulinzi wa sungusungu kwa kushirikiana na polisi ili kukabiliana na hali hiyo.

Nawatakia kheri ya Pasaka.

Tukumbuke kunawa mikono
Tuepuke misongamano isoyo lazima
Tuweke nafasi ya mita moja tunaposalimiana au kuongea.
 
Back
Top Bottom