Maisha hapo awali katika Mars

Kuna wakati unajiuliza kifaa kiko mwezini,( picha ya kifaa mwezini ) sijui mars huko alafu unaletewa picha yake sasa kilijipiga picha chenyewe ama kunakiwa na kifaa kingine cha pili kikikipiga picha kifaa cha kwanza?

Anyway, inasemekana pia huyu Mungu tunayemuabudu ni wa tatu, kwenue Rank zao, yaani sisi wengi tunamuabudu Mtoto wa Mungu mwenyewe ambae huyo Mungu Mkuu yeye hana time na sisi ila hao watoto wake ndio wameleta maseke yote haya tunayokutana nayo..alafu ki Ukweli hizi dini zinatuchocholesha sana, Tunaabudu Miungu ambayo yenyewe pia iko kwenye adhabu kutoka kwa Mungu Mkuu.
 
Hapo awali kupitia ushahidi wa maandiko matakatifu tuliona kuwa Ibilisi hakuwa na makao ya kudumu katika sehemu ambapo yapo makao rasmi ya Mungu Mkuu huko mbinguni. Bali tuliona kuwa yeye na malaika waliokuwa chini yake waliishi katika mbingu nyingine. Na walikwenda katika makao ya Mungu kwa sababu maalum, yaani kwa ajili ya kazi yao rasmi ya kuendesha nyimbo za sifa za utukufu kwa wakati wa ibada kuu ya Mungu Muumbaji.

Tuliona pia kuwa Ibilisi aliishi katika mbingu nyingine na ya chini kihadhi ukilinganisha na ile ya Muumbaji. Kwa hiyo basi upande wangu nilijenga dhana ya kuwa huenda sehemu hiyo mbingu alipoishi Ibilisi na malaika waliokuwa chini yake ilikuwa ni katika sayari ya Mars.

Aidha, tulikuja kuona ukweli ya kwamba Mungu kwa asili ya ukuu wa mamlaka yake, asingaliweza kukubali makazi yake rasmi yawe sehemu ambapo ungefanyika uasi wa kiumbe ambacho alikiumba Yeye mwenyewe na kwa utashi wake.

Ushahidi wa maandiko unatupa ushahidi ya kuwa jaribio lolote lile la kutaka kuendesha vita na Mungu huwa linamalizika kabla hata vita yenyewe kuanza.

Ukweli juu ya jambo hili tunaweza kulipata kupitia unabii kuhusu hatma ya vita vya Armageddon kama vile ifuatavyo;

UFUNUO 19

19 Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake. 20 Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti. 21 Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.

Namba 3 kupitia tafsiri za kimaandiko huwakilisha jambo ambalo lipo chini ya mamlaka ya kimbingu ambalo hudumu katika muda mfupi na hatimaye kwenda kufikia ukamilifu wake wote kama vile ambavyo lilikusudiwa. Ndivyo ambavyo ilipangwa kwa uasi wa asili wa Ibilisi.

Kwanza alijaribu kuendesha vita dhidi ya Mungu wake katika ulimwengu wa kiroho, ambapo malaika watakatifu walipambana naye na kumshinda.

Pili ataendesha vita kupitia wanadamu wakiwa katika ulimwengu wa kimwili kama vile ambavyo tumeona katika rejea ya Ufunuo 19 napo atashindwa kwa mara nyingine.

Na ili akapate kudhihirisha uovu wake atapata nafasi ya tatu, mara baada ya kutoka kifungoni kwa miaka 1,000 ataendesha vita vingine ya kimwili akiwaongoza tena wanadamu. Ataongoza vita nyingine dhidi ya Mungu akiwa na jeshi la wanadamu wote waovu waliowahi kuishi duniani ambao wote watafufuliwa na kupewa muda mfupi mno wa kuishi tena na ili wote wathibitishe uovu wao kuwa wanamtii Ibilisi. Nukuu ifuatayo inaweza kutupa tafakari zaidi;

UFUNUO 20

7 Wakati miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
8 Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
9 Walipita katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watakatifu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza.
10 Naye Ibilisi aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka madini ya kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.

Sasa baada ya kuona maandiko matakatifu yanatupa fununu zipi juu ya sehemu ya mbingu ambapo Ibilisi aliishi hapo awali. Sasa hebu tugeukie maandiko yake yeye mwenyewe na tuone yanatuambia nini juu ya jambo hili. Nafikiri wengi wetu wamekwipata taarifa ya sanamu ya mnyama iliyowekwa katika ofisi za makao makuu ya UN. Ni sanamu mfano wa chui mwenye mabawa, mwenye kinywa mfano wa simba na miguu mfano wa dubu.

Kiunabii mnyama kuwa na mfano wa simba huwakilisha dola ya kale ya Babeli ya kale na mfumo wa ibada zake za sanamu za kipagani, dubu huwakilisha dola ya kale ya Umedi & Uajemi na ibada zake za kipagani za kimajini na chui huwakilisha dola ya Kiyunani na ibada zake za kipagani za kimizimu.

Tunaweza hapa kujifunza kupitia mafunuo ya imani hizi za kipagani ili kujenga msingi wa kimaandiko, kifalsafa na imani za kidini. Jambo hili linathibitika katika kipindi cha dola ya kale ya Rumi na na ushawishi wake katika elimu ya sasa iliyopo duniani. Na ni hapa ndipo tunapata ukweli mwingine kuwa huenda ni kweli Ibilisi aliishi katika sayari ya Mars kabla ya kufukuzwa huko.

Elimu ya sasa hutuambiaa sayari ya Mars ama Mirihi kwa lugha yetu nzuri ya Kiswahili ipo umbali wa kilomita zipatazo milioni 54.6 kutoka ilipo sayari yetu nzuri ya dunia ama maili milioni 34.

Kihistoria na kisayansi sayari ya Mars ina muonekano wa rangi nyekundu, na kutokana na imani za kale za kipagani rangi hii ilihusishwa na matambiko ya damu na hivyo kuonekana inamwakilisha mungu wa mabaya kwa wa Wababeli wa kale, lakini Wamedi & Waajemi pamoja na Wagiriki waliona Mirihi kama mwakilishi wa mungu wa vita yaani "Ares" na jina hili likaja kupokewa na Warumi wa kale, huku nao wakiitafsiri sayari hii kuwa ni mungu wao wa vita mwenye hamu, uchu ama kiu kubwa ya kumwagika kwa damu.

Jina la mwezi wa tatu, yaani Machi limetokana na heshima ya Warumi kwa mungu Mars. Imani zote za dini za kale zilimpa sifa ya kipekee Mirihi kama mungu mwenye ujanja, hila na kiu ya damu ambaye hupenda machafuko na hatimaye kuleta matokeo ya vita.

Tunapata elimu nyingine ya kipagani kuwa Ares alishiriki katika Vita vya Trojan iliyotokea huko mbinguni ambapo alipambana na Athena na kushindwa katika vita hii. Tunaona ya kuwa Athena alikuwa na sifa tofauti kabisa na Ares kwa kuwa alitambulika kama mungu mwaminifu, mwadilifu na mwenye busara ambaye akilazimika kupigana, yeye hupigana vita vya haki na vya kimkakati.

Kwa hiyo maandiko matakatifu na mafundisho vyote hukubaliana ya kuwa vita katika ulimwengu wa kiroho vilitokea mbili. Naye Mungu mtenda haki alimshinda mungu muovu. Lakini mafundisho ya kipagani humtaja kwa uwazi mungu huyo muovu kwa alama ya sayari ya Mars ama Mirihi.
 
Safari ya kwenda sayari ya Mirihi katika picha
IMG-20220120-WA0038.jpg
IMG-20220120-WA0036.jpg
IMG-20220120-WA0037.jpg
 
Source ya hii habari wapi kamanda?
 
Source ya hii habari wapi kamanda?
Mkuu Dumas, mbona vyanzo vya habari ni vingi tu!? Mada ya yangu itapata mashiko tu kama itakuwa "critized" kupitia watu wadadisi na wenye ufahamu mzuri. Mimi sina uelewa wa kina wa kiimani nje ya Ukristo.

Kwa hiyo hata mimi pia nategemea hilo kutoka kwa watu wenye ufahamu zaidi wa hizi imani za kipagani. Hii miungu ya kigiriki ya Ares na Athena nimeipata kupitia "Google search engine".

Kwa hiyo mtu yeyote anaweza kuonyesha mapungufu yangu ya kiuelewa ama hata kuonyesha uongo uliopo ndani yake. Kwa kuwa hii ni dhana tu na pengine inakosa kabisa uhalisia.
 
Bado tupo katika sayari ya Mars ambayo imekuwa ni kivutio kikubwa kwa sasa kuliko eneo lingine lolote lile katika anga za juu. Zipo sababu za jumla zinatolewa kuhusu hamasa hii kubwa. Katika sayari hii nyekundu ya Mirihi kunani kule?

Chombo cha uchunguzi cha ExoMars rover nacho kwa sasa kinatarajiwa kuondoka duniani mnamo tarehe 20-09-2022 na hatimaye kutarajiwa kutua katika Mars siku ya tarehe 10-06-2023. Chombo hiki kinasimamiwa na European Space Agency (ESA) kwa kushirikiana na Russian Space Agency (ROSCOSMOS) nacho pia kinatarajiwa kufanyia kazi uchunguzi wa hapo awali uliofanywa na chombo kingine cha ExoMars orbiter.

Uchaguzi wa ExoMars orbiter umebaini uwepo wa maji mengi yaliyoganda katika bonde kubwa la Valles Marineris lililopo katika sayari hii. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa toka mwaka 1960 kuna jumla ya majaribio yapatayo 49 ambayo yamekwisha kufanyika ambapo miongoni mwa hayo, mashirika ya NASA ya USA na lile la China la CNSA ndiyo yameweza kufanikisha zoezi la vyombo vyao kutua katika ardhi ya sayari hii nyekundu.

Mashirika ya anga za juu ya nchi nyingi hapa duniani hivi sasa bado yanapigana vikumbo huko angani kwenda katika sayari hii kufanya uchunguzi. Mashirika kama lile la JAXA la Japan, Space X la USA, Canadian Space Agency, Italian Space Agency pamoja ISRO la India, yote yanaendelea na uchunguzi wa kisayansi katika sayari hii.

Hii ni miradi aghali mno na yenye kuhitaji uwekezaji wa fedha nyingi sana. Kwa nini iwe ni sayari hii tu na wala si nyingine yenye kuonyesha kuwa kivutio namna hii? Tajiri mwenye ukwasi mkubwa kuliko wote duniani, Elon Musk yeye ameahidi kupeleka watu kuishi katika sayari hii na hata kuigeuza kuwa koloni la dunia (lake binafsi!?). Huko mbeleni tutakuja kujua ni nani huyu Elon Musk, nini hasa anachokijua kuhusu siri iliyopo ndani ya sayari hii?

Kama ilivyokuwa ada hatuwezi kuangalia fununu za kihistoria zilizopo katika maandiko matakatifu na pia ushahidi uliopo katika mafundisho ya Ibilisi mwenyewe. Tukianza na Neno la Mungu tunapata tafakari ifuatayo;

A. Mafumbo ya Mungu

1 Wakorintho 2

10 Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mafumbo ya Mungu.
11 Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.

B. Fumbo za Ibilisi

Ufunuo 2

24. Lakini nyinyi wengine mlioko huko Thiatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezebeli na ambao hamkujifunza fumbo za Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.

25. Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.

Tukienda katika elimu ya kipagani inavyozungumza juu ya Ibilisi tunaweza kupata jambo fulani la maana. Mathalani tukienda katika "Lucifer wiki" tunaweza kupata michango mbalimbali ya wale waliozitoa roho zao kwake.

Kupitia kwa hawa wenye kumsujudu Shetani tunaona ya kwamba kuna vitu muhimu sana ambavyo Ibilisi ataweza kuimiliki dunia yote kama yeye ndiye mungu kamili, navyo ni;
a) Pete yake maalum iliyotengezwa kwa vito vya thamani kubwa
b) Sarafu ya pentekoste (Pentecost coin)
c) Kurasa 10 zilizopotea katika biblia yake ya Codex Gigas zenye "paramount satanic pray"
d) Madini adimu yatayowezesha kufunguliwa kwa shimo la kuzimu (Rejea Ufunuo 9:1-11)

Ni kweli hapo awali shetani aliumbwa akiwa mwenye madaraka makubwa na aliishi katika maisha ya fahari kubwa sana. Tunaweza kuirejea nukuu ifuatayo kutoka katika maandiko matakatifu;

EZEKIELI 28

13 Ulikaa Edeni, bustani ya Mungu.
Ulipambwa kwa kila namna ya johari,
akiki, topazi, yaspi, zabarajadi, berili,
sardoniki, johari ya rangi ya samawati, almasi na zumaridi.
Ulikuwa na mapambo ya dhahabu.
Yote uliwekewa tayari siku ulipoumbwa.

14 Nilimteua malaika kukulinda,
uliishi katika mlima wangu mtakatifu
na kutembea juu ya vito vinavyometameta.

15 Uliishi maisha yasiyo na lawama,
tangu siku ile ulipoumbwa,
hadi ulipoanza kufanya uovu.

16 Ufanisi wa biashara yako
ulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi.
Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa,
mbali na mlima wangu mtakatifu.
Na yule malaika aliyekulinda
akakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.

17 Ulikuwa na kiburi
kwa sababu ya uzuri wako.
Uliharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.
Nilikubwaga chini udongoni,
nikakufanya kuwa kioja kwa wafalme.

Ipo sababu yenye kuamsha shahuku hii kubwa ya kwenda katika sayari hii nyekundu ya Mirihi. Lakini kubwa kuliko zote ni hiyo ya funguo za kuzimu kama inavyorejewa katika maandiko matakatifu;

Ufunuo wa Yohana 9

1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona bnyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.
2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

Screenshot_20220129-152334.jpg
Screenshot_20220129-151330.jpg
Screenshot_20220129-180015.jpg

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom